Ushuru wa Kuagiza (import) Magari umepanda Kinyemela?

Ushuru wa Kuagiza (import) Magari umepanda Kinyemela?

Mkuu nisaidie kujibu. Nini faida ya kuagiza kupitia kampuni yako badala ya mteja kuagiza direct Japan?
ahsante kwa swali la msingi sana mzee wangu ;

1. USALAMA ;

Kwetu, EAPGS mteja anapoagiza kupitia sisi, anakua na uhakika wa usalama wa fedha yake, kati ya vithibitisho vingi anavyopata E F D risiti ni miongoni mwavyo.

2. UHAKIKA

Mteja, anakua na uhakika wa kile alichoagiza ndicho hicho anachokabidhiwa, kwa sababu hata yeye pia anapewa nafasi yakua anatazama procedures zote za gari yake hadi inapofika bandarini Dar es salaam

3. UNAFUU

Mteja anapoagiza gari kwetu, anapata unafuu wa bei kadharika wa gharama zingine ambazo angepaswa kuzilipia kwa wakati mmoja asilimia mia moja.
kwetu, mteja anapata nafasi ya kuzilipa kidogo kidogo kwa muda wa hadi. mwaka mmoja.

NOTE : HUDUMA HII SIO YA LAZMA, NI IWAPO MTEJA MWENYEWE ATAPENDA

Haya ni machache kati ya mengi.

karibuni sana

KAZI NI KWAKO !!!

EAPGS

MAFIATI AREA
MBEYA TANZANIA
WHATSAPP ONLY
+255 682 274 097
 
hii nchi ni ya hovyo sana huwa nashindwa kuelewaga ni kwasababu gani ushuru unakuwaga mkubwa kushinda bei ya gari" mfano: gari imetengenezwa Japani imegharimu materials kadhaa wa kadhaa mpaka inaikamilika, unakuta unaisafirisha kwa kutumia usafiri meli toka japan hadi kufika tanzania kama ni vitz gaharama ya kuisafirisha hata milioni mbili haifiki wakati huo kule japan ilipotengenezwa unakuta umeinunua kwa M 3.5 lakini cha kuskitisha ikifika tu pale bandarini yaani kitendo cha kuitoa pale tu unaweza ukaambiwa gharama ni milioni 5 sasa huu ni uzalendo kweli au tunaibiana? kinachosababisha gharama kuwa kubwa ni kitu gani hasa? ukiangalia si kwamba labda serikali ndio imeingia gharama za kuitengeneza na wala sio serikali iliyoingia gharama za kuisafirisha sasa kama serikali haijaingia gharama yeyote kwanini ushuru uwe juu kuliko hata ile gharama ya kuinunua hilo gari na kuisafirisha?
Nchi yako imekupa eneo la kufanya shughuli zako, barabara za kuendesha gari lako, ulinzi na vyuo vya kupata wanawake wako halafu hutaki kuongeza tumilioni kadhaa?
 
Nataka nichangie kidogo hapo, sio kwamba TRA huwa wanapandisha Kodi ikifika January ya kila mwaka Bali kinachofanyika ni hivi, TRA Kuna ushuru ambao unakatwa kulingana na idadi ya miaka ya Hilo gari tokea litengenezwe na Kodi yao ipo hivi
Gari iliyotengenezwa na kuagizwa kuja hapa nchini ikiwa na umri wa miaka 0-8 haitozw Kodi ya uchakavu, gari yenye miaka zaidi na 8 na ipo chini ya miaka 10 inatozwa 15% ya uchakavu na gari iliyo na miaka zaidi ya 10 inatozwa 30% sasa inaweza kutokea umeagiza gari yako mwaka 2021 mwezi november ikiwa ndani ya miaka 10 lakini bahati mbaya ikafika bandarini January 2 2022 hiyo gari tayari inakua imevuka miaka 10 na haitatozwa 15% ya Kodi badala yake itakatwa 30%
Uko sahihi sana mkuu.
Lakini pia kuna baadhi ya gari thamani ya CIF TRA wanaipandisha baada ya kipindi fulani kutokana na demand ya gari husika hivyo kupelekea kodi kuongezeka, nimetolea mfano T/IST model za miaka yote kodi zilipanda mwaka 2021.
 
Nataka nichangie kidogo hapo, sio kwamba TRA huwa wanapandisha Kodi ikifika January ya kila mwaka Bali kinachofanyika ni hivi, TRA Kuna ushuru ambao unakatwa kulingana na idadi ya miaka ya Hilo gari tokea litengenezwe na Kodi yao ipo hivi
Gari iliyotengenezwa na kuagizwa kuja hapa nchini ikiwa na umri wa miaka 0-8 haitozw Kodi ya uchakavu, gari yenye miaka zaidi na 8 na ipo chini ya miaka 10 inatozwa 15% ya uchakavu na gari iliyo na miaka zaidi ya 10 inatozwa 30% sasa inaweza kutokea umeagiza gari yako mwaka 2021 mwezi november ikiwa ndani ya miaka 10 lakini bahati mbaya ikafika bandarini January 2 2022 hiyo gari tayari inakua imevuka miaka 10 na haitatozwa 15% ya Kodi badala yake itakatwa 30%

Kuna hii kesi CIF ya TRA kuwa juu kuliko uhalisia au Bei iliyowekwa mtandao I ambayo ndio unailipa, hiyo inakuaje?

Yaani kitu kinauzwa Kwa $1000 lakini TRA anakwambia Bei ni $2000 au $1500.

Kingine unakuta gari unaiingiza kutolea Japan ila kwenye mfumo wa TRA wanakwambia imetokea Ulaya na hapo Kodi inatofautiana ( sijajua wanafikiria ni gari mpya na wanaangalia origin ya ilikotengenezwa?)
 
Kwanza TRA wao wanaangalia originality ya gari, wapi inapotengenezwa, lakini pia mfumo wao wa kucalculate Kodi wanatumia ile ya Bei ya gari ikiwa mpya au ndio kwanza ipo kiwandani inauzwa thamani yake ni kiasi gani? Kwa mfano labda IST mpya kabisa zilo km Japan inauzwa $4000 Basi TRA kwenye mfumo wao ukiingiza gari watacalculate Kodi kupitia thamani hiyo, lakini Kuna mambo mawili siku ukienda kuclear gari

01 gharama inaweza kuzid kulinganisha na ile ambayo wewe umeona kwenye website yao na hii inasababishwa na sababu ambayo nimeilezea hapo juu

02 gharama inaweza kupungua na hii huwa inasababishwa na invoice husika ya muuzaji amekuandikia kiasi gani

Lakini swala la msingi ambalo wauzaji wengi na waagizaji wengi wa magari hawaweki wazi kwenye Bei ni kwamba hizo used cars kutoka japan zinauzwa na zinapewa Bei kulingana na condition stage ndio maana unaweza kukuta gari aina moja, model moja, engine sawa na mwaka plus mwez wa usajili ni sawa na hata km zilizotembea zinalingana na rangi sawa Ila Bei ikatofautiana uliwah kujiuliza inasababishwa na Nini? Jibu ni hivi gari zote zinapewa Bei kulingana na condition stage gari iliyo na 3.0 condition stage haiwezi kuuzwa Bei sawa na iliyo na RA au 2.5, sasa hapa waagizaji wengi wenzangu hawawambii wateja wao na hata TRA hili hawawezi kujua hivyo unapolalamika ushuru kupanda jiulize je gari hii ingekua mpya thamani yake ni kiasi gani, na mm naichukua leo je itaangukia kwenye ushuru upi wa chakavu wa tra je ni 0%, 15% au ni 30%?
 
Kuna hii kesi CIF ya TRA kuwa juu kuliko uhalisia au Bei iliyowekwa mtandao I ambayo ndio unailipa, hiyo inakuaje?

Yaani kitu kinauzwa Kwa $1000 lakini TRA anakwambia Bei ni $2000 au $1500.

Kingine unakuta gari unaiingiza kutolea Japan ila kwenye mfumo wa TRA wanakwambia imetokea Ulaya na hapo Kodi inatofautiana ( sijajua wanafikiria ni gari mpya na wanaangalia origin ya ilikotengenezwa?)
Na TRA wao hawaangalii Hilo gari ni chakavu, au mpya wao CIF yao wanatoa kwenye gari ikiwa mpya thamani yake ni Bei gani?
 
Safi sana, kuna watu wanadhani kila mtu yuko gizani! Zamani nlijua wakikuagizia bei inapungua labda wana connection kumbe njaa tupu wanataka waponee humo!
wana njaaa kupitiliza, yaani unakutana na dalali koromeo limemkauka akisubiria pesa yako akalewe double kick
 
Nilikua najichanga angalau niagize BMW X3 ili niokote watoto wa Chuo kiulaini. Sasa kabla sijalipia Be Forward nikasema nichungulie Calculator ya TRA nimekutana na Maumivu yaani BMW X3 ya 2013 (CIF 9,656 USD) mikodi ya watoza ushuru inafika 12m hapo bado port charges etc. Huu ushuru mbona umepanda kinyemela? December 2021 ushuru ulikua 9m TZS kwa hgari hiyo hiyo! Twafaaa

View attachment 2114007
umechungulia xchange rate mkuu???!!??
 
Unaonaje pia kaka/dada ukaweka ushahidi na uthibitisho hapa?
Pengine itakua busara zaidi ili kwenda sambamba na tahadhari yako.

Pia, sioni tija ya kukebehi watu kwa kuita wajinga, kwasababu tuu mmepishana kimawazo.

Hekima ni utajiri mkubwa sana.
Hawa wanaokuagizia ni matapeli wakubwa. Nishakutana na wanaoitwa MAGARIRAHISI ni matapeli. Wapo kibao kama hao. Matapeli.
 
Back
Top Bottom