Ushuhuda kutoka kwa wanandoa waliowahi kuachana, hasa mliokuwa na watoto mkaamua kuacha kila kitu na kuanza upya

Dah!
Poleni sana.
Hakuna jambo rahisi, hakuna kukata tamaa na hakuna kuogopa. Ukiamua jambo, basi fanya tu na utasonga mbele. Kumbuka tu, katika kila uamuzi kuna gharama ikiwemo watu kutokukuelewa.

Nini ushauri wangu kwako kwa sasa?
Jipe muda zaidi, subiri na tafakari. Usijaribu kulifanya hili jambo kama la dharula. Vuta subira kwanza, baada ya muda ndio uamue (kuendelea kuishi pamoja au kuachana). Time heals&answers.
 
Naunga mkono
 
Kwamba tunamuuliza ili tuanze kumnanga!!!
Mbona una mtizamo hasi sana,
 
You need to speak up honey. Use your anonymity to your advantage so you can get rid of the weight in your heart and thus set off healing.

Usiogope, hamna jipya chini ya jua. Believe me, hakuna utakachopitia ambacho Ni geni duniani. So Acha uoga.

What is eating you up?
 
Uzito unakujaga pale ambapo hakuna communication kwenye ndoa. If the two of you cannot sit down to talk about your problems then it is very difficult to solve problems in your marriage.
 
Hapana. Nilivyoona Ni kwamba huyu Dada anampenda mume wake. Na mume ni first offence Ila ni kubwa kiasi. Simshauri asepe kwa Sasa. Forgiveness heals. But first we need to know just what the issue is.
 
I pray that she does not come to your inbox!
 
Kwakweli kuelezea kila kilichotekea nitareaveal identity za watu...ila kikubwa ni usaliti uliovuka mipaka..na yaliyotokana na usaliti ndio mazito zaidi...naombeni msaaada juu ua uzoefu wenu...mimi na mume wangu hatuwezi kurudi kama mwanzo...
Trust is like a broken glass. Once broken it cannot be the same again. But that does not mean that forgiveness cannot play it's part. People change... If he is cooperative you can go to therapy don't give up just yet.
 
Inawezekana upo sahihi but kumpa mtu ushauri bila kujua kilichotokea sio sahihi. Mfano anaposema usaliti dunia ya sasa imechafuka huwezi jua nature ya usaliti. Kuna usaliti wa kusamehe Kuna usaliti wa kusepa hapo hapo because lazima itakuwa na negative impact kwa watoto.

Anatakiwa achukue advantage ya anonymity yake ya kutojulikana humu asafishe moyo wake. In talking there is alot of healing.

I have experience in this. Talking is the best therapy and healing starts from this.
 
Kwa kifupi huenda umeruka matope unaelekea kuogelea kinyesi. Ukiwaza sana chanzo cha mtu kuvunja mahusiano ni ubinafsi, unajiwazia mwenyewe na kusahau kuwa wewe ni sehemu ya furaha ya watoto wako. Kwanini usitulie kwa muda ndani ya ndoa yako hadi maumivu yaishe?

Jipe muda...huenda uvumilivu wako utampa deni mumeo akabadilika, uendako hata uolewe maadam umeacha wanao huwezi kufurahia chochote. Kufa na wanao
 
Una roho ngumu kwanini unavunja ndoa ya watu
Furaha ndio kila kitu. Mimi mwenyewe ndoa imenishinda. Nimesepa na wanangu na nina furaha acha kabisa. Si kauliza tulio na uzoefu. Ndio nimempa uzoefu. Wanaume wa bongo wenyewe full michepuko, maugomvi. Bora kuwa mwenyewe kuliko kwenye ndoa iliyojaa masikitiko.
 
Huwa napata wakati mgumu sana ninaposikia watu waliooana na kuzaa, halafu mmojawapo anaona kuachana ndiyo jawabu la matatizo yaliyojitokeza kati ya huyo mume na huyo mke. Nilitegemea kuwa kama mmezaa basi fikra kubwa ingekuwa kufikiria hatma ya maisha ya hawa mliowazaa bila ridhaa yao.

Inanipa shida zaidi kama watu hawa wana elimu ya kutosha, wanaenda kanisani au msikitini. Na mwisho huwa nahisi yeyote anayemlalamikia mwenzake aghalabu naye ana ushetani wake ambao unamwongoza kumshambulia mpambe wa shetani wa mwenzie. Elimu, Mungu na wanajamii wakusaidie, utavuka hayo mapito.
 
Sioni sababu ya kutowaambia ndugu zako machungu unayopitia ndani ya ndoa yako. Kama watamchukia kwa matendo yake mabaya aliyokufanyia hadi kutaka kuikimbia ndoa so be it! Wa kulaumiwa ni yeye na si wewe. Waite ndugu zangu uwaeleze kila kitu na kuwaomba ushauri nini ufanye. Wala usichelewe kuwaambia ndugu zako.

 
Kuna ukweli unauficha ambao tungeanzia hapo..sasa ukisema mengine huwezi sema maana yake ushauli hautakusaidia chochote kwa sababu hautakidhi yote kulingana na uliyo yaficha kuyasema hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…