Ushirikina Kigoma: Mwanamke aliyefariki Oktoba 2018 na kuzikwa aonekana akiwa hai

Waha wanaendekeza sana ushirikina, hata walimu wanalalamika kulogwalogwa ovyo na wenyeji
 
Mkuu, mambo/taarifa zingine huwa zinafukiwa kwa masirahi mapana ya jamii na taifa kwa ujumla.

Unadhani serikali ikikiri kweli huyo mtu alikufa itakuwa ina'set precedent gani, nategemea waseme ni imani potofu tu na kitu kama hicho hakiwezekani.

Ila ukweli huyo hapo unamuona, awe na matatizo ya akili au timamu, hilo haliondoi ukweli kwamba ni mtu aliyezikwa tayari na mwisho wa siku kaonekana.

Sitarajii kwa mtu kama Millard katunga hadithi, sifikirii kama anaubavu wa kumshawishi kamanda wa police wa mkoa aseme hizo taarifa ni za kweli, issue ya kusubiri uthibitisho wa kiscience ni kufunika kombe tu.
 

Kwamba serikali inaficha watu wake wasijue wafu wanafufuka? Kwamba TZ haitaki kuutangazia ulimwengu kwamba ina uwezo wa kufufua wafu? Hili ni jambo la kheri kwanini serikali ifiche? Kwa maslahi gani hasa? I thought you're better than this.

Millard hajatunga ila anarusha ujinga uliotamalaki kwenye jamii ya watu wajinga kama alivyorusha habari ya mtu kujifungua jiwe, watu kupaa na ungo nk. Ujinga kama huu hauwezi ukuta kwenye vyombo vya habari vya kimataifa simply sababu wanajua ni ujinga hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza amini bila proof isiyoacha chembe ya shaka ambayo so far hakuna mtu kawahi kutoa proof zaidi ya hearsay stories na kulishana matango pori.

Mwaka juzi uliletwa uzi hapa jukwani wa mtu kufufuka huko huko Kigoma, walisema mtu huyo alikua Diwani. Diwani ni nafasi ya umma na taarifa zao ni public record, mimi niliuliza jina tu la huyo diwani sio kitu kingine. Tena niliahidi kutoa pesa taslim 500,000 TSH kwa mtu yeyote atayenipa jina tu. Sio mleta uzi au wajinga wengine walioamini walinipa jina hadi leo. Uzi huu hapa chini:

 
Hapo ni mauzauza tu hakuna chakufufuka, alifufuka Yesu Kristo basi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…