moja ya comment BORA kabisaa..
Wengi wanadhani wakipata pesa wataonekana bora zaidi na kuondoa udhaifu wao kumbe watu wanakaa kimya na kuwafurahisha ili wavune pesa zao. Ila kiuhalisia bado wanayaona madhaifu yao clearly na wakiona hawana faida tena bhasi wanatumia hayo hayo madhaifu kuwatelekeza
Mungu kaumba karibia kila kitu kwa upekee wake na ndio maana hakuna
kiumbe anaelingana na yeyote mwingine ingawa wanaweza kuwa wa jamii moja
na wakati mwingine mmoja kufananishwa na mwingine.
Binadamu hata wazaliwe pacha wa kufanana (identical)
bado wanazo tofauti, ziwe zinazoonekana ama nyingine zisizoweza
kuonekana kiurahisi kwa macho.
Kama ilivyo kwa uumbaji ni majaaliwa,
tukubali basi kuwa hata maisha tunajaaliwa na kufanikiwa kwetu kunatofautiana pia.
Ukiikataa kanuni hiyo ni kwakuwa umejaaliwa ujuaji.
Unaweza kujaaliwa Elimu/Ufaulu/Ujuzi nk.,
Mwenzako kajaaliwa kufanikiwa kwa njia nyingine kabisa isiyohitajiElimu kuubwa kama au zaidi yako.
Hivyo ndivyo ilivyo,taka-usitake, kubali au kataa.
Lakini ukweli ulio mchungu na unaouma 'ndani kwa ndani ';
Msomi upo na rundo la mavyeti yako ndani lakini unaishi
maisha ya nusu na robo.
-kisha kuna mpumbavu mmoja tena Std 7, au yule Fala uliemburuza sana darasani,
unashuhudia maisha yake ni yale ya;-ananing'inia tu juu kwenye balcony
huku akiawangalia kwa chini wanaze,kwenye swimming pool moja matata
mbele ya mjengo wake babkuubwa,huko nyuma 'wife' wake yupo bustanini
anagida na kunywa Mvinyo lainiiiii, lhali nyumba nzima imezunguukwa na wahudumu
wote wakiwajibika kuitumikia Familia ya yule fala, .
Achilia mbali miradi lukuki inayoingiza 'mafwedha' kwa kwena mbele.
Inauma ee?
Msomi unasubiri kamshahara/pension kako kasikofika hata katikati ya mwezi,
Hujaitusi tu elimu yako bado hapo?
Unasubiri nini kumbe?
Hapana usifanye hivyo,
Ndio maisha hayo.😆
Kisha eti mwingine anajifariji, "Nina Elimu" mwenzake hana.
Kwahivyo?
Sasa kusudio la maisha nini?
Uwe na Elimu utaabike???