NDIYO inawezekana kwa talaka kutoka pasipo uwepo (phsically) wa mwanandoa mahakamani, lakini ni lazima atawasilishwa na mtu anayetambulika kisheria (kwa power attorney), hususani kwa mazingira unayosema kuwa wanandoa wamekubaliana kuachana.
Power of Attorney inaruhusu mtu mwingine kumuwakilisha mahakamani na kutoa ushahidi kwa niaba yake mtu huyo ikiwa mwenye kesi yupo nje ya nchi au ni mgonjwa sana.
Hata hivyo, sio wanandoa ndio wataoamua kuwa ndoa yao imevunjika kiasi ch kutotengenezeka, bali mahakama ndio itakayoamua. Kwa hiyo pamoja na kuwa wamekubaliana kuachana, mahakama inaweza kutotoa talaka ikiwa inaona ndoa hiyo haijaharibika kihivyo.