Ushirikina Kigoma: Mwanamke aliyefariki Oktoba 2018 na kuzikwa aonekana akiwa hai

Ushirikina Kigoma: Mwanamke aliyefariki Oktoba 2018 na kuzikwa aonekana akiwa hai

Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma limetoa ufafanuzi juu ya taarifa za Mwanamke mmoja wa miaka 40 Mkazi wa Kazegunga ambaye anadaiwa kuonekana November mwaka huu baada ya kufariki October 17,2018 wakati akijifungua Mtoto katika Hospitali ya Baptist iliyopo Halmashauri ya Manispaa Kigoma Ujiji na kuzikwa Kazegunga alipokua kaiishi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma Filemon Makungu amesema kuna matukio mawili ya Watu ambao wameonekana wakiwa hai ingawa Familia wamesema walifariki “Matukio haya tumeyafatilia yote na inatakiwa kuthibitisha kisayansi tumeshapeleka vipimo kwa Mkemia Mkuu bado hatujaletewa majibu tukiletewa tutatoa maelezo yaliyokamilika lakini kwa matukio haya mawili bado upelelezi tunaendelea nao kujua kwa kina zaidi ili kujua ukweli wa yule aliyefariki na huyu aliyeokotwa akiwa hai”

Mwezi November mwaka huu Familia ilisema Mpendwa wao huyo alionekana katika eneo la Ilagala Wilayani Uvinza ambapo miezi 11 iliyopita tukio kama hili la Mtu kufariki kisha kuzikwa na kuonekana tena lilitokea Kijiji cha Kandaga Wilayani UVinza Mkoani Kigoma ambapo pia mazingira yake yanahusishwa na imani za kishirikina kutumika kupoteza Watu na kuonekana tena baada ya muda mrefu kupita.

AyoTV mpaka sasa imeshawahi kuripoti matukio matano kama haya ya kusemekana Mtu amefariki na kuzikwa na baadaye Ndugu kudai wamemuona tena Ndugu yako akiwa hai, matukio hayo yametokwa mwaka 2018 Kasulu, mwaka 2020 Kasulu, mwaka 2021 Kasulu, mwaka 2022 Uvinza na mwaka 2023 Kigoma DC.

#MillardAyoUPDATES

View attachment 2839832
Waha wanaendekeza sana ushirikina, hata walimu wanalalamika kulogwalogwa ovyo na wenyeji
 
Mkuu, najua umewahi kusikia watu wanapaa na ungo ila hujawahi kuona. Ukiuliza uthibitisho hakuna.

A few month ago kuna mama alisema kajifungua jiwe na watu walisema wamemuona mtoto kageuka jiwe, walipoenda hospital hakuna record, bdae yule mama alisema mwenyewe ni uongo. Naamini ulisikia hii story.

Kwenye hii story ya huyu mtu kufufuka, kwanza huyu mama anaonekana anachangamoto ya akili kama kawaida ya watu wanaosingiziwa na kuamini uchawi karibu wote huwa na changamoto ya afya ya akili.

Nakuhakikishia hii story ukichimba vizuri ina loopholes kibao na zote zitakuja to surface in a wk or so. Sijaona mtu hata mmoja akihakikisha pasi na shaka huyu mama kuzikwa na mahali alipozikwa. Zote ni hearsay tu.

Umewahi kujiuliza kwanini media kubwa huwa hawaripoti kabisa hizi tetesi za kizwazwa? Kama mtu kafufuka unadhani isingekua habari kubwa dunia nzima.


View: https://www.youtube.com/watch?v=vi5ZbxntvpE&t=52s

Mkuu, mambo/taarifa zingine huwa zinafukiwa kwa masirahi mapana ya jamii na taifa kwa ujumla.

Unadhani serikali ikikiri kweli huyo mtu alikufa itakuwa ina'set precedent gani, nategemea waseme ni imani potofu tu na kitu kama hicho hakiwezekani.

Ila ukweli huyo hapo unamuona, awe na matatizo ya akili au timamu, hilo haliondoi ukweli kwamba ni mtu aliyezikwa tayari na mwisho wa siku kaonekana.

Sitarajii kwa mtu kama Millard katunga hadithi, sifikirii kama anaubavu wa kumshawishi kamanda wa police wa mkoa aseme hizo taarifa ni za kweli, issue ya kusubiri uthibitisho wa kiscience ni kufunika kombe tu.
 
Mkuu, mambo/taarifa zingine huwa zinafukiwa kwa masirahi mapana ya jamii na taifa kwa ujumla.

Unadhani serikali ikikiri kweli huyo mtu alikufa itakuwa ina'set precedent gani, nategemea waseme ni imani potofu tu na kitu kama hicho hakiwezekani.

Ila ukweli huyo hapo unamuona, awe na matatizo ya akili au timamu, hilo haliondoi ukweli kwamba ni mtu aliyezikwa tayari na mwisho wa siku kaonekana.

Sitarajii kwa mtu kama Millard katunga hadithi, sifikirii kama anaubavu wa kumshawishi kamanda wa police wa mkoa aseme hizo taarifa ni za kweli, issue ya kusubiri uthibitisho wa kiscience ni kufunika kombe tu.

Kwamba serikali inaficha watu wake wasijue wafu wanafufuka? Kwamba TZ haitaki kuutangazia ulimwengu kwamba ina uwezo wa kufufua wafu? Hili ni jambo la kheri kwanini serikali ifiche? Kwa maslahi gani hasa? I thought you're better than this.

Millard hajatunga ila anarusha ujinga uliotamalaki kwenye jamii ya watu wajinga kama alivyorusha habari ya mtu kujifungua jiwe, watu kupaa na ungo nk. Ujinga kama huu hauwezi ukuta kwenye vyombo vya habari vya kimataifa simply sababu wanajua ni ujinga hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza amini bila proof isiyoacha chembe ya shaka ambayo so far hakuna mtu kawahi kutoa proof zaidi ya hearsay stories na kulishana matango pori.

Mwaka juzi uliletwa uzi hapa jukwani wa mtu kufufuka huko huko Kigoma, walisema mtu huyo alikua Diwani. Diwani ni nafasi ya umma na taarifa zao ni public record, mimi niliuliza jina tu la huyo diwani sio kitu kingine. Tena niliahidi kutoa pesa taslim 500,000 TSH kwa mtu yeyote atayenipa jina tu. Sio mleta uzi au wajinga wengine walioamini walinipa jina hadi leo. Uzi huu hapa chini:

 
Kwa hiyo unashangaa mtu mmoja mmoja kufufuka kabla ya siku ya mwisho wa dunia kuja, kama wangefufuka wengi usingeshangaa? Hapo kwa huyo mwanamke kuna kufufuka kweli au ni mauzauza ya kishirikina? Sasa hapo polisi watatoa maelezo gani ikiwa serikali haiamini ushirikina?
Hapo ni mauzauza tu hakuna chakufufuka, alifufuka Yesu Kristo basi.
 
Back
Top Bottom