Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Ushuhuda wangu: Mimi ni muathirika wa HIV (HIV Positive)

Mabaaria wa kula tunda kimasihara hii inawahusu siwaoni uku kabisa..mnaitajika viti vya mbele uku vipo wazi. yani Kiukweli mimi last time kupima ilikuwa 19/november 18 ila dah kuna rafu mbili nilizicheza af sielewi kbsa yani siku ya kupma tn itakuwaje. Ila Hongera dada Kwa ujasiri ulonao
Asante, muwe makini tu huko uraiani kumechafuka sana na hali ya uchumi ilivyo mbaya maambukizi yataongezeka sana. Mjitahidi kama hamuwezi kuwa na mpenzi mmoja basi jitahidini mtumie mipira jamani
 
Mtoa mada Inaonekana huko PM wala hauna usumbufu kama wengine
ID ya zamani kule wanaume ni wengi wasumbufu, hili pia nitoe angalizo kwa wana Jf hasa mabinti wawe makini kuna baadhi ya watu humu hawana mema nao unakuta wanawashawishi kwa vitu vidogo na kuishia kulala nao. Mimi wengi wanakuja na mambo ya kunihonga ila tukionana wanakuwa hawana la ziada hivyo ikitokea nimelala nao basi ujue walinivutia kwa vitu fulani na sio mambo ya hela na blah blah nyingine
 
Duh!! Pole saa mpendwa, sina cha kukwambia sababu natumai ushaambiwa saana, wala sina cha kukushauri sababu ushapata ushauri wa kutosha, pia sina sababu ya kukupa maneno ya kukutia moyo sababu kwa maelezo yako na kitendo cha kuandika huu uzi hapa tayari hii hali ushaipokea na wew unajionea kitu cha kawaida, kikubwa tu nakushukuru kwa kushare nasi hapa hii habari, yaweza kuwa matumaini kwa wale wasiokuwa na matumaini waliokata tamaa kwenye janga kama hili ama kwenye misanga tofauti tofauti, ni funzo pia kwetu soote.
Natamani ungekuwa mshikaji wangu kwenye maisha ya kawaida nje na jf.

Nakushukuru na ubarikiwe
Kila la kheri bibie.
Nitakufikiria na asante kwa maneno ya faraja pia
 
Back
Top Bottom