Ushuru wa Kuagiza (import) Magari umepanda Kinyemela?

Mkuu nisaidie kujibu. Nini faida ya kuagiza kupitia kampuni yako badala ya mteja kuagiza direct Japan?
ahsante kwa swali la msingi sana mzee wangu ;

1. USALAMA ;

Kwetu, EAPGS mteja anapoagiza kupitia sisi, anakua na uhakika wa usalama wa fedha yake, kati ya vithibitisho vingi anavyopata E F D risiti ni miongoni mwavyo.


2. UHAKIKA

Mteja, anakua na uhakika wa kile alichoagiza ndicho hicho anachokabidhiwa, kwa sababu hata yeye pia anapewa nafasi yakua anatazama procedures zote za gari yake hadi inapofika bandarini Dar es salaam

3. UNAFUU

Mteja anapoagiza gari kwetu, anapata unafuu wa bei kadharika wa gharama zingine ambazo angepaswa kuzilipia kwa wakati mmoja asilimia mia moja.
kwetu, mteja anapata nafasi ya kuzilipa kidogo kidogo kwa muda wa hadi. mwaka mmoja.

NOTE : HUDUMA HII SIO YA LAZMA, NI IWAPO MTEJA MWENYEWE ATAPENDA

Haya ni machache kati ya mengi.


karibuni sana

KAZI NI KWAKO !!!


EAPGS

MAFIATI AREA
MBEYA TANZANIA
WHATSAPP ONLY
+255 682 274 097
 
Nchi yako imekupa eneo la kufanya shughuli zako, barabara za kuendesha gari lako, ulinzi na vyuo vya kupata wanawake wako halafu hutaki kuongeza tumilioni kadhaa?
 
Uko sahihi sana mkuu.
Lakini pia kuna baadhi ya gari thamani ya CIF TRA wanaipandisha baada ya kipindi fulani kutokana na demand ya gari husika hivyo kupelekea kodi kuongezeka, nimetolea mfano T/IST model za miaka yote kodi zilipanda mwaka 2021.
 

Kuna hii kesi CIF ya TRA kuwa juu kuliko uhalisia au Bei iliyowekwa mtandao I ambayo ndio unailipa, hiyo inakuaje?

Yaani kitu kinauzwa Kwa $1000 lakini TRA anakwambia Bei ni $2000 au $1500.

Kingine unakuta gari unaiingiza kutolea Japan ila kwenye mfumo wa TRA wanakwambia imetokea Ulaya na hapo Kodi inatofautiana ( sijajua wanafikiria ni gari mpya na wanaangalia origin ya ilikotengenezwa?)
 
Kwanza TRA wao wanaangalia originality ya gari, wapi inapotengenezwa, lakini pia mfumo wao wa kucalculate Kodi wanatumia ile ya Bei ya gari ikiwa mpya au ndio kwanza ipo kiwandani inauzwa thamani yake ni kiasi gani? Kwa mfano labda IST mpya kabisa zilo km Japan inauzwa $4000 Basi TRA kwenye mfumo wao ukiingiza gari watacalculate Kodi kupitia thamani hiyo, lakini Kuna mambo mawili siku ukienda kuclear gari

01 gharama inaweza kuzid kulinganisha na ile ambayo wewe umeona kwenye website yao na hii inasababishwa na sababu ambayo nimeilezea hapo juu

02 gharama inaweza kupungua na hii huwa inasababishwa na invoice husika ya muuzaji amekuandikia kiasi gani

Lakini swala la msingi ambalo wauzaji wengi na waagizaji wengi wa magari hawaweki wazi kwenye Bei ni kwamba hizo used cars kutoka japan zinauzwa na zinapewa Bei kulingana na condition stage ndio maana unaweza kukuta gari aina moja, model moja, engine sawa na mwaka plus mwez wa usajili ni sawa na hata km zilizotembea zinalingana na rangi sawa Ila Bei ikatofautiana uliwah kujiuliza inasababishwa na Nini? Jibu ni hivi gari zote zinapewa Bei kulingana na condition stage gari iliyo na 3.0 condition stage haiwezi kuuzwa Bei sawa na iliyo na RA au 2.5, sasa hapa waagizaji wengi wenzangu hawawambii wateja wao na hata TRA hili hawawezi kujua hivyo unapolalamika ushuru kupanda jiulize je gari hii ingekua mpya thamani yake ni kiasi gani, na mm naichukua leo je itaangukia kwenye ushuru upi wa chakavu wa tra je ni 0%, 15% au ni 30%?
 
Na TRA wao hawaangalii Hilo gari ni chakavu, au mpya wao CIF yao wanatoa kwenye gari ikiwa mpya thamani yake ni Bei gani?
 
Safi sana, kuna watu wanadhani kila mtu yuko gizani! Zamani nlijua wakikuagizia bei inapungua labda wana connection kumbe njaa tupu wanataka waponee humo!
wana njaaa kupitiliza, yaani unakutana na dalali koromeo limemkauka akisubiria pesa yako akalewe double kick
 
umechungulia xchange rate mkuu???!!??
 
Unaonaje pia kaka/dada ukaweka ushahidi na uthibitisho hapa?
Pengine itakua busara zaidi ili kwenda sambamba na tahadhari yako.

Pia, sioni tija ya kukebehi watu kwa kuita wajinga, kwasababu tuu mmepishana kimawazo.

Hekima ni utajiri mkubwa sana.
Hawa wanaokuagizia ni matapeli wakubwa. Nishakutana na wanaoitwa MAGARIRAHISI ni matapeli. Wapo kibao kama hao. Matapeli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…