Ushuhuda: Hatimaye ametiki

Ushuhuda: Hatimaye ametiki

Hatimaye Ametiki(Based on true story)

Ilikua mwaka 2016 katika chuo cha elimu ya biashara(CBE) Tawi la Mbeya nilikuwa mwaka wangu wa pili nikichukua stashahada ya usimamizi wa biashara (diploma in Businesses administration). Nikiwa nimeketi kwa pembeni kipindi hicho ndo kuna wanafunzi wapya walio kua wanaripoti. Nilimuona binti mmoja ambaye alikuwa akitoka Eneo la utawala kufanya usajili lilikua ingizo jipya Chuo hapo, binti huyo yeye alikuwa mzuri mwenye kufanana na mabinti wa kimasai kulingana na mkao wake, tembelea pamoja na umbo na rangi yake.

Sikufuatilia sana nilimuona na kumfananisha na maasai.
Siku kadha kupita wakiwa wanaelekea siku za mwisho za Orientation binti huyo nilimuona amekaa peke yake sehemu nikaona si vyema kumuacha nikasigea karibu yake na kuanza mazungumzo japo kidogo.

Mimi: Mambo vipi sister

Yeye: Safi (Aliitikia salamu huku akiniangalia na kuonyesha nusu tabasamu nusu kuchukia kama nimevuruga mpango wake wa kukaa peke yake yaani sikumuekewa)

Mimi: samahani kwa kukuingilia je, itakuwa dhambi kwa mimi kukaa na wewe hapa?

Yeye: Hapana

Mimi: Samahani wewe ni mwenyeji wa Arusha eti

Yeye: Ndio mimi mwenyeji wa Arusha wilaya ya Karatu.

Nilimuuliza maswali hayo sababu akifanania na maasai. Nikaanza kwa kumuuliza Jina akagoma kunitajia, Nikaona hapa niende direct kuomba mawasiliano ikabidi nimfungukie unaweza nisaidia mawasiliano yako.
Yeye alikataa katukatu na kusema hawezi nipa Mawasiliano yake nilijitahidi kumdanganya akasema labda yeye achukue namba zangu nami bila hiyana nikamupatia.

Hapo tunapiga stori kidogo nikaachana nae nikawa nimemuacha amekaa. Siku zilipita ilikuwa nadra kumuona sababu lecture rooms tulitofautiana na wala hakuwahi nitafuta kwenye simu. Siku zikaenda kama mwezi mmoja yupo chuo nikaonana naye alikuwa amekaa alipenda kukaa peke yake mara nyingi nikamfata nikampasa salam akaitikia.
Nikauliza mbona kimya hata hukunitafuta akasema nitakutafuta muda bado haujafika. Basi nikamuuliza tena Jina akasema mda ukifika nitamfahamu alidai mda bado.

Tulipiga story kidogo akanyanyuka kuondoka nikamuuliza mbona unaondoka akasema anawahi kipindi nami nikamuacha.
Kama bahati CR wao alikuwa ni jamaa tulie fahamiana kwa mda mfupi sababu akitoka mkoa mmoja na mimi hivyo tulishare Kabila. Ilibidi nimtumie yeye kumfuata na kumueleza kua anisaidie kupata namba za binti fulani nikamuelekeza sifa za huyo binti ili ajaribu kupata mawasiliano yake, alisema atamtafta ili amfahamu. Baada ya siku kadhaa alisema amemuona sema hajapata kumfahamu Jina wala hajapata mawasiliano yake maana binti yupo serious sana.
Siku zikapita CR akasema amepata namba zake hivyo atanipatia.

Dahh kwakweli nilifurahi sana ilibidi nikomae na huyo CR ili nipate namba.
Siku moja nipo geto CR akanitumia namba 075XXXXXX4 Akaniambia Jina kanaitwa ka Adelina.

To be continued...
Uo ni undazkumtumia mwanaume mwenzqko kupata demu mfuate mwenyewe akizingua usiforce kashapta ngomq uyo kakuletea ww afu ww unajona mjanja
 
SHUHUDA: HATIMAYE AMETIKI (based on my true story) 2nd epsode

...Cr alinitumia namba za huyo binti pamoja na kutaja Jina lako hivyo hivyo nami nilishkuru kwa kupata namba za huyo binti aliye kua hataki mimi kua na mawasialiano yake. Ilinibidi nisiwe na haraka sana, Siku hiyo ilipita pasipo kumtafuta.
Siku iliyo fuata ilinibidi bora nimtafute maana wanasema ngoja ngoja huumiza matumbo.
Ikabidi nianze kufanya mawasiliano nayo kwa njia ya sms.
Mimi: Mambo
Kama ilivyo kawaida ya wadada wengi hasa wanao jiona na wasio penda mambo mengi ukimtafuta akiona namba ngeni lazima akufikishie kwenye kukuuliza kua wewe nani.
Yeye: Safi wewe Nani? Maana namba ngeni.
Maswali yalifululuzi kwa sms moja tu niliyo mwambie mambo. Nani sikutaka kufunguka Jina moja kwa moja nikaamua kutua vionjo.
Mimi: Bila shaka unanifahamu kwa maana mimi ni yule niliye kuomba namba hukutaka kunipatia, mimi ni yule niliye kuuliza juna hukutaka kuniambia, pia mimi ni yule uliye chukua namba yangu lakini hukutaka kunitafuta.
Nilimjibu kwa mfululizo huo ili asipate shaka ya kunijua mimi ni nani.
Kama ilivyo kawaida ya wadada hasa wanao jiona hawawezi sahau kabisa kuuliza maswali kama Namba yangu kakupa nani/Umetoa wapi.
Nami swali hilo akiniuliza namba nimetoa wapi? Nami nilimimpiga maneno kua nimeteseka sana hadi kupata namba yake, nikaongeza chumvi kua nimepata sehemu nyingi sana hadi kuipata, yaani nilimujaza maneno ili ajue huyo jamaa jaamua kweli.
Tulichati kidogo akaniuliza maswali mengi sana nami nikajibu kwa kuweka chumvi.
Baadaye kidogo akamalizia kwa kusema Asante kwa ushirikiano. Kwa kweli alinikata moto kabisa yaani kujitetea kote huko anakuja kusema asante kwa ushirikiano ina maana ndio Imeisha hiyo.
Nikaamua kumuaga na kumwambia nitamcheki mida, mtoto akakubali. Ilipo fika mida ya usiku nikamcheki
Alirespond vizuri nikamuulza maswali akajibu japo kwa nyondo jana kwamba hataki kuwe na mawasiliano baina yake na mimi. Ilibidi nikomae nae kibishi tu mpaka kieleweke.
Siku kadhaa zikapita nikiwa nachati nae ikabidi niombee kukutana nae akinihangaisha kabisa yaani hakutaka tukutane ananiuliza ninashida gani na kwanini niseme kwenye simu.
Kwakweli halikuwa lengo langu kusema ya moyoni kwa njia ya simu hivyo niliomba kukutana naye.
Yaani ilikuwa ni wajibu wangu kila Siku kumcheki kwa sms pamoja na kumpigia.
Siku zingine Alikubali kuonana nae ila mda ukifika anazungua tena.
Nilijitahidi kumbembeleza lakini alikataa katu katu. Lakini niliinyesha dalili zote za kumpenda.
Niliona nikichelewa sitampata kabisa kwahiyo ni bora nimfungukie Hata kwenye simu, Siku moja nikampigia simu ili nifunguke.
Akapokea simu yangu nami nikasema nimuelekeze, nikamuelekeza vitu vyote jinsi nilivyo mpenda since day one mpaka leo mtoto ikafika time yake ya kutoa majibu sasa...

To be continued...
 
Bible yenyewe inasema mshike sana elimu usimuache aende zake, sasa endelea kushika mambo mengine, afu wanawake wazuri wanaendelea kuzaliwa kila siku hata ukifika kazini huko utakutana nao! Unatafuta mama mzuri chuo na hata hauko tayari kuoa sasa si matumizi mabaya hayo😀
very true
 
Dogo ulikosea sana mwanamke siku ya Kwanza usianze na samahani pumbafu

First day ni ukauzu haswa mpaka akuogope, mwanamke akikuogopa ndo anakupa tension

Ulitudharirisha sana
 
Na hapo ujue alikuwa na mtu aliyekuwa kamchanganya

Yaani kumpata wewe kama ni kweli ni muda tu atakuacha labda ubadirike uwe mwanaume siyo kivulana
 
SHUHUDA: HATIMAYE AMETIKI (based on my true story) 2rd epsode

...Cr alinitumia namba za huyo binti pamoja na kutaja Jina lako hivyo hivyo nami nilishkuru kwa kupata namba za huyo binti aliye kua hataki mimi kua na mawasialiano yake. Ilinibidi nisiwe na haraka sana, Siku hiyo ilipita pasipo kumtafuta.
Siku iliyo fuata ilinibidi bora nimtafute maana wanasema ngoja ngoja huumiza matumbo.
Ikabidi nianze kufanya mawasiliano nayo kwa njia ya sms.
Mimi: Mambo
Kama ilivyo kawaida ya wadada wengi hasa wanao jiona na wasio penda mambo mengi ukimtafuta akiona namba ngeni lazima akufikishie kwenye kukuuliza kua wewe nani.
Yeye: Safi wewe Nani? Maana namba ngeni.
Maswali yalifululuzi kwa sms moja tu niliyo mwambie mambo. Nani sikutaka kufunguka Jina moja kwa moja nikaamua kutua vionjo.
Mimi: Bila shaka unanifahamu kwa maana mimi ni yule niliye kuomba namba hukutaka kunipatia, mimi ni yule niliye kuuliza juna hukutaka kuniambia, pia mimi ni yule uliye chukua namba yangu lakini hukutaka kunitafuta.
Nilimjibu kwa mfululizo huo ili asipate shaka ya kunijua mimi ni nani.
Kama ilivyo kawaida ya wadada hasa wanao jiona hawawezi sahau kabisa kuuliza maswali kama Namba yangu kakupa nani/Umetoa wapi.
Nami swali hilo akiniuliza namba nimetoa wapi? Nami nilimimpiga maneno kua nimeteseka sana hadi kupata namba yake, nikaongeza chumvi kua nimepata sehemu nyingi sana hadi kuipata, yaani nilimujaza maneno ili ajue huyo jamaa jaamua kweli.
Tulichati kidogo akaniuliza maswali mengi sana nami nikajibu kwa kuweka chumvi.
Baadaye kidogo akamalizia kwa kusema Asante kwa ushirikiano. Kwa kweli alinikata moto kabisa yaani kujitetea kote huko anakuja kusema asante kwa ushirikiano ina maana ndio Imeisha hiyo.
Nikaamua kumuaga na kumwambia nitamcheki mida, mtoto akakubali. Ilipo fika mida ya usiku nikamcheki
Alirespond vizuri nikamuulza maswali akajibu japo kwa nyondo jana kwamba hataki kuwe na mawasiliano baina yake na mimi. Ilibidi nikomae nae kibishi tu mpaka kieleweke.
Siku kadhaa zikapita nikiwa nachati nae ikabidi niombee kukutana nae akinihangaisha kabisa yaani hakutaka tukutane ananiuliza ninashida gani na kwanini niseme kwenye simu.
Kwakweli halikuwa lengo langu kusema ya moyoni kwa njia ya simu hivyo niliomba kukutana naye.
Yaani ilikuwa ni wajibu wangu kila Siku kumcheki kwa sms pamoja na kumpigia.
Siku zingine Alikubali kuonana nae ila mda ukifika anazungua tena.
Nilijitahidi kumbembeleza lakini alikataa katu katu. Lakini niliinyesha dalili zote za kumpenda.
Niliona nikichelewa sitampata kabisa kwahiyo ni bora nimfungukie Hata kwenye simu, Siku moja nikampigia simu ili nifunguke.
Akapokea simu yangu nami nikasema nimuelekeze, nikamuelekeza vitu vyote jinsi nilivyo mpenda since day one mpaka leo mtoto ikafika time yake ya kutoa majibu sasa...

To be continued...
"To be continued" Hovyo Kabisa👹😈😈
 
Uo ni undazkumtumia mwanaume mwenzqko kupata demu mfuate mwenyewe akizingua usiforce kashapta ngomq uyo kakuletea ww afu ww unajona mjanja
Watu tupo live na maisha hakuna ya kukata tamaa
 
Mtu atayechoka ataweka 'pozi' yeye mwenyewe...

Kuna tuliozoea kusoma hata kurasa 300 per day,sasa mambo ya inaendelea hadi unasahau episode iliyopita ilihusiana na nini inabidi unaanza upya kujikumbusha
🙏🙏🙏
 
Dogo ulikosea sana mwanamke siku ya Kwanza usianze na samahani pumbafu

First day ni ukauzu haswa mpaka akuogope, mwanamke akikuogopa ndo anakupa tension

Ulitudharirisha sana
Kweli kabisa mkuu 🙏🙏🙏 hilo nishajifunza
 
Na hapo ujue alikuwa na mtu aliyekuwa kamchanganya

Yaani kumpata wewe kama ni kweli ni muda tu atakuacha labda ubadirike uwe mwanaume siyo kivulana
Hahahah ashatiki
 
SHUHUDA: HATIMAYE AMETIKI (based on my true story) 2rd epsode

...Cr alinitumia namba za huyo binti pamoja na kutaja Jina lako hivyo hivyo nami nilishkuru kwa kupata namba za huyo binti aliye kua hataki mimi kua na mawasialiano yake. Ilinibidi nisiwe na haraka sana, Siku hiyo ilipita pasipo kumtafuta.
Siku iliyo fuata ilinibidi bora nimtafute maana wanasema ngoja ngoja huumiza matumbo.
Ikabidi nianze kufanya mawasiliano nayo kwa njia ya sms.
Mimi: Mambo
Kama ilivyo kawaida ya wadada wengi hasa wanao jiona na wasio penda mambo mengi ukimtafuta akiona namba ngeni lazima akufikishie kwenye kukuuliza kua wewe nani.
Yeye: Safi wewe Nani? Maana namba ngeni.
Maswali yalifululuzi kwa sms moja tu niliyo mwambie mambo. Nani sikutaka kufunguka Jina moja kwa moja nikaamua kutua vionjo.
Mimi: Bila shaka unanifahamu kwa maana mimi ni yule niliye kuomba namba hukutaka kunipatia, mimi ni yule niliye kuuliza juna hukutaka kuniambia, pia mimi ni yule uliye chukua namba yangu lakini hukutaka kunitafuta.
Nilimjibu kwa mfululizo huo ili asipate shaka ya kunijua mimi ni nani.
Kama ilivyo kawaida ya wadada hasa wanao jiona hawawezi sahau kabisa kuuliza maswali kama Namba yangu kakupa nani/Umetoa wapi.
Nami swali hilo akiniuliza namba nimetoa wapi? Nami nilimimpiga maneno kua nimeteseka sana hadi kupata namba yake, nikaongeza chumvi kua nimepata sehemu nyingi sana hadi kuipata, yaani nilimujaza maneno ili ajue huyo jamaa jaamua kweli.
Tulichati kidogo akaniuliza maswali mengi sana nami nikajibu kwa kuweka chumvi.
Baadaye kidogo akamalizia kwa kusema Asante kwa ushirikiano. Kwa kweli alinikata moto kabisa yaani kujitetea kote huko anakuja kusema asante kwa ushirikiano ina maana ndio Imeisha hiyo.
Nikaamua kumuaga na kumwambia nitamcheki mida, mtoto akakubali. Ilipo fika mida ya usiku nikamcheki
Alirespond vizuri nikamuulza maswali akajibu japo kwa nyondo jana kwamba hataki kuwe na mawasiliano baina yake na mimi. Ilibidi nikomae nae kibishi tu mpaka kieleweke.
Siku kadhaa zikapita nikiwa nachati nae ikabidi niombee kukutana nae akinihangaisha kabisa yaani hakutaka tukutane ananiuliza ninashida gani na kwanini niseme kwenye simu.
Kwakweli halikuwa lengo langu kusema ya moyoni kwa njia ya simu hivyo niliomba kukutana naye.
Yaani ilikuwa ni wajibu wangu kila Siku kumcheki kwa sms pamoja na kumpigia.
Siku zingine Alikubali kuonana nae ila mda ukifika anazungua tena.
Nilijitahidi kumbembeleza lakini alikataa katu katu. Lakini niliinyesha dalili zote za kumpenda.
Niliona nikichelewa sitampata kabisa kwahiyo ni bora nimfungukie Hata kwenye simu, Siku moja nikampigia simu ili nifunguke.
Akapokea simu yangu nami nikasema nimuelekeze, nikamuelekeza vitu vyote jinsi nilivyo mpenda since day one mpaka leo mtoto ikafika time yake ya kutoa majibu sasa...

To be continued...
2rd episode ndo nini
 
SHUHUDA: HATIMAYE AMETIKI (based on my true story) 3rd epsode
...Binti nilivyo maliza kumuelekeza ikabidi uwe wakati wake wa kutoa maamuzi.
Ukisikia siku ya kufa nyani miti yote huteleza ndo Siku ile sasa yaani mda mwingi nimefuatilia naongea naye na kuchati naye sasa wakati wa kutoa maamuzi ukifkiri na jinsi alivyokuwa anajibu kwa wakati huo namuelekeza nilijua fika hapa mkeka lazima utiki kulingana na mashambulizi na porojo nilizo kua nikimwambia.
Lakini binti majibu yake yalikuwa ni hapana yaani hawezi kua kwenye mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yeyote.
Nilijatahidi kumuelekeza zaidi binti alinikazia kabisa tena akasema nikiendelea kumfuatilia atakacho fanya sitakuja kusahau. Nami nilijitahidi kumuelewesha lakini akakaza mpaka Mawasiliano yakaisha hapo nikawa nimeambulia patupu.
Ilibidi nikomae nae kibishi tu mpaka kieleweke, nikawa nachati nae na kuongea naye mda mwingine namufuata tunabonga nae live.
Ikabidi niombe tena tuonane akawa kama anawleweka vile(uzuri wake kilicho nichanganya ni kuwa mda mwingine unawasiliana nae kama mpenzi mda mwingine kama adui).
Kwahiyo hayo yalinichanganya nisimuelewe kabisa, lakini nikaamua kukaza nikaamua kumuomba nafasi ya kukutana weekend akakubali akaniuliza sehemu gani kwa kua yeye kipindi hicho alikuwa anaishi majengo karibu na soko matola jirani na mitaa ya maendeleo, na ukilinganisha na mimi nilikuwa nakaa Uzunguni B. Hivyo ilinibidi nimwambie tukutane Garden ya mkoa aligoma akasema hapo hawezi labda sehemu nyingine, nikamuelekeza akakubali kua kesho tukutane ambayo ilikuwa siku ya j'mossi. Siku yenyewe ikafika nikamcheki akawa kimya tu, piga simu hapokei, tuma sms hajibu mpaka nikakata tamaa ilikuwa mida ya saa 9 alasili mpaka saa kumi jioni. Nilikata tamaa, Mara mida ya saa 11 jioni akanicheki yeye nikamwambia kuona akasema hawezi mda umeenda nikapiga porojo akagoma ikiwa imeshindikana.
Ikabidi niendelee kuhangaisha nae kama msemo mmoja usemao If you fail to convince, confuse them. huo msemo niliamua kuuapply yaani nikimuona amekaa namfata, akiwa anaelekea nyumbani namfata.
Kuna mda nilikuwa msumbufu zaidi hadi ikafikia mda mwingine ananiblock mda mwingine ndo ana unblock tena. Mbaya zaidi alinitesa kwa njia ya kuniblock harafu ananisumbua kwa kunitumia sms mara utateseka sana mara tusisumbuane yaani hapo mimi hata nikimujibu hawezi pata sms zangu.
Na mimi niliamua kumsumbua kwa kutumia namba zingine yaani naazima simu namchek iwe kupiga au sms ili ajue ni mimi. Maisha yakaenda kwa kusumbuana hivyo mda mwingine mawasiliano yanakuwepo mda mwingine ndio hivyo.
Kuna mda alinichukia kua mimi ni msumbufu, nakera,simuelewa na mubishi. Na ilikuwa kweli kabisa sema yeye aliyasababisha yeye.
Maisha yakaendelea hivyo hivyo kibishi.
Yaani ilikuwa semister ya kwanza hadi semister ya pili tunasumbuana.
Siku moja moja tukatibuana nae tukachati kwa majibu ya hovyo sana mpaka akawa kimya ilikuwa asubuhi, lakini ilipo fika mda wa saa8 mchana Mara nikaona sms yake ikinianza nami nikajibu kama ifuatavyo.
Yeye: today nakupa favor Si unataka kuonana na mimi.
Mimi: ndiyo
Yeye: lakini naishi mbali na chuo utaweza kuja?
Nami nikakubali kua popote naweza fika kikubwa anielekeze.
yeye: Panda daladala shukia darajani.
Wala sikujua ni darajani wapi huku moyo huamini Yaani mtu asubuhi tumetibuana harafu jioni hii anipe ofa.
Nikapiga moyo konde nikamuomba anielekeze darajani ya wapi nishukie.
Akaniekekeza kua nipande daladala za S/Kuu to Igawilo ndo akasema nishukie darajani. Nikaona nipande daladala maeneo ya Ujenzi ili kuelekea darajani kuonana na mtoto niliye kaa kumsubiri.

To be continued...
 
SHUHUDA: HATIMAYE AMETIKI (based on my true story) 4th epsode
... kabla sijaondoka najiandaa akanitumia sms akiniuliza kua nimefika wapi?. Yaani alizidi kunichanganya kichwani nikijiuliza amepatwa na nini?. Ila nikasema isiwe kesi nikajibu kwa kudanganya kuwa ndo nimepanda daladala wakati hata safari ya kwenda ujenzi kwa ajili ya kuchukua usafiri sijaanza. Ikabidi nielekee hapo kituo cha daladala Nikifa maeneo ya ujenzi kusubiri daladala, mda mfupi daladala ikafika nikapanda ili kuelekea kwa mtoto.
Nikiwa safarini hapo imefika mida ya saa 9 alasili, nilipo fika maeneo ya Sae nikamwambia nimekaribia kufika akaniuliza kua umefika wapi nikamueleza nipo Sae ndo naelekea Nanenane akajibu sawa.
Safari ikaendelea mpaka nikafika darajani ndipo nikashuka. Nikamutumia sms kua nimefika akawa kimya, nikatuma tena nyingine kama dk10 hivi hajarespond tu.
Hapo fika nikahisi kimeumana au ndo ameamua kunikomoa hivi Mara ndo nikaona sms yake ikijibu sawa.
Nikaamua ngoja nisubiri nikaelekea kwenye mgahawa flani jirani kujikinga na manyunyu kwa maana kulikuwa na manyunyu kidogo. Nipo nimetulia Mara paaaa!!!! Nikamuona mtoto anakuja kunichukua nikasema moyoni WOW hivi ni kweli? Nilijiuliza lakini ndio hivyo nikaamua kuvunga kwanza yeye hakuniona akafika mpaka darajani kituoni akachukua simu yake ili anitumie SMS nilikua namcheki ajaituma SMS yake akiniuliza nipo wapi?.
Mda huo nilikuwa nimejongea hadi kwake nikamshika bega, akageuka na kutabasamu kiaina na mimi moyoni ❤️ nikasema fantastic.
Nikamuuliza unanipeleka wapi kukaa na wewe huku akinitembeza akidai kua yeye si mwenyeji maeneo hayo ndo amekuja karibuni kwahiyo hajui pa kunipeleka, ila tuliongea huku tunatembea akawa analeta utani kua au anioeleke nyumbani kwao (huku aki smile kiaina😜😜😜na kucheka)
Nilikubali nae alisema unataka wanishangae kua nina tabia gani yaani nimpeleke mvulana kwetu si watasema mtoto hana adabu. Alisema hayo akisema bora hata ingekuwa nyumbani kabisa, leo hii nikuoekeke kwa ndugu?🤣🤣🤣.
Tulitembelea nae juu ya reli ikafika sehemu tukaketi tukapiga story nyingi tunafurahi wote akaniuliza vipi ulikuwa huamini kama ndo nimeamua kuonana na wewe?
Nami nikasema yaani hata sikuamini kama ndo wewe uliye nitumia sms na hata nilivyo kuja ulivyo chelewa kurespond sms na kuchelewa kufika nikajua ndo kabsa nimepigiwa.
Alicheka sana tabasamu kama lote, tulipiga story huku treni zikipita. Tulipiga story mara mvua ikashuka acha tulowane nami nikamwambia yaani tumekuwa kama wahindi hizi baraka ujue.. tulitafuta eneo ili kujistiri na mvua tukapata nyumba fulani ilikuwa imejengwa tukaingia kujikinga hapo.
Tukiwa tumelowana yeye kama bahati alikuwa amevaa sweta nami sikuwa na sweta nilikua na T-shirt tu. Alinipa pole nami niliitikia, alianza utani kama mtu ambaye tupo kwenye mahusiano mara ajaribu kuvua sweta anipatie, mara ajaribu kuniambia njoo tujifunike wote. Kwakweli lilifrahia hali hiyo, niliomba japo nipige nae picha ya ukumbusho Lakini aligoma na kuniambia nisjali ipo siku tutapiga picha mpaka tuchoke, mda ulienda sana kama usiku ulijaribu kuingia akaomba tuondoke nilimwambia natamani sana kukaa nae, alisema pia ipo siku tutakaa mpaka tuchokane.
Ilimbidi anisindikize Kurudi nyumbani tukafika hadi darajani ili mimi niondoke.
Bila kusahau siku hiyo kila neno moja au hatua moja inaambatana na utani aliniambia au tuondoke wote harafu mimi nitarudi siku nyingine. Nilikubali lakini ilikuwa sehemu ya utani, niliondoka na kumuaga nikamuacha nilipo fika nyumbani nikamwambia mimi nimefika salama nae alijibu wala usijali.
Mawasiliano yakaendelea lakini sikutegemea kama huyo binti uamuzi wake ulikuwa kama jinsi alivyo niambia katika chatting.

To be continued...
 
Back
Top Bottom