Usianzishe biashara wala kutafuta kazi kupitia waganga wa kienyeji

Usianzishe biashara wala kutafuta kazi kupitia waganga wa kienyeji

Nilienda akanipa dawa nichemshe ninywe kwa ajili ya tumbo. Leo narudi tena nahisi kale ka bibi kamenipa ndogo bado sijapona.

Kana dawa nyingi kanauzia sokoni, leo nitakauliza kwa utani kama ni kaganga[emoji23][emoji23][emoji23]

Kila nikienda nakaachia buku mbili nikakaomba hiyo dawa kanipe niipande kwangu kakakubali eti leo niende kanipe niipande.nikipona mchango ndo nitakaamini.
Hahaha[emoji23]
 
Freemason hawatumii ushirikina, kafara zao wanazofanya ni kwa ajili ya kujikinga na mabaya na wanafanya in a very smart way
Na hawa jamaa si kwa ajili ya makapuku ni mpaka wakuone umefikia level fulani ya cash au nafasi kwenye jamii ndio wanakuvuta kwao, huwatafuti wao bali wao wanakutafuta wewe
Hivi vyama vinavyotafuta wanachama mitandaoni ni vya kitapeli
Mkuu mshana wamenichanja huku mwenzio hata kama umestaafu nisaidie mawazo hii michale yao isinidhuru
 
Mkuu mshana wamenichanja huku mwenzio hata kama umestaafu nisaidie mawazo hii michale yao isinidhuru
Paka ndimu na limao na wala usipate hofu kabisa hakuna baya litakupata
 
Kila mnyama ana ibada yake wakati wa kuchinjwa.. Na hii ibada ni kuzuia mabaya yote yatokanayo na huko kuchinjwa kwake kwa mchinjaji na kwa mlaji .. Waislam wanajua sana hiki kitu
Huko vilingeni na kwenye madhabahu za giza mnyama anakatwa shingo na kuachwa arukeruke hadi kifo..huo ukatili hauna msamaha
Sasa chief, huku kwenye mabanda ya kuuza chakula, mahotel, bars n.k tunakuwa na uhakika kuwa hawa wanyama wanakuwa wamechinjwa au wamekatwa shingo na kuachwa warukeruke hadi kifo? Au tunajitoa tu sadaka wakati mwingine?
 
Ulimwengu wa ushirikina ni mkongwe na mpana mno..actually ukongwe wake ni tangu kuumbwa kwa dunia kiimani... Uchawi una kaliba na matabaka mbalimbali na mengi tuu ambako yote yako chini ya mwamvuli mkubwa wa ushirikina, humo kuna
Waganga wa jadi
Wachawi
Walozi
Wanga
Wafuga majini
Wafuga mapepo
Wazee wa kitabu nknk
Ni ngumu sana nasema ni ngumu sana sana kumkuta mmoja ni mjuzi na controller wa kaliba zote hizo.. Hiyo ni level ya juu mno!
Kuna watu ambao wamewahi kufikia level hizo?
 
Kila mnyama ana ibada yake wakati wa kuchinjwa.. Na hii ibada ni kuzuia mabaya yote yatokanayo na huko kuchinjwa kwake kwa mchinjaji na kwa mlaji .. Waislam wanajua sana hiki kitu
Huko vilingeni na kwenye madhabahu za giza mnyama anakatwa shingo na kuachwa arukeruke hadi kifo..huo ukatili hauna msamaha
Hapa nimekuelewa ndugu
 
MKUU.. nasikia huwa wanakwambia kafara ndogo (kuku,mbuzi,ng’ombe nk) mwanzoni alafu ukishaifanya kadri unavyoona mafanikio wanakuagiza / wanakubadilikia utoe kafara kubwa (watu.. ndugu na wazazi) hii inakuaje? Kama utakataa kuendelea nayo?
 
OK sawa lakini maslahi yangu niliyotangaza bado yanajieleza wazi kwamba mimi sio mganga na sijawahi kuwa mganga wa kienyeji.. Ushirikina niliofanya mimi ni Fantasy witchcraft.. Huu hauna maagano wala hauna madhara kwa wengine na ndio maana niliweza kuuacha na kuokoka
Umeokoka.....!!!!???
 
Sasa chief, huku kwenye mabanda ya kuuza chakula, mahotel, bars n.k tunakuwa na uhakika kuwa hawa wanyama wanakuwa wamechinjwa au wamekatwa shingo na kuachwa warukeruke hadi kifo? Au tunajitoa tu sadaka wakati mwingine?
Vyovyote iwavyo hukutenda wewe kwahiyo hapo huna mawaa
 
MKUU.. nasikia huwa wanakwambia kafara ndogo (kuku,mbuzi,ng’ombe nk) mwanzoni alafu ukishaifanya kadri unavyoona mafanikio wanakuagiza / wanakubadilikia utoe kafara kubwa (watu.. ndugu na wazazi) hii inakuaje? Kama utakataa kuendelea nayo?
Mara nyingi kafara za mafanikio huanza na mbuzi ama ng'ombe, lakini kafara sio kitu cha kudumu, lina kikomo cha kuwa .... Hapo kuna mawili likiisha nguvu lazima ufanye tena ama ukitaka kupanda viwango lazima ufanye tena..
 
Natangaza maslahi yangu! Mimi sio mganga na sifanyi ushirikina tena!

Kati ya waganga wote wa kienyeji ni asililia kumi hivi kati ya mia moja ndio wakweli na kati ya hao wakweli ni asilimia 5 tu ndio wenye masharti nafuu na wanaoweza kukusaidia moja kwa moja..! Ishu ya kuwajua feki na wakweli tutaona huko mbele

Kwanza lazima tukubaliane kuwa ushirikina ni utumwa, na ushirikina ni masharti na vigezo..Na ushirikina ni kitu chenye kuhitaji update kila wakati.. Na waganga wengi ni wapigaji!

Pamoja na shida zako zote usijaribu kwenda huko kwenye ushirikina kutafuta 'assist' huko unaenda kufanya registration kwenye data base yao na hatimaye kuwa kwenye himaya yao. MAKINIKA!

Chochote kinachohusika na ajira ama biashara ukiachana na visomo vya kidini lazima kitahusisha damu. Automatically itakuwa damu ya mnyama hasa mbuzi na ng'ombe ama kuku.. Kwa uchache kabisa na kwa siri kubwa damu ya mtu itahusika.

Mnyama anayechinjwa kwa shughuli za ushirikina ni wazi analazimishwa kufa kabla ya muda wake wa kufa kutimia. Vita yake yoyote ya kiroho baada ya hapo utaibeba wewe.. Kwahiyo utakuwa na vita mbili ama zaidi ya kupigana.. Vita yako, vita ya kuku, vita ya mbuzi nknk.. Na hapa ndio siri ya side effect asiyokwambia mganga, Lakini lingjne ni hili... Yule mnyama aliyetumika kukutengenezea mambo yako ana ukomo wake wa kuwa, hivyo wakati wake wa kufa ukifika, kafara ulilotengenezewa nalo hufa rasmi..! Hapo ndio utaona mambo yako yanavyoanza kuyumba na hatimaye kuharibika kabisa

Lingine ni kwamba kuna wakati katika maisha mambo huenda mrama bila sababu yoyote ile..ni asili tu inafanya kazi, wewe kwa kuhofia kuwa tayari umeshapigwa na kitu kizito tena, utakimbilia kwa mtaalam wako tena, na yeye hata kama hakuna tatizo atalitengeneza na kukutisha sana. Juu ya yote kwakuwa tayari uko kwenye database zao kuna wakati huamua kukorofisha mambo ili tu umuendee ajione bingwa ama kuna kitu umtimizie

Mwishowe unakosa kabisa ladha ya maisha unafanya biashara lakini hutulii ni makafara kwa kwenda mbele, una kazi yako nzuri Lakini masharti ni kama yote unapata pesa Lakini huna furaha nazo.

Mganga naye ni binadamu akiamua kula bata hutengeneza tatizo kwakuwa kila mganga ni mchawi.. Pesa ya kutengeneza tatizo ndio huwa pesa ya starehe kwakuwa haimpi masharti kama ile pesa ya kilinge inayotokana na tatizo genuine!

Mwanzoni mwa biashara, ajira na hata mahusiano na miradi mingine epuka sana kuyanajisi na ishu za giza yasije yakaja kukutesa mbeleni, kwa kuwa kuingia huko ni rahisi sana lakini kutoka ni habari nyingine. Na ni shughuli pevu

Mkuu nina ishu nataka kuuliza
Lakini nashindwa ku access dm
Kama unaweza ni dm kwanza ntashkuru
 
Back
Top Bottom