Usianzishe biashara wala kutafuta kazi kupitia waganga wa kienyeji

Usianzishe biashara wala kutafuta kazi kupitia waganga wa kienyeji

Ila ujue kila mahali penye utajiri au cheo kuna siri iliyofichika. Mungu hana upendeleo wa kumpa fulani na kumyima fulani. Mungu ni upendo, anampenda kila binadamu. Wengi wapo kwenye asilimia 5 yenye masharti magumu. Hakuna mtu mjasiri na mvumilivu kama tajiri, wengi wana roho ya paka.
 
"Ushirikina ni masharti na vigezo, na ushirikina huitaji update kila wakati"

"Yule mnyama uliyemtumia kutengenezea kafara nae ana muda wake wa kuishi, hivyo muda wake ukifika kikomo na kafara lako pia huisha"

Hizo nukuu zako hapo juu nimezielewa haswa.
Ngoja nikuongezee na hii

"Mnyama anayechinjwa kwa shughuli za ushirikina ni wazi analazimishwa kufa kabla ya muda wake wa kufa kutimia.. Vita yake yoyote ya kiroho baada ya hapo utaibeba wewe.. Kwahiyo utakuwa na vita mbili ama zaidi ya kupigana.. "

Muhimu sana.

SUKAH
 
Nimeelewa mkuu. Ndio maana hata maswali yangu yapo katika wakati uliopita. Ungeweza kujibu ingetusaidia kuelewa haya mambo zaidi.
OK sawa lakini maslahi yangu niliyotangaza bado yanajieleza wazi kwamba mimi sio mganga na sijawahi kuwa mganga wa kienyeji.. Ushirikina niliofanya mimi ni Fantasy witchcraft.. Huu hauna maagano wala hauna madhara kwa wengine na ndio maana niliweza kuuacha na kuokoka
 
Still mkuu unatunyima tu taarifa chache zinazoweza kutupa funzo. Hebu naomba niambie fantasy witchcraft ni nini
 
Ngoja nikuongezee na hii

"Mnyama anayechinjwa kwa shughuli za ushirikina ni wazi analazimishwa kufa kabla ya muda wake wa kufa kutimia.. Vita yake yoyote ya kiroho baada ya hapo utaibeba wewe.. Kwahiyo utakuwa na vita mbili ama zaidi ya kupigana.. "

Muhimu sana.

SUKAH
Mshana katujazia madini tupu, naona ningetakiwa copy & paste thread yote.
 
Natangaza maslahi yangu! Mimi sio mganga na sifanyi ushirikina tena..!

Kati ya waganga wote wa kienyeji ni asililia kumi hivi kati ya mia moja ndio wakweli na kati ya hao wakweli ni asilimia 5 tu ndio wenye masharti nafuu na wanaoweza kukusaidia moja kwa moja..! Ishu ya kuwajua feki na wakweli tutaona huko mbele

Kwanza lazima tukubaliane kuwa ushirikina ni utumwa, na ushirikina ni masharti na vigezo..Na ushirikina ni kitu chenye kuhitaji update kila wakati.. Na waganga wengi ni wapigaji..!

Pamoja na shida zako zote usijaribu kwenda huko kwenye ushirikina kutafuta 'assist' huko unaenda kufanya registration kwenye data base yao na hatimaye kuwa kwenye himaya yao..MAKINIKA!

Chochote kinachohusika na ajira ama biashara ukiachana na visomo vya kidini lazima kitahusisha damu.. Automatically itakuwa damu ya mnyama hasa mbuzi na ng'ombe ama kuku.. Kwa uchache kabisa na kwa siri kubwa damu ya mtu itahusika..

Mnyama anayechinjwa kwa shughuli za ushirikina ni wazi analazimishwa kufa kabla ya muda wake wa kufa kutimia.. Vita yake yoyote ya kiroho baada ya hapo utaibeba wewe.. Kwahiyo utakuwa na vita mbili ama zaidi ya kupigana.. Vita yako, vita ya kuku, vita ya mbuzi nknk.. Na hapa ndio siri ya side effect asiyokwambia mganga, Lakini lingjne ni hili... Yule mnyama aliyetumika kukutengenezea mambo yako ana ukomo wake wa kuwa, hivyo wakati wake wa kufa ukifika, kafara ulilotengenezewa nalo hufa rasmi..! Hapo ndio utaona mambo yako yanavyoanza kuyumba na hatimaye kuharibika kabisa

Lingine ni kwamba kuna wakati katika maisha mambo huenda mrama bila sababu yoyote ile..ni asili tu inafanya kazi, wewe kwa kuhofia kuwa tayari umeshapigwa na kitu kizito tena, utakimbilia kwa mtaalam wako tena, na yeye hata kama hakuna tatizo atalitengeneza na kukutisha sana.. Juu ya yote kwakuwa tayari uko kwenye database zao kuna wakati huamua kukorofisha mambo ili tu umuendee ajione bingwa ama kuna kitu umtimizie

Mwishowe unakosa kabisa ladha ya maisha unafanya biashara lakini hutulii ni makafara kwa kwenda mbele, una kazi yako nzuri Lakini masharti ni kama yote ...unapata pesa Lakini huna furaha nazo
Mganga naye ni binadamu akiamua kula bata hutengeneza tatizo kwakuwa kila mganga ni mchawi.. Pesa ya kutengeneza tatizo ndio huwa pesa ya starehe kwakuwa haimpi masharti kama ile pesa ya kilinge inayotokana na tatizo genuine!

Mwanzoni mwa biashara, ajira na hata mahusiano na miradi mingine epuka sana kuyanajisi na ishu za giza yasije yakaja kukutesa mbeleni, kwa kuwa kuingia huko ni rahisi sana lakini kutoka ni habari nyingine..Na ni shughuli pevu
hichi kichwa hiki kina madini mno jpo wengi humu hawajalifahamu hilo
 
Still mkuu unatunyima tu taarifa chache zinazoweza kutupa funzo. Hebu naomba niambie fantasy witchcraft ni nini
Hapana kaka trust me ningeweza kuroga kabisa mbona nisingehangaika na ajira na kipato kama wengine?[emoji23] fantasy witchcraft ni kwa ajili ya kujifunza zaidi na kufurahisha hadhira bila kudhuru uumbaji wowote..! Kwa nanma yoyote ile
 
Una exposure kwenye upande huo lakini sema labda tu hutaki kutuibia siri. Au labda masharti ya huko yanakubana ila fresh kaka asante kwa muda wako.
 
Back
Top Bottom