Watanzania wote tunapaswa tuitii na kuiheshimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977
Katika Katiba hiyo, ibara ya 71(1)(e) inatamka wazi kuwa "Ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge, basi ubunge wake utakoma" mwisho wa kunukuu
Huyu Cecil Mwambe tarehe 15/02/2020 alikihama chama chake cha Chadema na kupokelewa katika ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi kwa mbwembwe nyingi na bashasha na Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally na kukabidhiwa kadi ya CCM, mbele ya makamera ya waandishi wa habari
Ule msemo wa ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni ndiyo haya anayoyafanya Spika Ndugai, ambaye ameamua kuisigina sigina Katiba ya nchi yetu na kuamua kuwa ubunge wa Cecil Mwambe haujakoma na anaendelea nao!
Cha ajabu zaidi Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, tayari alishamwandikia barua, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumtaarifu kuhusu kukoma kwa ubunge wa Cecy Mwambe, kutokana na kuhama kwake chama kilichompa ubunge mwaka 2015 cha Chadema, hata hivyo Spika Ndugai amedai kuwa haitambui barua hiyo ya Mnyika, kwa vile haijaambatanisha na barua yake mwenyewe Cecil Mwambe ya kukihama chama hicho!
Hivi ushahidi gani anaoutaka Spika Ndugai zaidi ya kadi ya uanachama aiyopewa na Katibu wake Mkuu wa CCM, Dkt Badhiru Ally, hapo tarehe 15/02/2020??
Kama ni hivyo ni kwanini Spika Ndugai hajamrejeshea ubunge wake, Lazaro Nyalandu ambaye pia alikihama chama chake cha CCM na kuhamia Chadema??
Huu utekelezaji wa double standards anaoufanya Spika Ndugai, katika utekelzaji wa shughuli za Bunge, kwa kukipendelea waziwazi chama chake cha CCM, hakika ataiitumbukiza nchi kwenye dimbwi la damu!