Ukisema mumeo hapendi communication mimi naweza kukushauri kupitia hiyo hiyo kauli yako Moja..
You mess with his ego.Kama kuna kitu kinavunja ndoa mapema nakufanya sisi wanaume tuanze kufanya matukio ya kutosha bila kujali hili wala lile ni kucheza na ego zetu...
Mi naweza kukushauri wewe kidogo tu ujue wapi ukikosea na kwanini mwanaume kaja kuwa wa ajabu ajabu ingawa siwezi jua km alikuwa hivyo toka mwanzo
Kauli na matendo kuna kauli ukiongea mbele ya mwanaume inaweza kumuuma sana to the point mpk ukavunja ndoa yako kabla ya kuvunjika rasmi cha ajabu ni wanaume wachache sana Wapo tyr kusema wapi ego zao zilikuwa attacked utaona anakupiga matukio hakujali tena anafanya vitu ambavyo mwanzo alikuwa hawezi kufanya,HATAKI muliongelee sababu hata akikuelezea anahisi utadharau kitu anachokwambia utaona ni gubu lake tu
Nakupa mfano hai,kuna jamaa yangu mmoja alikuwa mtu poa sn mixer kuweka familia yake kwenye DP sasa ndoa ikamkubali akanenepa sana akawa na bonge la kitambi sasa siku tumeenda kula kwake akawa hajashiba akaomba mkewe amuongezee chakula,mkewe akalopoka we nae unapenda kula sana chakula chote kile ndo mana unatumbo km Mimba cheki wenzako hujisikii vby mume wangu???
Mimi bwana namjua mshikaji vzr sababu ni mtu wangu km hata hajaoa na navyomjua jamaa hawezi utani ni mwepesi wa kujaa sumu.Kwa ile kauli mbele yetu moja kwa moja,nilijua jamaa kaumia sana tena sana basi chakula kikaja akala vijiko kadhaa akasema najisikia nimeshiba...
From that day,jamaa alibadilika kbs akawa mlevi mbwa,anatembea na mabaamedi sasa akilewa alikuwa anarudi kauli moja hivi mke wangu anasema mimi natumbo kama mimba,nimemfanyia vingapi yule mwanamke mimi..
Sasa imagine watu wanataka kusuluhishwa
Mwanamke atasema mume wangu kabadilika kawa malaya,mlevi ananitukana hajali familia.
Mwanaume hata sema kitu sababu ana grudge utasikia nitajirekebisha ila moyoni anasema huyu mbwa ananiambia mimi na tumbo km mimba plus akituchek rafikiz ake ni kama tunamkumbusha kauli yake mkewe kwamba ona wenzako...KAMWE hawezi kusema kauli hiyo ndo imembadilisha ila in fact ni kauli hiyo ambayo mwanamke pengine aliongea kwa masihara tu
Wanaume tuna ego issue ukiona ugomvi mwanaume hataki muuzungunzie,mwanamke kumbuka tu kauli gani ukiongea na tendo gani ukitenda ambalo kwakujua au kutokujua ulikugusa ego..
Mwanaume anakuwa na hasira na wewe lkn hawezi kukwambia ulipokosea sababu utahisi labda ni upuuzi lkn moyoni anawaka moto sasa unataka mwanaume aseme nimekuwa malaya sijali familia sababu mke wangu aliniambia mbele ya marafiki zangu nina tumbo km mimba????nosense hawezi katuuuuu atakubali yameisha mkiondoka matukio tu
Wanawake utawasikia ‘upo lafu km huna hela’ ‘yaani wewe umezubaa kweli’ ‘cheki wanaume wenzako wanavyopambana’ ‘kama hujui kuchagua zawadi bora unipe hela nikanunue mwenyewe’ ‘we nae wanakuchezea sababu umezubaa sana’ ‘cheki alivyomuoga’ ‘umelegealegea sana na wewe’
Ndugu yangu hizo hapo juu zilivyo za kijinga hivyo hivyo ukizirudia rudia kwa mwnaume ambaye ana big ego niamini mimi unaweza kuvunja ndoa,Niamini mimi sababu ni mwanaume najua .