Nimesoma comments zote hadi mwisho, Nimegundua wabongo wengi humu ndani ni wajuaji sana, halafu wanajiona ni miamba ( wanajua kila kitu ).
Yaani kuana aina nne za ujuaji :-
- Anajua kama anajua
- Anajua kama hajui
- Hajui kama anajua
- Hajui kama hajui
Sasa wajuaji wa humu wapi hapo kwenye no.4, Yaaai hayajui kama hayajui alafu kutwa kushupaza shingo kama manyumbu. Ndio maana wengine huwa hawatoagi siri kama hizi, kwasababu ya hizi tabia za kinoko.
Imagine, jamaa hajaomba hela, hajahitaji msaada kwa mtu, ame weka tu mbinu yale aliyoitumia ikamlete mafanikio fulani, uziri maelezo yake yameshiba na yamejitosheleza.
Sasa hizi habari sijui za kimba, sijui upumbavu gani zinatoka wapi? Punguzeni utoto basi nyie watu, sio kila jambo ni lakudharau na kulifanyia mzaha... Unaweza kukuta huyu mleta mada age ipo 60+ huko, yaani ni mtu mzima wakuitwa Baba / Babu, sasa mtu kama huyo anapoamua kutupatia mbinu zake zilizomletea mafanikio fulani halafu wewe unaweka maneno ya kejeli na dhihaka, hizi unajisikiaje ndani ya nafsi yako?
Jamani hebu tubadilikeni, tuweni hata na adamu na staha kwenye kujibu nyuzi kama hizi hapa sio chit chat mazee.
Kupitia kisa hiki, unaweza kuta kuna member mwengine nae alikua anajiandaa kuleta ushuhuda wake namna alivyofanikiwa kwenye jamba filani, halafu anakutana na negativity kama hizi, unadhani atamwaga mchele kwenye kuku wengi?
Mleta mada nakupongeza kwa ujasiri, halafu nimegundua una emotional stability kubwa sana, licha ya dhihaka nyingi ulizoshambuliwa nazo lakini umebaki calm na unajibu comments in positive way, nadhani meditaton imekusaidia, hapa sina hakika zaidi kama ni hiyo meditation au ni hulka yako tu yakuwa humble.
Nakupa tano mkuu kwenye hilo na nikutakie kheri zaidi. Nami ninapitia hizi changamoto maishani ambazo sinabudi kuamini zina uhusiano na imani ya upande wa pili.
Yaani masikio yangu yana uzito wa usikivu, tatizo hili limenipata ukubwani tu, nimeenda hospitali zote kubwa hadi agakhan hapo na hivi vi polyclinic vyote vya wahindi vilivyopo hapo upanga na kisutu lakini masikio yako sawa, hawaoni tatizo lolote. sijapata ufumbuzi wa tatizo langu.
Kupitia uzi wako nitaanza tiba hii ya mkojo halafu nitaangalia matokeo juu ya tatizo langu sugu lisiloonekana hospitali zote kubwa.