chrisbleez
JF-Expert Member
- Dec 28, 2016
- 752
- 1,239
Mtu anaefanya dharau na kutothamini nduguze ama mtu yeyote wa nje atambue kuwa ipo siku ataondoka na ataacha kila kitu.
Ilo lipo wazi mkuu linajulikana lkn pamoja na ilo kuendekeza ndugu ni kujitaftia au kujiongezea umaskini hii ni kwa mujibu wangu naomba nisinukuliwe vibaya sijasema kwa ujumla wake hii ni kwa nionavyo mimi
Wacha nitoe mfano mdogo tu kwa faida ya wengine,katika hicho kipindi chote ambacho sikuwa mtamu nilionekana fala mbele ya ndugu zangu na hali hii nimekuwa nayo tangu mdogo sikuwahi kuonekana mtu mbele za watu kwa miaka yote nimeishi kwa manyanyaso na kutothaminika nimekuwa nikipatwa na majaribu ya kishirikina mara kwa mara tangu udogo wangu
Nimekuwa nikinusulika kuuwawa na washirikina tena hawa hawa ndugu zangu wa karibu sana tena sana na majaribu mengine nilikuwa nayashuhudia kwa macho yangu nikiwa ninaakili zangu timamu
Baadae nilipata mtu wa kunifungua akili,akanifanya kuwa mtu mpya na hapo ndipo nikaanza kuonekana mtu kati ya watu alafu leo hii eti nije nimpe nafasi mtu anaeitwa ndugu[emoji1787]sio rahisi
Naomba nimalizie kwa kusema ndugu ni watoto wako pamoja na familia yako nikimaanisha baba,mama na watoto