Usifanye kosa la kutoa nafasi ya Mungu kwa ajili ya kumpendezesha bosi

Usifanye kosa la kutoa nafasi ya Mungu kwa ajili ya kumpendezesha bosi

Mwl Mwakujonga

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2023
Posts
384
Reaction score
758
Mungu siku zote hatabakia kuwa Mungu na nafsi yake ni yakwaza hana mbadala

Yusufu akiwa kwa potifa alikutana na mtihani kati ya kuchagua kumpendezesha mke aa potifa au kumpendezesha Mungu, na Yusufu akachagua kumpendezesha Mungu

Tumekuwa na changamoto kwa watumishi wa sekta binafsi au serikali kuwa na tabia ya kubadilika kulingana na mazingira kwa lengo la kuwapendezesha viongozi

Unakuta kabla haujapata kazi ulikuwa ni mtumishi mzuri wa Mungu ulikuwa ni muimbaji wa kwaya na haukosi vipindi vya kwaya lakini mara baada ya kupata kazi umeacha kumtumikia Mungu kwa njia ya nyimbo

Daniel alijua ushindi wake ni mahusiano yake na Mungu ndio maana hakukubali kula chakula cha mfalme kwa sababu alijua chakula ni njia koja wapo ya kumtenga na Mungu wake

Ulikuwa mtumishi mzuri wa Mungu siku ya jumapili ulikuwa busy na kazi ya Bwana ila mambo yamebadilika umepanda cheo unafanya kazi hadi jumapili , ile nafasi ya Mungu ambayo ulikuwa unatoa kwa siku ya jumapili kama kumpe heshima Mungu umeiondoa kwa kusema kazi ni nyingo ukasahau kwamba sio kwa wingi wa kazi ulizokuwa unafanya ndizo zilizokupa upendeleo kwa Mungu bali ni mahusiano yako na Mungu

Yusufu alijua kilichokuwa kinampa kibari katika kazi ya potifa ndio maana hakukubali kukosana na Mungu kwa ajili ya mke wa potifa


Daniel kipindi cha mfalme Dario alipewa mtihani wa kutokumwabudu Mungu kwa siku 30 tu,Lakini Daniel alijua kilichokuwa kinampa kibari kwa mfalme ni uhusiano wake na Mungu ndio maana hakukubali kumkosa Mungu kwa ajili ya kazi

Leo hii tumecha kusali, tumeacha mikesha , tumeacha maombi , tumeacha kusoma neno la Mungu kwa ajili ya kuwapendez wanadamu, ni kweli kazi ni nyingi lakini kwanini kazi zichukue nafasi ya Mungu ? Kwa nini kazi zisichukue nafasi ya kupumzika?

Nimeona wale ambao walikubali kupoteza mahusinao yao na Mungu kwa ajili ya kazi mwisho wa siku kazi zao zilikuja kukosa ubora na kukosa kibari kwa viongozi wao , sio kwamba hawakuwa wanafanya kazi vizuri hapana walifanya vizuri sana na kunavipindi wanakesha maosfini kwa lengo la kuboresha kazi zao lakini mwisho wa siku kazi zao zilikosa ubora au kibali kwa viongozi wao, kitu ambacho hatujui wana wa Mungu popote tulipo kadri Yesu anapopata heshima kadhalika na sisi tunapata heshima

Tunapokuwa kazini sisi ni punda ambao tumembeba Yesu na kwa sababu Yesu yuko juu yetu tutaendelea kupata heshima lakini Yesu akishuka siku hiyo ndio tutajua kwamba heshima yetu ilibebwa na Jina la Yesu.


Siku zote kumbuka punda aliyembeba Yesu alipata sifa na heshima kwa sababu Yesu alikuwa juu yake kadhalika sisi Yesu amapokuwa ndani yetu na anapata heshima katika utumishi wetu kadharika sisi

Ester alisahau kwamba kilichompa sifa ya kuolewa na mfalme ashuero sio kwamba alikuwa mzuri kuliko wanawake wote hapana ni kwa sababu alimbeba Yesu, inawezekana ndoa yako imeyumba kumpe uzuri wako ambao mume au mkeo aliuona ni kwa sababu ulikuwa umebebwa na Bwana siku Bwana akiondoka ujue na uzuri wako umeondoka na Mungu atusaidie
 
Mwl Umenyooka sana 🙏🙏... Ila hapo umeandika "hatabaki" unageuza maana kabisa au Mimi ndio sijaelewa.?
#Shida zetu zisifanye tukampa Mwanadamu nafasi ya Uungu...
 
Back
Top Bottom