Magari chakavu ni mzigo mkubwa sana kwa taifa, ingawa tunaona unafuu kwa "individuals" lakini tnashindwa kufikiri. Wala siyo "rocket science", fikra ndogo sana tu, vipi nchi za kitajiri ambazo zina kila kitu, ziyachoke na kuyatupa kwa bei poa, wewe uyarundike kwenu? Yamewashinda nini hao wanaotaka kuyapeleka "scrap yard" halafu sisi tunayakimbilia?
Kinachotakiwa ni simply kuyapiga marufuku magari chakavu yote, kupunguza ushuru wa gari mpya, na kuziwekea ukomo wa kutumika barabatani, maximum iwe miaka 10 kwa gari ndogo na miaka 15 kwa gari za "commercial". Automatically gari mpya zitashuka bei wakipenda wasipende na tutakuwa na assembly plant zetu kwa kuanzia, na hatimae tutaunda asilimia kubwa ya vifaa vipya hapahapa nchini, tena vyenye ubora tutaoupanga sisi, ilimradi tuipige msasa TBS rushwa iuliwe kule.
Ni ajabu sana, mpaka leo tunashindwa kuunda japo vioo tu vya magari vyenye ubora, ili hata tukiagiza gari mpya tunawaambia tunalinunua bila vioo, vioo tunakuja kubandika vyetu. Hivyo hivyo kwa vifaa vyote, kidogo kidogo.
Maendeleo hayaji bila maamuzi magumu ya viwanda, tena hatuhitaji viwanda vikubwa, vidogo vidogo tu.
Wasomi wetu naona kazi na sifa yao ni ya kujaza makaratasi tu ukutani na kugombania safari za kwenda nje "kula bata". Siyo kuwa busy kwenye labs na workshops kujaza ubunifu mitaani. Unamkuta anajisifu "mimiMechanical Engineer", ukimuuliza unaunda nini? Anakukodolea macho kama mjusi kabanwa na mlango. Hana jibu.