Ni ngumu saana kurudisha imani ila ni ngumu zaidi kuanza upyaaaa hasa kama watoto wako kati yenu, waweza jidanganya mwaka ama miwili ila inafail....sikushauri hata kidogo take ur time, heal and all shall be well, wanaume ni walewale na wanawake ni walewale...kubwa duaaa!!!Nawasalimu sana ndugu wana JF.
Kwakweli lengo la ndoa ni kuishi pamoja kwa uaminifu na upendo na kulea familia pamoja.
Nafaham humu kuna watu wenye calibre tofauti na uwezo wa hali ya juu kupambanua mambo kutokana na experience...
Naomba experience yenu, je ilikua rahisi kuanza upya? Kwenda mahakamani kutoa talaka rasmi imeshindikana kabisa..ninachotaka ni kutengana kwa muda napo imeshindikana..hapo more than three children kwenye ndoa wapo involved, ten years na wengine below .simchukii kabisa mume lakini forgiving and forgetting what happened nashindwa kabisa..imani haipo Yarabi tena...nimekata tamaa kabisa...
Imefikia kipindi natafuta kazi mikoani ili nipone moyo...jamani wenzangu mliwezaje...sijashare na ndugu yangu hata mmoja....nikiwaeleza kila kitu watamchukia na they will never forgive him...
Nimeamua kumstiri mume wangu..sijaandika kila kitu ila baadhi yenu ni wanaume ila mngeumia sana na kutoa chozi...ndoa yetu ni ya serikali...naomba experience yenu especially kwa nyie mliokua na watoto mkaamua kuacha kila kitu na kuanza upya..
Bottom line zimwi likujualo halikuli likakwishaaa.....