Ushuhuda: Nilichokiona kwenye kikao cha ukoo/familia, bila pesa huthaminiwi

Ushuhuda: Nilichokiona kwenye kikao cha ukoo/familia, bila pesa huthaminiwi

Kwanza kabisa watu wanaweza kudhan hii ni comedy ila ni ukweli mtupu.

Wiki kadhaa zilizopita kulikuwa na kikao cha ukoo kuhusu jambo flani hivi nyeti, kikao kilitubidi twende kijijini kwetu.

Tulifika vizuri tu na kusalimiana ila sasa kikao kilipotaka kuanza, kuna ndugu yetu flani uchumihaujamkaa sawa aliambiwa aende getini awe anaangalia usalama ama kupokea wageni.

Mwengine naye kikao kilipoanza baada ya kama dakika 20 aliitwa aende kupasua kuni kwa ajili ya kuota moto tukimaliza kikao

Mwengine aliruhusiwa kubaki ila aliishia kukaa kimya maana kila akijaribu kuongea anakatwa jicho fulani ivi mpaka anakosa raha.

Kiukweli niliumia sana
Wewe ni mnafki kwasababu kama kweli uliumizwa na yaliyofanyika kwa ndugu zako kwanini usiongee waziwazi kwenye hicho kikao kwamba hufurahishwi na wanachofanyiwa ndugu zako... unakuja huku kuhadithia
 
Wewe ni mnafki kwasababu kama kweli uliumizwa na yaliyofanyika kwa ndugu zako kwanini usiongee waziwazi kwenye hicho kikao kwamba hufurahishwi na wanachofanyiwa andugu zako... unakuja huku kuhadithia
Kimodo. Elewa kwamba huyu hakua na uchumi wa Kati hivyo hata angesema asingesikilizwa.
Kimodo. Umesha wahi ku attend kikao Cha wachaga wenye hela? Kama gari yako Ni pick up au vitz usitegemee kusikilizwa. Sasa itakua huyu hata bodaboda Hana.
 
Huo ukooo umekufa, kwetu kikao kinaongozwa na watu wanaotuzidi umri na siyo wanaotuzidi pesa,tajir akizingua achague moja kula fimbo au atoe faini ya dume la moooo!
 
Back
Top Bottom