Usianzishe biashara wala kutafuta kazi kupitia waganga wa kienyeji

mkuu nawezaje kuzifut hizo signature?
Paka ndimu na chumvi.Pili kataa kabisa kuamini kwamba msaada wako unatoka huko.
Wema imani kwa Mungu Mkuu anaweza.
Ukifanya hivyo utakuwa umeswicth off bluetooth.
Yaani kujifuta kwenye usajili wao
 
Kaka Mshana Jr nisaidie katika hili please


Nimeona andiko lako kuhusu Biashara na ushirikina...naomba nisaidie jambo moja mimi ni mfanyabiashara kwa hapa mtaani ndo mfanyabiashara kinara wa shughuli za huduma za kifedha(Mpesa,Airtel,Bank etc) na kuuza Simu,,ofisi yangu mimi ndo msimamizi mkuu zaidi kuna kijana mmoja kama fundi ambae yeye kaweka meza yake kwa nje na mara chache sana wadogo zangu wakiwa likizo huwa wananisaidia japo watu huwa wananihisi ni mshirikina ila sijawahi kanyanga kwa mganga yeyote yule ila nawazaga sana kwenda siku moja kutafuta kinga ya biashara kwani kuna michezo kama ya chuma ulete huwa naona mwaka jana mwanzoni ilitokea sana unashangaa hesabu inapungua laki mbili ukicheki sms zotee za miamala ziko sawa ila hela hamna ukawa ni mchezo kila mwezi tar za 15-20 napoteza laki mbili hadi tatu,,nikawaza kwenda kwa mganga ila katika pitapita kuna jamaa nikasikia huwa ana michezo ya chuma ulete sana na mwanzoni hakuwa mteja wangu ila mwaka jana alinizoea sana kuwa anakuja na nilivopima siku nayoona hasara lazima alikuja kutuma pesa nikaona isiwe kesi kazi si yangu nikamtumia ujumbe wa kumuomba katika maisha yake yote asikanyage katika eneo langu la biashara wala kuisogelea wala kutuma mtu yeyote,,akataka kujua sababu nikamwambia nimeamua iwe hivyo,,alituma baadhi ya watu kunihoji nikawaambia hakuna sababu nimeamua sitaki kumuona,,tokea nimpige marufuku mambo yakaenda vizuri sana nashukuru Mungu kwa kweli kama miezi minne mfululizo(wa nane hadi 12) sijawahi pata loss yeyote ila juzi nahisi tena ule mchezo umerudi sijui ni nani tena kanisababishia ya laki mbili...


Kaka hebu naomba ushauri au maelekezo wapi naweza kwenda au nini nifanye kuidhibiti biashara yangu isichezewe kabisaa


Asante
 
Wew Mkuu barikiwa sna leo nakupa credit Mimi nimfatiliaji Mzuri WA mada zako Ila sio mchangiaji

Nimejifunza Mengi sna kupitia wew hasa haya Mambo ya uchawi, maji ya Baraka ect

God bless you.
Amina [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Uganga ama uchawi haupo, ni watu wenye akili fupi tu wanaweza kuamini kitu kinaitwa uganga, uchawi, ulozi ama ushirikina, ni watu wenye akili ndogo tu wanaamini hayo mambo.
Kwani umeshaona mambo yote duniani.naamini hujawa na kama hujawai kuona yote ya dunia sema wewe hujawai kuona ila usiseme kua jambo flani halipo kabisa duniani.Dunia ni zaidi ya uijuavyo wewe na binadamu wana mengi yakushangaza.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ushauri wangu
1. Ulipoteza na ukajizuia kwenda kwenye ushirikina...Ilikuwa ni test kwako baada ya kufaulu ukaongozwa kumjua aliyekuwa anakuchezea.. Sasa inarudi tena huoni kuwa huo ni mtihani mwingine unajaribiwa?
2. Sikushauri uende huko yaani ni sawa na kuruka mkojo ukanyage kinyesi... Huko utatishwa sana ili uwekwe sawa..
Kwenye biashara za fedha kuna ushirikina mwingi sana hivyo nakushauri kwenye droo yako ya pesa usikose kipande cha ndimu na cha chumvi ya mabonge
 
Asante kaka nitatafuta leo leo ndimu,,
 
Bila shaka 90% ya waliokupa Likes hapa wameshafanya sana Shirki na 10% iliyobaki ndiyo Sisi ambao hatujaufanya na kamwe hatutoufanya pia.

Hongera na Asante kwa Elimu hii Kubwa.
 
Uganga ama uchawi haupo, ni watu wenye akili fupi tu wanaweza kuamini kitu kinaitwa uganga, uchawi, ulozi ama ushirikina, ni watu wenye akili ndogo tu wanaamini hayo mambo.
Hahahaha kwamba wewe una akili kubwa kuliko manabii walio utambua upo?

Kwamba wewe una amini kuna Muumba ila uchawi haupo, wewe nae umeme kidogo kichwani.
 
Nini tofauti ya mapepo na majini?

Samahani kwa usumbufu mkuu.
Kiasili mapepo yanatokana na wafu na roho zinazohamanika.. Majini ni viumbe walioumbwa kwa moto na wasiotokana na wafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…