Ushuhuda: Biashara ya mchele ni ngumu mno!


huku tulipo tuna mchele tuna stock tokea ya mwaka 2019,2020 na 2021 (japo hii imesua sua)

hii 2019 ilikuwa komesha
 
Ninavyojuwa mimi hii biashara ni kama kumchinja Kobe ni ya timing.

Inabidi ununuwe mpunga uhifadhi ghalani kwako hukohuko mkoani, usubili bei ikae vizuri sometimes huna haja ya kuleta mchele Dar unawauzia hukohuko vijijini wanakuja wenyewe.

Kwa mtazamo wangu mtu mwenye mtaji wa million 10 ndio anaweza kufanya biadhara hii bila stress, maana kuna kipindi unahifadhi stock ghalani unapiga mishe nyingine ndogondogo kuzungusha pesa ya matumizi ili usile mtaji.
 
If you want to go somewhere it's best to find someone who has already been there...Hii ni moja ya kanuni moja nzuri katika biashara nakushauri uifuate.
Kabla ya yote napenda nikuambie ukweli tu hakuna biashara rahisi(easy money) kila biashara lazima ukubali kuwa mjinga kwa siku za mwanzo tena hii inabidi uwe unaweka katika akili yako.Biashara ni kama kuendesha baiskeli kwa mara ya kwanza lazima utaanguka lakini baada ya muda unakuwa kipanga.
Usikate tamaa endelea mwanga upo mbele
 
Ndio hivyo wengine tumeingilia biashara za watu
 
Nauchukua huu ushauri mkuu, lakini uhalisia biashara hii ya nafaka kuanza na mtaji kama huu ni stress na maumivu
 
Nilichojifunza pia biashara yoyote ile ni mtaji ukiwa na elimu husika ya biashara mtaji NI muhimu saana ni ngumu sana kuanza na laki 7 then uje ufikishe million 100 ni ngumu sana wakuu
Mtaji ukiwa mdogo sana unatakiwa pia uangalie na biashara ya kufanya maana sasa kama una laki 7 hapohapo ununue mzigo, uusafirishe, ulipie gharama mbalimbali, bado ukute na wewe unakula hapo hapo kwenye iyo laki 7, bado upate na faida juu... aisee inakua vigumu.
 
Ni ngumu sana mkuu, kwa idea yako ya biashara unafikiri nifanye nini kwa huo mtaji?
 
Ni ngumu sana mkuu, kwa idea yako ya biashara unafikiri nifanye nini kwa huo mtaji?
Nadhani kuna biashara zinazohitaji mitaji midogo ungeweza kuanza na hizo ili ukuze mtaji wako taratibu then baadae ndio uingie kwenye hiyo biashara ya mchele. Ukitafuta humu jukwaani kuna nyuzi nyingi zinatoa miongozo.
 
Kulima ndio umefeli kabisa
Siyo kweli...acha kutia mtu uoga kama uliwahi kuferi ni wewe,shamba lina maisha kuliko ajira nyingi kwa 80%. Mnachokosea ni kudhani shamba linamfaidisha mkulima kwa miaka miwili lakini kumbe ni la hasha
 
Wenye mitaji mikubwa ndio wanafaidika mkuu
Kwa soko la nje sawa lakini la ndani, hata uwe na mtaji mkubwa lakini kama huna store yako ya kuuzia bado ni mtihani!!kwani tatizo linaanzia kwa wenye store, unamuachia mzigo na bei yeye anakuja kukwambia bwana hii bei kwa sasa sokoni ni ngumu kwani kuna mchele mzuri zaidi ya huu bei yake ipo chini zaidi, unakubali punguza kidogo, yeye huko hapunguzi, ile inakuwa yake, mnaenda tena anasema bwana leo yameingia mawe hayo ni balaa, huu wako kwa bei hii hautauza!!wenye store zao sawa.kuna ubababishaji sana kwenye hii biashara na faida yake ni ndogo sana hivyo kidogo tu umeumia
 
Mkuu kwa congo mchele unapeleka uvira ama maeneo gani?
 
safi nimefika pale kwenye pwani ya uvira kwenye lile soko sijui na wewe unafnyia biashara yako hapo ndugu?
Ya ni soko la maendeleo hapo uvira, japo nilikuwa na mpango wa kufika hadi BUKAVU,
 
Ya ni soko la maendeleo hapo uvira, japo nilikuwa na mpango wa kufika hadi BUKAVU,
Safi sana siku nikianza mishe za congo nitakucheki Mdau vipi Mama Riziki unamfahamu aise maana kipindi kile ndiye nilikua nampelekea mzigo sijui anapatikana mpaka sasa pale sokoni?
 
Mkuu Kuna biashara ya karanga wengi hawajaijua ni mzr maduka ya jumla kwa Sasa ni 2900 mpaka 3000.maduka ya reja reja ni 3500.Nenda Dodoma karanga za kubangua na mkono ni 2200/za mashine ni 2000 mpaka 1900 Lete mjini then deal na maduka ya reja reja au nenda moja kwa moja kwa wamama wauza karanga fanya nao biashara .utarudi kunitafuta
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…