nsanzu
JF-Expert Member
- Jul 29, 2015
- 4,673
- 5,402
Jomba iko hiviUnahangaika kutafuta mali kula na mademu na kuhudumia mahawara ukifa washikaji zako wanakuja kukomba mali kwa jina la watoto wako uliozaa na hawara. Ukiangalia hauna ndugu ambaye ana maisha mazuri na anaweza kutetea wanao. Unakufa unaacha ndugu hawana hata hela ya kufungua kesi na kuajiri wakili sembuse ya kuhonga Jaji. Kuna ile ishu ya Shamimu Mwasha na mumewe walipelekwa Jela ndugu zao wanaishi magomeni. Ilibidi watoto waondoke Mbezi Beach waende kuishi magomeni. Jamaa angewabeba ndugu zake wanae wangekuwa wanaishi maisha mema. Nimeona mengi sana kuna kiwanja nimenunua bei chee kwa sababu marehemu ameacha ndugu darasa la saba 😂 😂 😂 😂 . Ukiangalia mke hajui hata process za kuomba mkopo benki. Huku nyumba zake ndogo wengi ni mabaamedi. Kiulaini nikachukua kiwanja ni uzembe wetu sisi wanaume. Sisemi kuwa mimi ni mtakatifu lakini tukumbuke kumwomba Mungu atuepushie hili.
Baba na mama ikomboeni familia yenu kwa kila nyanja fulu stopu.