Ushuhuda kutoka kwa wanandoa waliowahi kuachana, hasa mliokuwa na watoto mkaamua kuacha kila kitu na kuanza upya

Poleh mpenzi
Ndio mana heri kuongea na 'professional' ambae unaweza kufunguka ya moyoni without the fear of being judged.,na atakusaidia utoke hapo uende mbele

Naomba nikupe PM contacts za one therapist i know
Just try mpenzi.,coz sometimes moyo unashindwa kubeba vitu
 
Kwakweli kuelezea kila kilichotekea nitareaveal identity za watu...ila kikubwa ni usaliti uliovuka mipaka..na yaliyotokana na usaliti ndio mazito zaidi...naombeni msaaada juu ua uzoefu wenu...mimi na mume wangu hatuwezi kurudi kama mwanzo...
Pole sana, usaliti ni tatizo kubwa na halipaswi kuvumiliwa haswa kama ni jambo linalo jirudia, ushauri wangu :

1. Ondoka nyumbani ili upate utulivu wa akili na hisia
2. Shirikisha wazazi, wasimamizi wa ndoa na ikibidi viongozi wa dini watakusaidia mawazo na faraja
3. Tafuta Wataalam wa saikolojia watakusaidia ushauri
3. Kama mkitengana ni lazima watoto wataathirika, hili wanasheria watakupa utaratibu wa kufuata

Kimsingi hupaswi kuumia peke yako, unahitaji msaada wa ndugu, marafiki na wengine ili wakusaidie kulibeba na kukushauri
 
Mbona mahakamani inawezekana kabisa na ni rahisi unless mmoja awe hataki, napo kama mmoja hataki mtapewa muda wa kutafakari maamuzi yenu then mrudi tena mahakamani.

Tafuta hakimu mahakama ya mwanzo muelezee shida yako atakwambia nini cha kufanya.

Pia unaweza kuondoka hapo mnapoishi, ukarudi nyumbani au ukapanga chumba, kama unahofia watoto unaondoka nao, unaenda kuanza maisha upya, japo sio rahisi ni strong woman tu ndo anaweza hii kitu
 
Kwakweli kuelezea kila kilichotekea nitareaveal identity za watu...ila kikubwa ni usaliti uliovuka mipaka..na yaliyotokana na usaliti ndio mazito zaidi...naombeni msaaada juu ua uzoefu wenu...mimi na mume wangu hatuwezi kurudi kama mwanzo...
Achaneni tu. Time heals. Kuliko watoto kukua kwenye nyumba ya ugomvi kila siku bora muachane au mnataka mpaka mpigane vitu vizito vichwani?
 
Tafuta shughuli ya kufanya ili ujikeep busy, shughuli yoyote hata kulima bustani pembeni ya nyumba ukapanda mboga mboga, au biashara yoyote tu itakayokufanya uamke alfajir na kurudi jioni. Hii pia ni tiba
 
Uamuzi unao wewe.
Kuna dada yangu mmoja alikua kwenye ndoa yenye mateso kibao, na yeye alihofia kuondoka kwenye hiyo ndoa kwa kuwaza mustakabali wa watoto wao (walikua wamejaliwa watoto 4, ndoa yao ilikua na miaka 12). Mwisho wa siku alikuja kufariki kwa ugonjwa wa HIV/AIDS. Akawaacha duniani hao watoto ambao alikua anahofia kuondoka kwenye ndoa kwa ajili yao. Mume ambae ndie alimuambukiza bado yupo pia anadunda.

The bottom line is, "Uamuzi ni wa kwako". Kuanza upya inawezekana ila ni pale tu wewe utakapoamua na kuamini inawezekana.
Kuna mtu aliwahi kusema, "whether u believe you can or you cant, you are right."
Tuliza akili ufikiri kwa kina ni nini hasa unakitaka, halafu fanyia kazi maamuzi yako.
kissgarage
 
Njoo inbox hutajuta kwa ushauri! U will experience joyfully moment!

Lakini Kama bado unampenda huyo bonge la bwana! Kama mmejenga gawaneni upande kila MTU aishi upande wake! Lakini Kama hilo huwezi! Jipe muda, Rudi kwenu Kijijini Kama likizo ya matazamio! Hili litampa muda huyo mwanaume kuona umuhimu wako, Kama atakufata kijijini msamehe tibia donda songa mbele; asipokuja kukufuata Kijijini hiyo transition period itakupa majibu kuwa hupendwi!

Kwahiyo utakuja kuomba talaka!

Note; Wakati wakuondoka kwenda kijijini usioneshe kuwa unataka talaka, coz jamaa atauza kila kitu afilisike ghafla ili mje kugawana vichache ambavyo havitakusaidia.
 
Kumsitiri nini? Amefanya jambo la aibu ya au
aina gani lisolosemeka?
 
@kadogooCate mahakamani ni mchakato kidogo sio suala la simple simple.
 
@kadogooCate mahakamani ni mchakato kidogo sio suala la simple simple.
Mkuu suala la talaka ni la kisheria, huwezi kukwepa mchakato wake na kwa kweli ni jambo linalochukua muda na linaumiza hisia na hata uchumi, mleta mada anahitaji kupata ushauri wa kumuandaa kisaikolojia kama kweli amedhamiria kudai talaka
 
Kwa umri nilionao.... Nimekuja kugundua.... Ukijaribu kummiliki Mwamamume.... Utaumia sana kihisia, kimwili, kisaikolojia, kimatendo, kifikra.... Utaumia Kila Kona. Utakuwa mtu wa mawazo na kununa muda wote. Nimeacha kabisa hii TABIA.

Umemfumania mumeo na mwanaume nini? Maana sijui kama kuna kubwa zaidi ya hilo
 
[emoji3516]
Wewe tulia wewe -
Huna hoja.

Hakuna suluhu inapatikana kwa kufichaficha taarifa za msingi.

Mtoa mada, tumia codes kuwasilisha tukio,
Ili malejendari tuliowahi kutalikiana zaidi ya mara mbili tukupe uzoefu.
 
Si wanasemaga ndoa ya Kikristo ndiyo ndoa ngumu kuvunjika? Nadhani hujawa serious ndoa ya mkataba ukikomaa mahakamani rufaa zako tatu tu unachomoka unakuwa huru.

Ila pole sana!
 
Pole my dear ila you have to be strong Sana Kama umeona haiwezekani Tena beba wanao ondoka pigania furaha Kuna watu wanaishi kwenye magereza si ndoa Mimi kiukweli kitu chochote kitakachotaka kuniharibia furaha yangu nakiondoa haraka Sana kwenye maisha yangu napenda kuwa happy siwezi kukaa kwenye ndoa ya mateso never
 
Usuluhishaji bora wa ndoa ni muhimu sana mke na mume wote wateme nyongo zao bila kuficha kitu kwenye kikao chao wenyewe kama wanandoa.

Na mara nyingi mkishindwa kuafikiana basi mlipeleke kwa kiongozi wa imani yenu, mkishindwana hapo mlipeleke kwa wazee wa pande zote mbili au mahakaman.

Binafsi mara kadhaa ndoa yangu inapitia misuguano kadha wa kadha ila namshkuru Mungu huwa tunamalizaga wenyewe mimi na mama watoto hasa kila mmoja huwa muwazi na kufunguka yaliyo moyoni kwa lengo la kutafuta nini hasa chanzo cha tatizo na huwa suluhu inapatikana.

Hivyo basi kukupa msaada kwa unayopitia hata ukituelezea hapa itakua tumepata malalamiko ya upande mmoja tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…