KAMA UTANI
Member
- Aug 25, 2023
- 6
- 0
Watanzania tuna ushabiki sana na pia hatupendi mtu mwingine azungumze mabaya wa kile wanachoamini wao hakina dhambi (kitakatifu) hata kama anaona kwa macho yake.Maeneo ambayo mitume na manabii walipelekwa ujue watu wake walikuwa ni wagumu sana kuelewa masuala ya Mungu muumba kwa kipindi hicho hasa ni bara Asia na maeneo ya karibu.Sisi kwenye uovu tuseme ukweli katika maeneo yote na siyo kushindana.Swala la ushoga siyo utamaduni mzuri kwetu,tukatae tu kwa nguvu ndugu zangu.Ameleta nani,ameanzisha nani,wakina nani wanaongoza sidhani kama itaondoa tatizo.Lakini dhambi Ina pande mbili:Upande wa kwanza ni wale wanaofanya dhambi hiyo binafsi, Upande wa pili ni wale wanaofanya na kushawishi wengine kufanya eidha kwa lazima au kushawishi kwa njia nyingne.TUPENDANE WATANZANIA NA TUUNGANE.