Ushuhuda kutoka kwa wanandoa waliowahi kuachana, hasa mliokuwa na watoto mkaamua kuacha kila kitu na kuanza upya

Ushuhuda kutoka kwa wanandoa waliowahi kuachana, hasa mliokuwa na watoto mkaamua kuacha kila kitu na kuanza upya

Nawasalimu sana ndugu wana JF.
Kwakweli lengo la ndoa ni kuishi pamoja kwa uaminifu na upendo na kulea familia pamoja.

Nafaham humu kuna watu wenye calibre tofauti na uwezo wa hali ya juu kupambanua mambo kutokana na experience...

Naomba experience yenu, je ilikua rahisi kuanza upya? Kwenda mahakamani kutoa talaka rasmi imeshindikana kabisa..ninachotaka ni kutengana kwa muda napo imeshindikana..hapo more than three children kwenye ndoa wapo involved, ten years na wengine below .simchukii kabisa mume lakini forgiving and forgetting what happened nashindwa kabisa..imani haipo Yarabi tena...nimekata tamaa kabisa...

Imefikia kipindi natafuta kazi mikoani ili nipone moyo...jamani wenzangu mliwezaje...sijashare na ndugu yangu hata mmoja....nikiwaeleza kila kitu watamchukia na they will never forgive him...

Nimeamua kumstiri mume wangu..sijaandika kila kitu ila baadhi yenu ni wanaume ila mngeumia sana na kutoa chozi...ndoa yetu ni ya serikali...naomba experience yenu especially kwa nyie mliokua na watoto mkaamua kuacha kila kitu na kuanza upya..
Kuachana/kutengana imeshindikana kutokana na nini? Basi muishi nyumba moja ila kila mtu kivyake kama suala ni kulea watoto na kuwekeana siri.
Uwe na msimamo, hakuna unyumba, msije wote kufa kwa magonjwa muwaache watoto yatima.
 
Kwakweli kuelezea kila kilichotekea nitareaveal identity za watu...ila kikubwa ni usaliti uliovuka mipaka..na yaliyotokana na usaliti ndio mazito zaidi...naombeni msaaada juu ua uzoefu wenu...mimi na mume wangu hatuwezi kurudi kama mwanzo...
Kwamba mke kagonga mdogo wako hadi katia mimba ama ishu ni nini?
 
Waliomwelewa mtoa mada hawajatoa ushauri wowote,ambao hatujamuelewa kidogo tumejitahidi kubalance equation,

Hata hivyo napenda kukushauri hivi, amani ya moyo wako ni kitu cha Kwanza katika maisha, fanya kike kinachoupa amani moyo wako.
 
Kwakweli kuelezea kila kilichotekea nitareaveal identity za watu...ila kikubwa ni usaliti uliovuka mipaka..na yaliyotokana na usaliti ndio mazito zaidi...naombeni msaaada juu ua uzoefu wenu...mimi na mume wangu hatuwezi kurudi kama mwanzo...
Msome mtu anaitwa iddy makengo fb utagundua tatizo lako ni dogo
 
Ni ngumu sana kushauri kitu ambacho hukijui, Ila process ya kuvunja ndoa nenda mahakama ya mwanzo fasta
 
Nawasalimu sana ndugu wana JF.
Kwakweli lengo la ndoa ni kuishi pamoja kwa uaminifu na upendo na kulea familia pamoja.

Nafaham humu kuna watu wenye calibre tofauti na uwezo wa hali ya juu kupambanua mambo kutokana na experience...

Naomba experience yenu, je ilikua rahisi kuanza upya? Kwenda mahakamani kutoa talaka rasmi imeshindikana kabisa..ninachotaka ni kutengana kwa muda napo imeshindikana..hapo more than three children kwenye ndoa wapo involved, ten years na wengine below .simchukii kabisa mume lakini forgiving and forgetting what happened nashindwa kabisa..imani haipo Yarabi tena...nimekata tamaa kabisa...

Imefikia kipindi natafuta kazi mikoani ili nipone moyo...jamani wenzangu mliwezaje...sijashare na ndugu yangu hata mmoja....nikiwaeleza kila kitu watamchukia na they will never forgive him...

Nimeamua kumstiri mume wangu..sijaandika kila kitu ila baadhi yenu ni wanaume ila mngeumia sana na kutoa chozi...ndoa yetu ni ya serikali...naomba experience yenu especially kwa nyie mliokua na watoto mkaamua kuacha kila kitu na kuanza upya..
Sikunyengine. Unasajili ID mpya alaf unaandika mwandiko tofaut na ID yako then unafunguka yote kwa kuhadithis kama RFK ako,ndio kakuambia anapitia hayo majanga....ungepata ushauri murua kbs....
 
tangu awali nilikwambia kuwa huyo ulie nae ni jini makaba....mwaka na zaid unaumia na upo na huchukuo hatua!!?
 
Ukisema mumeo hapendi communication mimi naweza kukushauri kupitia hiyo hiyo kauli yako Moja..

You mess with his ego.Kama kuna kitu kinavunja ndoa mapema nakufanya sisi wanaume tuanze kufanya matukio ya kutosha bila kujali hili wala lile ni kucheza na ego zetu...

Mi naweza kukushauri wewe kidogo tu ujue wapi ukikosea na kwanini mwanaume kaja kuwa wa ajabu ajabu ingawa siwezi jua km alikuwa hivyo toka mwanzo

Kauli na matendo kuna kauli ukiongea mbele ya mwanaume inaweza kumuuma sana to the point mpk ukavunja ndoa yako kabla ya kuvunjika rasmi cha ajabu ni wanaume wachache sana Wapo tyr kusema wapi ego zao zilikuwa attacked utaona anakupiga matukio hakujali tena anafanya vitu ambavyo mwanzo alikuwa hawezi kufanya,HATAKI muliongelee sababu hata akikuelezea anahisi utadharau kitu anachokwambia utaona ni gubu lake tu

Nakupa mfano hai,kuna jamaa yangu mmoja alikuwa mtu poa sn mixer kuweka familia yake kwenye DP sasa ndoa ikamkubali akanenepa sana akawa na bonge la kitambi sasa siku tumeenda kula kwake akawa hajashiba akaomba mkewe amuongezee chakula,mkewe akalopoka we nae unapenda kula sana chakula chote kile ndo mana unatumbo km Mimba cheki wenzako hujisikii vby mume wangu???

Mimi bwana namjua mshikaji vzr sababu ni mtu wangu km hata hajaoa na navyomjua jamaa hawezi utani ni mwepesi wa kujaa sumu.Kwa ile kauli mbele yetu moja kwa moja,nilijua jamaa kaumia sana tena sana basi chakula kikaja akala vijiko kadhaa akasema najisikia nimeshiba...

From that day,jamaa alibadilika kbs akawa mlevi mbwa,anatembea na mabaamedi sasa akilewa alikuwa anarudi kauli moja hivi mke wangu anasema mimi natumbo kama mimba,nimemfanyia vingapi yule mwanamke mimi..

Sasa imagine watu wanataka kusuluhishwa

Mwanamke atasema mume wangu kabadilika kawa malaya,mlevi ananitukana hajali familia.

Mwanaume hata sema kitu sababu ana grudge utasikia nitajirekebisha ila moyoni anasema huyu mbwa ananiambia mimi na tumbo km mimba plus akituchek rafikiz ake ni kama tunamkumbusha kauli yake mkewe kwamba ona wenzako...KAMWE hawezi kusema kauli hiyo ndo imembadilisha ila in fact ni kauli hiyo ambayo mwanamke pengine aliongea kwa masihara tu

Wanaume tuna ego issue ukiona ugomvi mwanaume hataki muuzungunzie,mwanamke kumbuka tu kauli gani ukiongea na tendo gani ukitenda ambalo kwakujua au kutokujua ulikugusa ego..

Mwanaume anakuwa na hasira na wewe lkn hawezi kukwambia ulipokosea sababu utahisi labda ni upuuzi lkn moyoni anawaka moto sasa unataka mwanaume aseme nimekuwa malaya sijali familia sababu mke wangu aliniambia mbele ya marafiki zangu nina tumbo km mimba????nosense hawezi katuuuuu atakubali yameisha mkiondoka matukio tu

Wanawake utawasikia ‘upo lafu km huna hela’ ‘yaani wewe umezubaa kweli’ ‘cheki wanaume wenzako wanavyopambana’ ‘kama hujui kuchagua zawadi bora unipe hela nikanunue mwenyewe’ ‘we nae wanakuchezea sababu umezubaa sana’ ‘cheki alivyomuoga’ ‘umelegealegea sana na wewe’

Ndugu yangu hizo hapo juu zilivyo za kijinga hivyo hivyo ukizirudia rudia kwa mwnaume ambaye ana big ego niamini mimi unaweza kuvunja ndoa,Niamini mimi sababu ni mwanaume najua .
 
Labda wew mwanamke nkushauri , Mwanaume aachwi kwasababu za usaliti.
Labda ulete Hoja nyingne . KUvunja Ndoa utaleta matatzo makubwa sana sana sio kwako bali kwa hiko kizazi chako ktakuja poteza muelekeo maisha
NB:-katk familia yetu wa kambo aliacha na baba ila shida wanayopata watoto n kubwa zaid hadi mama mdogo anaona bora yeye angelivumilia

Usizan wew unaptia magumu yawez kuw kwa wengne ni madogo ni jinsi unavyoyapokea katk Akili yako.
 
Back
Top Bottom