Ushuhuda: Leo nimekutana na kipanga jeuri wa darasani. Kweli hakuna uhusiano wa uwezo darasani na wa maisha halisi

Maisha ni Kama gwaride ukisikia nyumaaa! geuka !!!wa Kwanza anakuwa wa mwisho wa mwisho anakuwa wa kwanza
 

Hii kama chai inataka kuzidi sukari, huyo alikuwa kipanga kweli au kishoka?
akikujibu ni-tag.

Maana vipanga wenye alama "B" na "A" kwenye PCM, PCB, PGM ukikutana naye, respect yake lazma umpe.

Maana akikosa hela anaweza kukamata madogo wa A-Level akawapigia Topic Moja ya "Advanced Physics" au "Pure Mathematics" kwa Tsh. 20,000/- hapo akiwa na wanafunzi 20 tu anaweza kula mpaka Tsh. 400,000/- zake fasta kwa Topic moja tu tena bila makato ya kodi.
Tena Topic yenyewe unakuta anaimaliza kwa siku 12 tu.

Mimi li-kipanga lolote lile lenye "A" au "B" zake za A-Level kwenye combination za PCM, PCB, PGM, CBG na EGM.
Likipanga la hivyo huwa hata nilikute limechoka vipi huwa bado naliheshimu sanaaaa.
 
Jua kuna akili za shuleni na akili za kwako mwenyewe sisi sote tunatumia akili binafsi katika kufanya vizuri katika maisha ,hapa ndipo tunatofautiana akili.
Wengi waliokua na akili darasani waliona wana akili ya kuwin maisha pale ni class kuna x toa y sawa na 2 ,maishani akuna izo mambo huku kuna kutafuta pesa haijalishi shuleni ulikuaje.

Na akili sio kupata pesa akili ni kutumia pensa kufanikisha malengo ulio jiwekea.


Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Man down, I repeat man down
 
Vilaza bana basi roho yako kwatu [emoji3][emoji3]
 
Mchawi sio lazima aruke na ungo.Kitendo cha kufurahia mwingine kuwa na maisha magumu kisa alikuwa anakuzidi kitaaluma ni uchawi tosha. Ukisikia huyo jamaa kafukuzwa hapo utafurahi, ukisikia jamaa anaumwa utafurahi,kiufupi wewe ni mchawi.
 
wewe ndio hujui. ukiajiriwa na mtu hata kama unamzidi au unalingana nae Umri huyo mtu anabaki kua kijana wako tu. Ndio maana wenye Peasa wanaitwa wazee tena na watu Wazee.
 
Bora hata usingemtumia msg maana anahisi unamsanifu,ila tusiwe na tabia ya kukufuru,maisha siku zote ni kupanda na kushuka,kutokuwa na akili ya darasani sio kutokufaulu maisha,binadamu katika swala la kufanikwa kila mtu huwa na karama zake alizopewa na Mungu...
 

Japo hiyo hali ipo ila kwa hii story yako ni TANGO PORI.
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Nimecheka lakini man sio poa, usijaji watu hivyo [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] unaweza kuta jamaa alikua vizuri darasani sema mtaani akakosa connections na wengi wao wanaokua darasani vizuri ni wale unakuta kwao maisha yao ni magumu kimtindo, wapo wengi sana mbona mjini, ila usicheke mzee [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Kumbe na wewe ulikuwa kipanga bro hahaaaaa
 
Unajikubali na hali yako imemshinda hiyo maana shuleni pia alikua na na dharau kama mdau alivyosema kuwaita wenzake vilaza, kama asingekua na dharau shuleni siajabu angeweza hata kumuomba jamaa connection za kazi, life imepinda halafu unajifanya imenyoka, ila pia huwezi kuchagua kazi kuna baadhi ya kazi ni daraja kwenda kufikia kwenye lengo
 

moja ya comment BORA kabisaa..
Wengi wanadhani wakipata pesa wataonekana bora zaidi na kuondoa udhaifu wao kumbe watu wanakaa kimya na kuwafurahisha ili wavune pesa zao. Ila kiuhalisia bado wanayaona madhaifu yao clearly na wakiona hawana faida tena bhasi wanatumia hayo hayo madhaifu kuwatelekeza
 
Maneno yako yanayo faraja ambayo haina tija saaana.

kwanza Elimu na Akili ni vitu viwili tofauti ambavyo kwa namna mmoja ama nyingine vinaweza kuingiliana au kukanganywa katika kuvielewa.
Iwapo tunazungumzia Elimu/Cheti basi tuihusishe na ujuzi na iwapo tunazungumzia Akili/Ujanja basi tubainishe za wapi Darasani ama Mtaani/Duniani/Kimaisha.

Wapo watu na Elimu zao lakini wanafeli maisha bila ya kujali kipato walichonacho na pengine kufulia kabisa pamoja na kwamba wanavyo vyeti vyao (Kutokuweza kuitumia Elimu waliyonayo kujiendesha au kujipa misha yenye unafuu machoni mwa wanaowazunguusha)

Kwa upande mwingine, wapo wasio na Elimu kabisa lakini maisha yao ni tambarale kufikia hata hao wenye ma-Phd. kuwa waajiriwa wao.

Kufupisha mada hata uwe na vyeti chumba kizima,
Iwapo havikufanyi uwe na misha bora,mazuri na yenye furaha mpwa umefeli.

Hoja ya kuwa kwakuwa unayo Elimu basi unao uwezekano wa kuyarekebisha hiyo ni kujifariji.

Elimu ni nyenzo yakurahisisha mengi yatakayotawala maisha yako.
Iweje asie na nyenzo atoboe wewe ulie nayo ushindwe kisha usema eti, kwakuwa unayo nyenzo basi ipo siku,lini?
Faraja!
 
Mungu kaumba karibia kila kitu kwa upekee wake na ndio maana hakuna
kiumbe anaelingana na yeyote mwingine ingawa wanaweza kuwa wa jamii moja
na wakati mwingine mmoja kufananishwa na mwingine.

Binadamu hata wazaliwe pacha wa kufanana (identical)
bado wanazo tofauti, ziwe zinazoonekana ama nyingine zisizoweza
kuonekana kiurahisi kwa macho.

Kama ilivyo kwa uumbaji ni majaaliwa,
tukubali basi kuwa hata maisha tunajaaliwa na kufanikiwa kwetu kunatofautiana pia.

Ukiikataa kanuni hiyo ni kwakuwa umejaaliwa ujuaji.

Unaweza kujaaliwa Elimu/Ufaulu/Ujuzi nk.,
Mwenzako kajaaliwa kufanikiwa kwa njia nyingine kabisa isiyohitajiElimu kuubwa kama au zaidi yako.
Hivyo ndivyo ilivyo,taka-usitake, kubali au kataa.

Lakini ukweli ulio mchungu na unaouma 'ndani kwa ndani ';
Msomi upo na rundo la mavyeti yako ndani lakini unaishi maisha ya nusu na robo.
-kisha kuna mpumbavu mmoja tena Std 7, au yule Fala uliemburuza sana darasani,
unashuhudia maisha yake ni yale ya;-ananing'inia tu juu kwenye balcony
huku akiawangalia kwa chini wanaze,kwenye swimming pool moja matata
mbele ya mjengo wake babkuubwa,huko nyuma 'wife' wake yupo bustanini
anagida na kunywa Mvinyo lainiiiii, lhali nyumba nzima imezunguukwa na wahudumu
wote wakiwajibika kuitumikia Familia ya yule fala, .
Achilia mbali miradi lukuki inayoingiza 'mafwedha' kwa kwena mbele.

Inauma ee?

Msomi unasubiri kamshahara/pension kako kasikofika hata katikati ya mwezi,

Hujaitusi tu elimu yako bado hapo?

Unasubiri nini kumbe?

Hapana usifanye hivyo,
Ndio maisha hayo.πŸ˜†

Kisha eti mwingine anajifariji, "Nina Elimu" mwenzake hana.
Kwahivyo?

Sasa kusudio la maisha nini?
Uwe na Elimu utaabike???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…