Ushuhuda: Leo nimekutana na kipanga jeuri wa darasani. Kweli hakuna uhusiano wa uwezo darasani na wa maisha halisi

Kila shule na kila faculty vyuoni ina hawa viumbe wanaitwa vipanga; ni watu ambao wanafanya vizuri sana darasani aidha kwa kutumia jitihada kubwa ama uwezo mkubwa wa akili waliojaaliwa.

Tatizo sio kuwa kipanga, tatizo ni kuwa kipanga jeuri, ni wale watu wanaofanya vizuri darasani na kuona kwao tayari washapita mtihani wa maisha, yaani ni wale type za kuringa, zenye kujitenga pamoja na vipanga wenzao, wanaonyima watu chabo kwenye mitihani n.k

Sasa navyosoma zamani kulikuwa kuna huyu bwana alikuwa na tabia hizi na kiukweli kwake namba yake ilikuwa ni moja tu, yani alikuwa na tabia kama hizo nilizotaja, Chuoni assignment zake, notes zake za summary, n.k alikuwa anatunyima na hata kuwaita wazi wazi wasio na uwezi darasani ni vilaza.

Nimekodisha frem sehemu flani nimeweka binti awe anauza maana mimi muda mwingi nipo kazini, sasa kuna rafiki yangu tunaefanya nae kazi akavutiwa kufungua biashara ya kipati cha ziada, nikamshauri achukue fremu eneo lile nililopo maana ni pazuri, basi taratibu zikafanyika na rafiki yangu akafungua stationery kubwa tu.

Leo nlipotoka kazini nilienda dukani kwangu kuhesabu mzigo lakini pia lengo kuu nilikuwa na shauku kubwa ya kuona mradi wa huyu rafiki yangu maana leo ndio rasmi alianza kuuza.

Kufika pale nikapigwa na butwaa, nikaona kijana wa kazi pale ni yule kipanga, kiukweli nilihisi nmechanganya sura maana nilijua jamaa atakuwa huko kwenye vitengo vya juu au kufundisha vyuoni.

Nlimwita jina akaitikia nikajua hapa sijakosea ni yeye, basi ndio nikamkumbusha ndo akanijua akaniambia kafungua steshonari yeye, mimi nikawa namchora tu mbona ananidanganya, rafiki yangu akafika akamtambulisha huyo ndio kijana wake wa kazi, dah basi kwa kipanga ikawa aibu tupu.

Wakati wanafunga tukaagana na yule rafki yangu na mimi nikafunga maana dada wa kazi alikuwa kaniacha, nikamkuta njiani kipanga nikamwambia apande kama anajitaji lifti yeye akasema anasubiri mtu.

Usiku huu namcheki WhatsApp, nmemtumia message hadi sasa kaisoma ila hajajibu
[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Nina 29 yeye ana 28 sisi ni wazee??
Kwa mtu intelligent akisoma content ya ujumbe wako atagundua ulichotaka kuonyesha ni kuwa wewe umefanikiwa kwa kuwa una usafiri ( gari) na yule kipanga bado anabangaiza basi! Akili ya kijinga sana unayo!
Walk your path, kila mtu ana- destination yake ! Huwezi jua huyo " Kipanga" ana mipango gani na anawaza nini!
Hayo "mafanikio" kidogo uliyonayo haya- justy kuwa wewe ni mwerevu na huyo "Kipanga" ni mjinga!
Wewe kinachokusumbua ni akili ndogo ya kimasikini uliyonayo!
The true race of life is to compete with yourself and not others!
 
haya mambo yapo sana kuna kipanga jeuri alitusumbua sana sasa hivi yupo pale Spur Masaki ni muhudumu anatuletea pizza mezani
 
Kwa mtu intelligent akisoma content ya ujumbe wako atagundua ulichotaka kuonyesha ni kuwa wewe umefanikiwa kwa kuwa una usafiri ( gari) na yule kipanga bado anabangaiza basi! Akili ya kijinga sana unayo!
Walk your path, kila mtu ana- destination yake ! Huwezi jua huyo " Kipanga" ana mipango gani na anawaza nini!
Hayo "mafanikio" kidogo uliyonayo haya- justy kuwa wewe ni mwerevu na huyo "Kipanga" ni mjinga!
Wewe kinachokusumbua ni akili ndogo ya kimasikini uliyonayo!
The true race of life is to compete with yourself and not others!
Mshamba huyo na pia ana roho ya chuki
 
nashangaa watu wanapinga tu,ila kwa awamu hii kila kitu kinawezekana kabisa.

halafu kama aliamua kukudanganya ni wazi kwamba huyo ana apuuzi wa asili,si ajabu hata alipata mchongo akaharibu kwa tabia zake za kijinga.
 
Wewe mleta mada kwanza Inferiority complex inakusumbua,pia una low self esteem.

Watu kama wewe walioshindwa elimu ya darasani kazi yao kubwa mtaani hata makazini ni kuwananga wenzao ambao walikuwa na akili nyingi za darasani ila kwa namna moja au nyingine bado hawajafanikiwa.

Hata kama huyo kipanga alikuwa anajisikia sio sababu ya wewe kumuandama hivi,tambua zile zilikuwa age za utoto na watoto/wanafunzi hupenda kushindana.

Inaonekana unasikia raha kumwona mwenzako kwenye hali hiyo...shame on you!Acha iyo tabia maramoja ni aibu kwako especially kama ni man.
 
Kila shule na kila faculty vyuoni ina hawa viumbe wanaitwa vipanga; ni watu ambao wanafanya vizuri sana darasani aidha kwa kutumia jitihada kubwa ama uwezo mkubwa wa akili waliojaaliwa.

Tatizo sio kuwa kipanga, tatizo ni kuwa kipanga jeuri, ni wale watu wanaofanya vizuri darasani na kuona kwao tayari washapita mtihani wa maisha, yaani ni wale type za kuringa, zenye kujitenga pamoja na vipanga wenzao, wanaonyima watu chabo kwenye mitihani n.k

Sasa navyosoma zamani kulikuwa kuna huyu bwana alikuwa na tabia hizi na kiukweli kwake namba yake ilikuwa ni moja tu, yani alikuwa na tabia kama hizo nilizotaja, Chuoni assignment zake, notes zake za summary, n.k alikuwa anatunyima na hata kuwaita wazi wazi wasio na uwezi darasani ni vilaza.

Nimekodisha frem sehemu flani nimeweka binti awe anauza maana mimi muda mwingi nipo kazini, sasa kuna rafiki yangu tunaefanya nae kazi akavutiwa kufungua biashara ya kipati cha ziada, nikamshauri achukue fremu eneo lile nililopo maana ni pazuri, basi taratibu zikafanyika na rafiki yangu akafungua stationery kubwa tu.

Leo nlipotoka kazini nilienda dukani kwangu kuhesabu mzigo lakini pia lengo kuu nilikuwa na shauku kubwa ya kuona mradi wa huyu rafiki yangu maana leo ndio rasmi alianza kuuza.

Kufika pale nikapigwa na butwaa, nikaona kijana wa kazi pale ni yule kipanga, kiukweli nilihisi nmechanganya sura maana nilijua jamaa atakuwa huko kwenye vitengo vya juu au kufundisha vyuoni.

Nlimwita jina akaitikia nikajua hapa sijakosea ni yeye, basi ndio nikamkumbusha ndo akanijua akaniambia kafungua steshonari yeye, mimi nikawa namchora tu mbona ananidanganya, rafiki yangu akafika akamtambulisha huyo ndio kijana wake wa kazi, dah basi kwa kipanga ikawa aibu tupu.

Wakati wanafunga tukaagana na yule rafki yangu na mimi nikafunga maana dada wa kazi alikuwa kaniacha, nikamkuta njiani kipanga nikamwambia apande kama anajitaji lifti yeye akasema anasubiri mtu.

Usiku huu namcheki WhatsApp, nmemtumia message hadi sasa kaisoma ila hajajibu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787]
 
Wewe unaonekana una matatizo makubwa ya majivuno, riziki anapnga Mungu mwenyewe na yeye kukudanganya ni tabia ya kawaida ya binadamu asiyetaka maswali wala kuchimbwa zaidi,hivyo kitendo cha akiendelea kumchimba au kutoka ukaribu wa kinafiki na kumwelezea mafanikio uliyoyapata ni kumwongezea stress na humsaidii mwache mwenyewe..
 
Mungu kaumba karibia kila kitu kwa upekee wake na ndio maana hakuna
kiumbe anaelingana na yeyote mwingine ingawa wanaweza kuwa wa jamii moja
na wakati mwingine mmoja kufananishwa na mwingine.

Binadamu hata wazaliwe pacha wa kufanana (identical)
bado wanazo tofauti, ziwe zinazoonekana ama nyingine zisizoweza
kuonekana kiurahisi kwa macho.

Kama ilivyo kwa uumbaji ni majaaliwa,
tukubali basi kuwa hata maisha tunajaaliwa na kufanikiwa kwetu kunatofautiana pia.

Ukiikataa kanuni hiyo ni kwakuwa umejaaliwa ujuaji.

Unaweza kujaaliwa Elimu/Ufaulu/Ujuzi nk.,
Mwenzako kajaaliwa kufanikiwa kwa njia nyingine kabisa isiyohitajiElimu kuubwa kama au zaidi yako.
Hivyo ndivyo ilivyo,taka-usitake, kubali au kataa.

Lakini ukweli ulio mchungu na unaouma 'ndani kwa ndani ';
Msomi upo na rundo la mavyeti yako ndani lakini unaishi maisha ya nusu na robo.
-kisha kuna mpumbavu mmoja tena Std 7, au yule Fala uliemburuza sana darasani,
unashuhudia maisha yake ni yale ya;-ananing'inia tu juu kwenye balcony
huku akiawangalia kwa chini wanaze,kwenye swimming pool moja matata
mbele ya mjengo wake babkuubwa,huko nyuma 'wife' wake yupo bustanini
anagida na kunywa Mvinyo lainiiiii, lhali nyumba nzima imezunguukwa na wahudumu
wote wakiwajibika kuitumikia Familia ya yule fala, .
Achilia mbali miradi lukuki inayoingiza 'mafwedha' kwa kwena mbele.

Inauma ee?

Msomi unasubiri kamshahara/pension kako kasikofika hata katikati ya mwezi,

Hujaitusi tu elimu yako bado hapo?

Unasubiri nini kumbe?

Hapana usifanye hivyo,
Ndio maisha hayo.😆

Kisha eti mwingine anajifariji, "Nina Elimu" mwenzake hana.
Kwahivyo?

Sasa kusudio la maisha nini?
Uwe na Elimu utaabike???

Kila mtu ni BORA katika nafasi yake dunia hii na huwezi kuondoa UBORA wa mtu katika kitu flani kwa wewe kuwa BORA katika kitu kingine.. Hiyo ni NEVER na HAIPO zaidi ya kujifariji tu

BAKHRESA kuwa BORA katika Biashara inamaanisha amemzidi ubora WARIOBA katika nafasi yake sababu hazalishi mabilioni ya shilingi katika account zake. WARIOBA kuwa Bora Katika Elimu na uongozi inamaanisha ni Bora kuliko BAKHRESA katika nafasi yake kwa sababu hajawahi kupata Degree au Uwaziri.

Kiufupi, Wape watoto wako majumba na kila kitu lakini kama huna elimu historia yako itabaki ile ile kuwa baba yao uliishia darasa la nne C na huna msaada kwenye elimu zao zaidi ya usimamizi wa kuhadithiwa na ADA.
Kipanga nae atabaki na historia yake hata kama anamiliki kitanda na Godoro tu ambalo haliwezi lipia wanae ada ila atakuwa na uwezo mkubwa kuwasimamia kielimu.

ukiona Darasa la nne linakuharibia CV kwenye hela zako, Rudi Darasani.. Ukiona Pesa Huna sawa na vyeti vyako, unaingia mtaani. Hakuna mbadala. THE END
 
Nina 29 yeye ana 28 sisi ni wazee??
Kwa umri huu bado sana kwenye maisha na hukupaswa kumuandika huyo jamaa kama mtu alienyuma kimaisha huku wewe ukijiona umeshatoboa. Narudia tena bado,bado na bado mno. Mimi binafsi ni shahidi na utayakumbuka maneno yangu
 
Mara nyingi stori kama hizi huwa zinatoka kwa watu waliofeli masomo yao darasani au waliokuwa hazichaji kichwani na huwa faraja yao pekee ni kusubiri kipanga mmoja apigwe na maisha warudi kusema 'yako wapi sasa'!

Lakini wanasahau kwamba ukiwa na cheti au akili, hela bado una nafasi ya kuitafuta. Lakini hata kama una hela, kama hazichaji kichwani bado haziwezi kuja na hauwezi kuzitafuta akili kwa hela zako
Kwani akili ni nini? Kuwa wa kwanza darasani au kufaulu mtihani?
 
Back
Top Bottom