Ushuhuda wangu kuhusu RADI (my own testimonial)Nimeshuhudia RADI! Mara mbili, Ni kweli RADI ni kuku kabisa! Tena jogoo anaevutia haswa!

Story za wazee wa mkoa wa njombe ndani ndani huko wanadai radi ni mnyama kama kondoo vile na ana miguu sita pia na msumeno mgongoni, wapo walio wahi kutana nae wote wanasimulia mfanano huo ila mwishoe huishia na mianga mikali na ngurumo zisizo na kifani yaani hii radi tuijuayo. Wana dhana nyingine kwamba radi za namna hii (radi zenye mkono wa mtu) huchochewa na kuvaa nguo rangi nyekundu ila hukingwa kwa kukaa jirani na mnyama kondoo, inasemekana kondoo hupigana na huyo mnyama radi, pia kukaa eneo lenye mianzi (baobab tree) inasemekana radi ikipiga lile eneo lile basi anaweza akanasa kwenye mianzi hiyo kama mnavyojua mti wa mwanzi ulipasuliwa katikati huwa na uwezo mkubwa wa kubana ktkt yake.

Twaweza chukulia tu ni story ila wazee wale walikuwa serious kwa hizo story, ila wao wanàamini hivyo sasa wewe nenda na physics zako utake kufanya majaribio, kuna story moja niwape kwa ufupi, kuna mradi mmoja uliitwa NDDT Ulitekelezwa kuanzia miaka ya 1980's katikati mpka miaka ya 2010 hivi ulikuwa chini ya NORAD, NIDA NA SWEDISH yaan zile nchi za scandinavia waliungana, walipeleka wazungu kujitolewa kama walimu walijenga camps za shule ziliitwa maarufu shule za NDDT, sasa miaka ya 90 mwanzoni kuna mzungu alikuwa na mahusiano mazuri na jirani yake ambaye ni mwenyeji, siku akamuuliza naskia kuna usafiri wa chap chap wa kufumba na kufumbua ni kweli? Yule mzee jina nahifadhi alimjibu hata mimi ni mtaalamu, akamwambia siku moja tujaribu wakakubaliana hivyo, siku imefika alipewa maelekezo yote alitekeleza destination yao ikawa na njombe mjini kiasi cha kama 80 km kutoka hapo kijijini Lupembe, basi bwana aliambiwa fumba macho akafumba baada ya muda fumbua akafumbua, ile kufumbua alikuwa nje ya hotel ya magazeti, enzi hizo ni hotel maarufu sana njombe, basi mzungu yule akaingia hotelini akaagiza soda, akanywa akamwambia mzee mwavi.... Nirudishe process ikarudiwa akawa nje ya nyumba ya yule mzee, mzungu akaaaga akarudi kwake, akatafakari, aka ona bora a park mizigo yake arudi tu ulaya.


Kama wewe ni mzaliwa wa Dar es salaam au sio mkazi wa nyanda za juu kusini utaona hizi ni story tu, pole sana!
 
Nakuunga mkono kwa uliyoyaandika......kila sehemu kuna namna wanavyomfahamu mnyama radi binafsi nilishawahi kuona tukio la mti kupigwa radi lkn nilipofika kuangalia nikakuta kuna makucha ya mnyama yamekwaruza hivyo nami nikaanza kupata wasiwasi huenda radi ni mnyama kweli......vitu kama hivi ukimueleza mtu anaejidai ni msomj hawezi kuelewa

Kanda ya ziwa huamini radi anafanana na jogoo ila maeneo ya kusini radi hufanana na mnyama mwenye miguu sita
 
Ww utakuwa msukuma maana hadith kama hizi wasukuma wanazipenda sana HAKUNA KITU kama bwana mkubwa
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa naanza kupata picha, radi kumbe hutofautiana kutokana na eneo inapotokea, hizi nilizoshuhudia mm zilitokea kanda ya ziwa. Kuna vitu deep havijafunuliwa kuhusu RADI tumefichwa kwenye kichaka kwamba radi ni umeme, ila ukichunguza kuna mambo ya kiimani na kimungu hapa zaidi ya sayansi.
 
Na hapo ndipo ile dhana ya uwepo wa mkuu wa vyote Mungu) hudhihirika wazi.
Tatizo la stori zenu za dizaini hii ni hilo TU..Nimeshalitaja tatizo...

Kama hujaelewa,tatizo Huwa ni 'story' TU.

Hamna ushahidi, Bali inatulazimu tukuamini wewe mtoa stori.
Pamoja na teknolojia kukua kiasi cha kila mtu mzima aliyebarehe anamiliki smartphone na anaweza kustream live matukio ya ajabu...Lakini Duniani kote hakuna Ushahidi wa video au live stream ya matukio ya hivi.

Mengi Huwa ni simulizi za mdomoni TU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…