Usidanganyike! Sex meditation ni ibada za kishetani

Kuna mlango wa fahamu kwa kila mmoja ulifunguka uliokuwa umefungwa ambao haukutakiwa kufunguliwa ambao uliwaonyesha ukweli wa sehemu zao za siri.

Hapa ni utambuzi. Hata Mungu alipata mshangao nani amesema u uchi? Je umekula matunda ya mti wa katikati wa ujuzi na mema niliowakataza?

Kama ni kujamiiana walishaambiwa nendeni mkaijaze dunia na kuitiisha. Wengezaa vipi bila tendo la ndoa.

Kwanini Mungu aufiche tena huo mti na kuwafukuza bustanini, kama ni tendo wasingelifanya baada ya kufukuzwa bustanini. Hapa ndipo ninapoegemea.
Kwanini ufahamu ufunguke kwenye uchi na si kwenye akili? Hata kwenye milango nane ya fahamu uchi haumo.. Huoni kuna mashaka hapo?
 
Hawakuambiwa na yeyote isipokuwa fahamu zao zilifunguka baada ya kula tunda la mti wa katikati wa mema na mabaya.

Hili tunda liko hivi iwapo unaweza kulila sasa hivi hapo ulipo unapata nafasi ya kujua mambo mengi mema na mabaya ambayo ulikuwa hujui, siri za mbingu, siri za Mungu ambazo hutakiwi kuzijua.
Biblia ni mawazo ya wanadamu ya kinadharia yanayo daiwa kuwa ya Mungu bila uthibitisho kamili..waliomo kwenye biblia hawakuwa na biblia sasa aliye toa hizi taarifa za hawa watu ni nani? Labda useme biblia iliandikwa na Adamu mwenyewe la sivyo huyu Adamu ni mtu wa kufikirika na kusadikika....
 
Kisha wakasikia sauti ya BWANA Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, BWANA Mungu asiwaone. 9BWANA Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? 10Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. 11Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi?
Mshana mbona unaniangusha? Maarifa ya utambuzi wa mwanadamu yanatoka akilini au rohoni kwenye utu wa ndani na siyo mwilini, na Kuna vyakula ukila maarifa yako yanaongezeka kiasi cha kujitambua nakuondoka kwenye ujinga Mimi nafahamu kwa elimu uliyonayo ya mambo ya kiroho unajua kabisa Kuna vyakula gani ukila jicho lako la tatu linafunguka, na kujamiiana huwa kunakusogeza mbali na roho yako maana unakuwa unaunganisha roho nyingine muda huo ndo maana mpaka ujisafi kuondoa janaba ubaki wewe kama wewe, hilo tunda ni tunda la Kula Wala siyo tunda la kufanya, na Ili uamini hata dhambi zingine zinafanywa kwa kufanya kama kuua na kuiba ndo maana hiyo sex ni kufanya, ila hapo tunaambiwa walikula tunda na siyo kufanya, na kula ndo Kuna Siri kubwa hata kuishi kwa mwili Kuna vyakula vyake na hivyo hivyo kupata nguvu za kiroho pia Kuna vyakula vyake na wewe unalijua hilo.
 
Nimesita kwa muda kuweka hii mada lakini usiku huu baada ya meditation nimejikuta navutika kuiweka hapa lakini vilevile nikitimiza ahadi ya mdau Ms mol

Kwanza ni lazima tutambue kuwa ngono na tahajudi ni vitu vya kihisia zaidi kiroho zaidi kupitia jumbamwili linalowaka tamaa.

Tahajudi(meditation) ni somo moja pana sana lenye mazuri mengi na mabaya mengi. Tahajudi inatumiwa na:

Matapeli
Wafanya mazingaombwe
Wanasiasa
Wafanyabiashara
Wanazuoni
Washika dini (mitume na manabii)

Waabudu sanamu na nguvu za giza kama imani za kishetani nk
Wote tunajua nguvu ya ngono na hii ndio dhambi ya asili, Adamu aliangukia hapa, Samsoni wa Delila hapa hapa, mfalme Suleimani na hekima zake alikuwa na wake mia tatu na masuria idadi hiyo hiyo (hapa King Mswati anasubiri sana)

Ngono imewaangusha wengi sana kuanzia washika dini, viongozi mbalimbali mpaka watu wa kawaida kabisa

Tahajudi inatumiwa na kutumika vibaya na watu wenye agenda za siri, agenda za kukidhi tamaa zao za mwili kwa jina la tahajudi.

Kuna wenye kumaanisha lakini ni wachache mno, wengi wanaofanya sexual meditation ni wale wa imani za kishetani bila kujitambulisha wazi, lakini pia ndani ya ibada za kishetani, ngono ni kipengele kimoja muhimu sana. Nimehudhuria nimeona.

Najua Wengi wana munkari wa kutaka kufanya meditation, lakini ni vema sana ukawa makini na kile unachotarajia ama kutaka kufanya.

Mambo mengi siku hizi yamefanyiwa kolabo. Jihadhari sana unapojifunza hizi elimu ngeni

Alamsiki

Jr.!
8d360ad30bcff26152135b63c50d57d5.jpg
Mleta mada nadhani nimuda sasa wakufanyia maboresho ya kile ulichokiandika maana kina mapungufu mengi
 
Biblia ni mawazo ya wanadamu ya kinadharia yanayo daiwa kuwa ya Mungu bila uthibitisho kamili..waliomo kwenye biblia hawakuwa na biblia sasa aliye toa hizi taarifa za hawa watu ni nani? Labda useme biblia iliandikwa na Adamu mwenyewe la sivyo huyu Adamu ni mtu wa kufikirika na kusadikika....
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]sawa.

Mafunuo ya Roho Mtakatifu unayajua?
 
Tunda ni zaidi ya tafsiri ya matunda mnayofahamu
Ninaweza kukuelewa na kukubaliana na wewe na ndio maana nikasema ni fumbo na ujuzi wa mema na mabaya.

Kama ni ngono kwanini hatukupata maarifa zaidi maana tunafanya kila siku.

Kama ni zaidi ya tunda la kawaida kwanini zile siku za mwisho tutakula tunda kila mmoja ili tusitende dhambi tena. Je tutafanya ngono?
 
Kwanini ufahamu ufunguke kwenye uchi na si kwenye akili? Hata kwenye milango nane ya fahamu uchi haumo.. Huoni kuna mashaka hapo?
Sehemu ya mwili wa mwanadamu hasa mtu mzima kama Adam na Hawa Ni sehemu zipi zinazohotajika kuzibwa na zinazoonewa aibu Ni zipi kama siyo viungo vya uzazi?

Ni dhahiri walipojikuta wamepata ufahamu wakajizipa mwanzo Mungu hakuwa amewapa ufahamu huo.

Na badaye Mungu aliwatengenezea mavazi akawavika aliona majani hayawahahi tena.
 
Mshana mbona unaniangusha? Maarifa ya utambuzi wa mwanadamu yanatoka akilini au rohoni kwenye utu wa ndani na siyo mwilini, na Kuna vyakula ukila maarifa yako yanaongezeka kiasi cha kujitambua nakuondoka kwenye ujinga Mimi nafahamu kwa elimu uliyonayo ya mambo ya kiroho unajua kabisa Kuna vyakula gani ukila jicho lako la tatu linafunguka, na kujamiiana huwa kunakusogeza mbali na roho yako maana unakuwa unaunganisha roho nyingine muda huo ndo maana mpaka ujisafi kuondoa janaba ubaki wewe kama wewe, hilo tunda ni tunda la Kula Wala siyo tunda la kufanya, na Ili uamini hata dhambi zingine zinafanywa kwa kufanya kama kuua na kuiba ndo maana hiyo sex ni kufanya, ila hapo tunaambiwa walikula tunda na siyo kufanya, na kula ndo Kuna Siri kubwa hata kuishi kwa mwili Kuna vyakula vyake na hivyo hivyo kupata nguvu za kiroho pia Kuna vyakula vyake na wewe unalijua hilo.
Sasa hili ni jambo jipya kwangu..
Mkuu,anzisha uzi mwingine kuhusu hili tafadhali.
 
Sehemu ya mwili wa mwanadamu hasa mtu mzima kama Adam na Hawa Ni sehemu zipi zinazohotajika kuzibwa na zinazoonewa aibu Ni zipi kama siyo viungo vya uzazi?

Ni dhahiri walipojikuta wamepata ufahamu wakajizipa mwanzo Mungu hakuwa amewapa ufahamu huo.

Na badaye Mungu aliwatengenezea mavazi akawavika aliona majani hayawahahi tena.
Tatizo sio kuzibwa tatizo ni ufahamu na kwanini wakawa na aibu ya 'ufahamu' wakati walikuwa wenyewe Eden?
 
Hivi Mshana Jr bila shaka unajua maana ya kushuhudiwa ndani yako, kujihisi una hatia baada ya kutenda kosa haijalishi upo kwenye watu au uko peke yako. Nafsi inapokusuta inakukosesha amani mpaka unapotubu ndio unapata afueni na amani inarejea.

Adam na Hawa walikuwa wametenda dhambi ya uasi kwa kukataa kutii amri ya Mungu wao kutokula tunda,sasa ile asili ya utu wa ndani ilifedheheka, dhambi waliyotenda ilipelekea majuto na kuwaletea aibu ndio maana waliposikia sauti ya Mungu wao wakajua atawaona wako uchi ndio kisa wakajificha.

Kwa mtazamo wangu inaitwa dhambi ya asili kwasababu ni dhambi ya kwanza kutendwa na mwandamu kwa kukataa kutii maagizo ya Mungu wake. Dhambi ni uasi, uasi ni kuwa kinyume na maelekezo, sheria, kanuni ulizopewa uzifuate.
 
7seven kuna kitu hapa watu wanashindwa kukifafanua vizuri iwe kiroho na hata kimwili pia
1. Kuna bustani ya Eden ambayo ni makazi ya Adam na Eva
2. Kuna miti ya matunda mbalimbali kwa ajili ya chakula cha wawili hao ama watatu ( hapa pia inaibuka dhana ya vegan ila tuiweke pembeni kwasasa)
3. Kati ya miti yote kuna 'mti wa kati' wa ujuzi wa mema na mabaya! Huu wanakatazwa wasile matunda yake.. Maana wakila watakufa.. Kuna dhana ya kifo hapa
4. Kuna nyoka/ibilisi.. Je huyu naye ni mkazi wa Eden?
5.kuna ushawishi wa huyo nyoka kwa Eva? Kwanini asiwe Adam?
6. Kuna dhana ya kula tunda na kutokufa na kujua mema na mabaya
7. Baada ya kula tunda wanafumbuliwa na kujiona wako uchi!

Swali langu! Kwa nini ufahamu uwapeleke kwenye kuwaonesha utupu na si maarifa mengine?
 
Maswali yako yana mashiko.

Kwanini walikula na wakajikuta wako uchi.

Uchi kiroho ni hali ya kutokuwa na nguvu ya Mungu, utukufu wa Mungu umeondoka kabisa juu ya mtu.

Nguvu ya Mungu au Utukufu wa Mungu ndio unaokuleta karibu na Mungu, unaleta mahusiano ya karibu au mazuri.

Sasa Adam alipokuwa ametenda dhambi hakuwa na ule uwezo wa kumkaribia Mungu maana hana tena nguvu au utukufu na ukamilifu wa kuwa karibu naye tena ndio maana alijificha.

Uchi unaweza kuwa umetumiwa kama Lugha ya picha kumaanisha yu mwepesi hana nguvu tena baada ya kutenda dhambi, kwasababu ni wanadamu ile nguvu ya utukufu wa Mungu ilikuwa ndani ya miili yao.

Tumuangalie Samson. Nguvu zake zilikuwa katika nywele zake mashumi 7,jiulize swali zile nguvu zilikuwa zinatendaje kazi?

Ni kwasababu katika nywele zimefunikwa na utukufu wa Mungu, ndipo lilipo fumbo la nguvu zake. Pasipo nywele hawezi kufanya kazi ya Mungu inayomuhitaji kuwa na nguvu.

Mfano mwingine Daudi. Asingeweza kumpiga Goliath kama siyo utukufu wa Mungu kupitia lile jiwe la kombeo, unapata picha hapa.

Ndani ya jiwe ndipo palipokuwa na nguvu ya Mungu iliyomuua Goliath. Kwahiyo kwenye jiwe bado ni fumbo. Jiwe la kawaida lisingeweza kumuua yule pandikizi la mtu.

Kwahiyo uchi kama uchi na tunda ni fumbo la imani lakini tunda halimaanishi tendo la ndoa, ni uharibifu wa mahusiano ya kimungu na mwanadamu.
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]sawa.

Mafunuo ya Roho Mtakatifu unayajua?
Roho mtakatifu ni nini? Ukisha sema roho ni undefined creature zisizo na ubinadamu...wala hazina uhalisia na uthibitisho Roho ni imagination thing haionekani kwa macho...
 
7seven kuna kitu hapa watu wanashindwa kukifafanua vizuri iwe kiroho na hata kimwili pia
1. Kuna bustani ya Eden ambayo ni makazi ya Adam na Eva
2. Kuna miti ya matunda mbalimbali kwa ajili ya chakula cha wawili hao ama watatu ( hapa pia inaibuka dhana ya vegan ila tuiweke pembeni kwasasa)
3. Kati ya miti yote kuna 'mti wa kati' wa ujuzi wa mema na mabaya! Huu wanakatazwa wasile matunda yake.. Maana wakila watakufa.. Kuna dhana ya kifo hapa
4. Kuna nyoka/ibilisi.. Je huyu naye ni mkazi wa Eden?
5.kuna ushawishi wa huyo nyoka kwa Eva? Kwanini asiwe Adam?
6. Kuna dhana ya kula tunda na kutokufa na kujua mema na mabaya
7. Baada ya kula tunda wanafumbuliwa na kujiona wako uchi!

Swali langu! Kwa nini ufahamu uwapeleke kwenye kuwaonesha utupu na si maarifa mengine?
Bustani ya Eden.

Hii kwa mujibu wa Biblia ilikuwa duniani. Ilikuwa ni sehemu yenye raha, hakukuwa na majuto wala uchungu na ilikuwa inalindwa na kutunzwa na Adam

Kwanini ilindwe na kutunza? Sababu wangetokea waharibifu. Mungu alishajua yupo ambaye angetokea na kuharibu.

Shetani ni roho ya uharibifu. Shetani haji kwa umbo halisi, anakuja katika mawazo yenye ushawishi hasi.

Shetani alishajua kwamba Adam na Hawa wana maisha mazuri sana na wamekatazwa kula mti wa matunda ya katikati wenye ujuzi wa mema na mabaya. Kumbuka shetani aliishi mbinguni anaijua kwa kiasi chake, kwahiyo anajua mambo mengi sana ya huko.

Alichofanya ni kumshawishi Hawa kwa kumdanganya ale matunda yale halafu baadaye ampe na Adam.Shetani hana umbo halisi,kama alimpa tunda Hawa halafu baadaye Hawa akaja kumpa Adam ,sasa walifanyaje ngono wakati shetani hana mwili?

Mwanamke siku zote ni mdadisi, anapenda vitu vizuri, ule mti ulikuwa unatamanisha kwa uzuri, katika moyo wake alishaanza kuutamani ndipo kwa kuusoma moyo wake akamuijia mawazoni na kumshawishi ale maana hatakufa kama Mungu alivyowaambia sema atakuwa sawa na Mungu.

Kisha akapewa tunda na shetani akala, badaye akampa mume wake. Kumbuka wakati shetani anakuja Adam hakuwepo.Shetani alijua atampata Adam kupitia kwa udadisi wa mke wake.

Bustani ilikuwepo hapa duniani. Baada ya dhambi ilifichwa pamoja na mti wake wa ujuzi na mema.
 
Roho mtakatifu ni nini? Ukisha sema roho ni undefined creature zisizo na ubinadamu...wala hazina uhalisia na uthibitisho Roho ni imagination thing haionekani kwa macho...
Kuwa muwazi kwamba unataka kujua nini maana ya Roho Mtakatifu na mambo ya kiroho.

Swali unaamini uwepo wa Mungu, kwamba ni muweza wa kila kitu?
 
Maswali yako yana mashiko.

Kwanini walikula na wakajikuta wako uchi.

Uchi kiroho ni hali ya kutokuwa na nguvu ya Mungu, utukufu wa Mungu umeondoka kabisa juu ya mtu.

Nguvu ya Mungu au Utukufu wa Mungu ndio unaokuleta karibu na Mungu, unaleta mahusiano ya karibu au mazuri.

Sasa Adam alipokuwa ametenda dhambi hakuwa na ule uwezo wa kumkaribia Mungu maana hana tena nguvu au utukufu na ukamilifu wa kuwa karibu naye tena ndio maana alijificha.

Uchi unaweza kuwa umetumiwa kama Lugha ya picha kumaanisha yu mwepesi hana nguvu tena baada ya kutenda dhambi, kwasababu ni wanadamu ile nguvu ya utukufu wa Mungu ilikuwa ndani ya miili yao.

Tumuangalie Samson. Nguvu zake zilikuwa katika nywele zake mashumi 7,jiulize swali zile nguvu zilikuwa zinatendaje kazi?

Ni kwasababu katika nywele zimefunikwa na utukufu wa Mungu, ndipo lilipo fumbo la nguvu zake. Pasipo nywele hawezi kufanya kazi ya Mungu inayomuhitaji kuwa na nguvu.

Mfano mwingine Daudi. Asingeweza kumpiga Goliath kama siyo utukufu wa Mungu kupitia lile jiwe la kombeo, unapata picha hapa.

Ndani ya jiwe ndipo palipokuwa na nguvu ya Mungu iliyomuua Goliath. Kwahiyo kwenye jiwe bado ni fumbo. Jiwe la kawaida lisingeweza kumuua yule pandikizi la mtu.

Kwahiyo uchi kama uchi na tunda ni fumbo la imani lakini tunda halimaanishi tendo la ndoa, ni uharibifu wa mahusiano ya kimungu na mwanadamu.
Bado kuna siri kubwa na mkanganyiko mkubwa na tafakuri yake si ya kitoto wala mijadala yake haihitaji majibu mepesi
 
Back
Top Bottom