Usifanye ujinga wa kumbadilisha ‘mwanamke aliyeharibika’ ili uishi naye

Usifanye ujinga wa kumbadilisha ‘mwanamke aliyeharibika’ ili uishi naye

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Mahusiano ya kudumu hayataki mbwembwe.

Mahusiano ya kudumu hayataki hisia kuzidi akili.

Mahusiano ya kudumu yanahitaji uhalisia sio kuigiza.

Mahusiano ya kudumu yanahitaji msingi mzuri kuanzia mwanzo.

Niamini mimi, mbwembwe na maigizo vitafika mwisho na hamtaelewana ila mkichukuana katika uhalisia mtaishi sana tu.

Usijibadilishe ili umpate kaka.

Unapotaka mahusiano ya kudumu hakikisha umefanya uchunguzi na kuona kwamba mwanamke anajaa kwenye hesabu za mifumo yako.

Mwanamke anaweza kuacha baadhi ya mambo yake ili awe na wewe.

Mwanamke anaweza kupoteza uhuru wake ili awe na wewe.

Usihitaji mahusiano ya kudumu kwa mtu wa kula na kusepa, itakuumiza.

Usimbadilishe mwanamke alieharibika ili awe mtu bora kwako, hiyo sio kazi yako. Badala yake tafuta ambaye tayari kalelewa vizuri.
 
Kesho beba bango lenye maandishi yafuatayo.

Hatuna Nchi nyingine zaidi ya Tanzania. Tuilinde amani ni mtaji wetu,
Tuitunze,
Tusikilizane,
Tuheshimiane,
Tushikamane.
 
Kesho beba bango lenye maandishi yafuatayo.

Hatuna Nchi nyingine zaidi ya Tanzania. Tuilinde amani ni mtaji wetu,
Tuitunze,
Tusikilizane,
Tuheshimiane,
Tushikamane.
Upo nje ya mada
 
Wapo waliobadilika na wanazo familia bora kabisa !!

Muda mwingine changamoto za maisha zinawabadilisha tu, huwa wanabadilika !
Tabia ya mtu haibadiliki tabia ni kama ngozi je unaweza kuibadilisha ngozi? Hao unaosema wamebadilika wameficha makucha
 
Mtoa mada unaongea hayo kwanza hujaoa wewe. Ipo hivi mwanamke huwezi kumjua tabia yake bila kuwa naye(Kuoa) kumchunguza kabla ya kumuoa bado siyo kipimo direct cha kujua tabia yake. Unachotakiwa kufanya we oa tu itajulikanq mbele ya safari. Kuna vitu vingine kwa upeo wa kibinadamu hatuwezi ila Mungu ndo kila kitu. Huwezi mpata mwanamke ambaye ni perfectly 100%. Kumbuka hata wewe ni kipengele kwanini wakitazama kibanzi kilichopo kwa mwenzio ilihali huangalii bolti ndani ya jicho lako mwenyewe?
 
Naunga mkono hoja.
 
Kesho beba bango lenye maandishi yafuatayo.

Hatuna Nchi nyingine zaidi ya Tanzania. Tuilinde amani ni mtaji wetu,
Tuitunze,
Tusikilizane,
Tuheshimiane,
Tushikamane.
Wapumbavu kweli hawa, yaani uibe uchaguzi, uue, utese na kuumiza kisha uje na meseji za kipumbavu namna hii??
 
Back
Top Bottom