Usidanganywe na stori za vijiweni, ijue Sheria ya Ndoa na Talaka

Usidanganywe na stori za vijiweni, ijue Sheria ya Ndoa na Talaka

Je ikitokea wanandoa Wana kesi ya Talaka ambapo kesi imetumia muda mrefu zaidi ya Miaka 5 ( ikiwapo rufaa za kutosha).Endapo mwana ndoa mmoja akafariki wkt bado hukumu ya rufaa haijatoka, je Mali walizochuma zitakuwa chini ya umiliki wa nani?
 
Mtashtakiwa ugoni, mdaiwe fidia kama Profesa wa SUA na manzi wake wa CRDB😅😅
Mkuu

Mgawanyo wa asilimia wa mirathi kuanzia mke,watoto,wazazi na ndugu upoje!!?

Na Hii dhana ya wanawake ku tu kill wanaume na kurithi mali ni dhana tu au ina ukweli kwamba wake wanarithi vingi kuliko ndugu!!?

Tunaomba majibu Ili tujitoe kwenye club ya" kataa ndoa" na hofu ya vifo vya kukusudiwa hasa vya kishirikina ambavyo serikali haitambui ushirikina!!

Tiririka nipo NASUBIRIA kusoma!
 
Je ikitokea wanandoa Wana kesi ya Talaka ambapo kesi imetumia muda mrefu zaidi ya Miaka 5 ( ikiwapo rufaa za kutosha).Endapo mwana ndoa mmoja akafariki wkt bado hukumu ya rufaa haijatoka, je Mali walizochuma zitakuwa chini ya umiliki wa nani?
Kesi za Talaka ni kesi za madai na hivyo sheria ya mwenendo wa madai (The Civil Procedure Code Cap 33 R.E 2019 hutumika. Mdai au mdaiwa anapokufa, kesi husimama kwa muda ili apatikane msimamizi wa mirathi wa marehemu ndiye aendelee na kesi. Kwa hiyo, vivyo hivyo, mali walizochuma ikitokea mahamaka imezigawa, basi marehemu atabaki nazo ila kwa uangalizi wa msimamizi wake wa mirathi.
 
Mkuu

Mgawanyo wa asilimia wa mirathi kuanzia mke,watoto,wazazi na ndugu upoje!!?

Na Hii dhana ya wanawake ku tu kill wanaume na kurithi mali ni dhana tu au ina ukweli kwamba wake wanarithi vingi kuliko ndugu!!?

Tunaomba majibu Ili tujitoe kwenye club ya" kataa ndoa" na hofu ya vifo vya kukusudiwa hasa vya kishirikina ambavyo serikali haitambui ushirikina!!

Tiririka nipo NASUBIRIA kusoma!
Mgawanyo wa mirathi hufanywa na msimamizi wa mirathi vile apendavyo, hakuna asilimia maalum zilizowekwa (isipokuwa kwenye mifuko ya jamii wao ndio wana kanuni zao za kugawa yale mafao kwa warithi wa marehemu ambapo mtoto mdogo hupata kikubwa kuliko wengine, na mke au mume hupata kidogo kidogo kuliko watoto).

Hata hivyo, kuepusha migogoro isiyo na msingi, mahakama ilishauri kuwa msimamizi wa mirathi agawe mali baada ya kujadiliana na kukubaliana na warithi. Ikiwa warithi hawakubaliani basi msimamizi wa mirathi anagawa mali atakavyo.

Hata hivyo, somo la mirathi linakuja, tutaelezana kwa kina pia, tuombe uzima.
 
Asante kwa someone zuri
Swali..nikiishi na mwanamke tukapata na mtoto (Bila ndoa ya aina yoyote) naweza kuooa mke mwingine kwa ndoa rasmi..
Ikitokea n
 
Asante kwa someone zuri
Swali..nikiishi na mwanamke tukapata na mtoto (Bila ndoa ya aina yoyote) naweza kuooa mke mwingine kwa ndoa rasmi..
Ikitokea n
Ndiyo unaweza kuoa kwa ndoa rasmi lakini itakuwa ni ndoa ya wake wengi
 
Mkuu

Mgawanyo wa asilimia wa mirathi kuanzia mke,watoto,wazazi na ndugu upoje!!?

Na Hii dhana ya wanawake ku tu kill wanaume na kurithi mali ni dhana tu au ina ukweli kwamba wake wanarithi vingi kuliko ndugu!!?

Tunaomba majibu Ili tujitoe kwenye club ya" kataa ndoa" na hofu ya vifo vya kukusudiwa hasa vya kishirikina ambavyo serikali haitambui ushirikina!!

Tiririka nipo NASUBIRIA kusoma!
Kwenye mirathi ndugu wanaingiaje? Mirathi ni ya mke na Watoto, au kama amekufa mke hapo ndio Wazazi wake wanaweza kuwa sehemu ya wanufaika wa Mirathi hiyo.
 
KANUNI YA KUGAWA MALI 50-50 BAADA YA TALAKA HAITATUMIKA TENA! MAHAKAMA YA UPEO

Katika kesi ya talaka, kila mhusika anapaswa kuacha ndoa na mali aliyoipata wakati wa muungano" - Mahakama.
Muhtasari
• Majaji wakuu waliamua kwamba masharti ya Ibara ya 45(3) ya Katiba kuhusu usawa katika ndoa hayaruhusu mahakama yoyote kubadilisha haki za umiliki zilizopo za wahusika.

• Majaji wakuu waliamua kwamba masharti ya Ibara ya 45(3) ya Katiba kuhusu usawa katika ndoa hayaruhusu mahakama yoyote kubadilisha haki za umiliki zilizopo za wahusika.
Wenzi wa ndoa hawana haki ya moja kwa moja ya asilimia 50 ya sehemu ya mali ya ndoa baada ya talaka, Mahakama ya Juu imeamua kusuluhisha mojawapo ya masuala yenye utata katika Sheria ya Familia.

Ikitangaza kuwa kanuni ya 50:50 haitumiki kabisa, mahakama ya juu ilisema kwamba katika kesi ya talaka, kila mhusika anapaswa kuacha ndoa na mali aliyoipata wakati wa muungano ingawa mwenzi anaweza kupata zaidi kulingana na mchango wake katika ndoa na upatikanaji wa mali ya ndoa.

Mahakama ya majaji watano ikiongozwa na naibu jaji mkuu Philomena Mwilu pia ilishikilia kuwa kila mwenzi katika ndoa lazima athibitishe mchango wake katika utajiri wa familia ili kuwezesha mahakama kuamua asilimia inayopatikana kwake katika ugawaji wa mali ya ndoa.

Mahakama ilisema kuwa mtihani wa kuamua kiwango cha mchango wa mhusika ni mojawapo ya msingi wa kesi.

Uamuzi huo unatarajiwa kutoa sura ya ugomvi wa kisheria kati ya waume zao wa zamani na wake wa zamani kuhusu kugawana mali baada ya ndoa zao kusambaratika.

Majaji wakuu waliamua kwamba masharti ya Ibara ya 45(3) ya Katiba kuhusu usawa katika ndoa hayaruhusu mahakama yoyote kubadilisha haki za umiliki zilizopo za wahusika.

Masharti hayo yaliyotajwa kufanya kazi tu kama njia ya kutoa usawa wakati wa kuvunjika kwa ndoa huku kila mhusika akiwa na haki ya kupata mgao wao wa haki wa mali ya ndoa, ilisema mahakama.
 
Back
Top Bottom