Usiginwaji wa Katiba Bungeni: Watetezi wa Haki za Binadamu nchini walaani. Wawakumbushia umuhimu wa kila raia kuilinda Katiba ya Nchi

Usiginwaji wa Katiba Bungeni: Watetezi wa Haki za Binadamu nchini walaani. Wawakumbushia umuhimu wa kila raia kuilinda Katiba ya Nchi

Watanzania wote tunapaswa tuitii na kuiheshimu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977

Katika Katiba hiyo, ibara ya 71(1)(e) inatamka wazi kuwa "Ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge, basi ubunge wake utakoma" mwisho wa kunukuu

Huyu Cecil Mwambe tarehe 15/02/2020 alikihama chama chake cha Chadema na kupokelewa katika ofisi ndogo ya Chama Cha Mapinduzi kwa mbwembwe nyingi na bashasha na Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally na kukabidhiwa kadi ya CCM, mbele ya makamera ya waandishi wa habari

Ule msemo wa ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni ndiyo haya anayoyafanya Spika Ndugai, ambaye ameamua kuisigina sigina Katiba ya nchi yetu na kuamua kuwa ubunge wa Cecil Mwambe haujakoma na anaendelea nao!

Cha ajabu zaidi Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, tayari alishamwandikia barua, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumtaarifu kuhusu kukoma kwa ubunge wa Cecy Mwambe, kutokana na kuhama kwake chama kilichompa ubunge mwaka 2015 cha Chadema, hata hivyo Spika Ndugai amedai kuwa haitambui barua hiyo ya Mnyika, kwa vile haijaambatanisha na barua yake mwenyewe Cecil Mwambe ya kukihama chama hicho!

Hivi ushahidi gani anaoutaka Spika Ndugai zaidi ya kadi ya uanachama aiyopewa na Katibu wake Mkuu wa CCM, Dkt Badhiru Ally, hapo tarehe 15/02/2020??

Kama ni hivyo ni kwanini Spika Ndugai hajamrejeshea ubunge wake, Lazaro Nyalandu ambaye pia alikihama chama chake cha CCM na kuhamia Chadema??

Huu utekelezaji wa double standards anaoufanya Spika Ndugai, katika utekelzaji wa shughuli za Bunge, kwa kukipendelea waziwazi chama chake cha CCM, hakika ataiitumbukiza nchi kwenye dimbwi la damu!
 
Maagizo toka juu unayajua!?
Hayo maagizo toka juu, ambayo hayataki kuitii Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ambayo Jiwe aliapa kuitii na kuiheshimu, ndiyo ambacho ninachokisema kuwa kitasababisha umwagikaji mkubwa wa damu nchini
 
Hata WHO imekataa kutoa msaada wa pesa kwa Tanzania kutokana na kukiuka haki za binadamu na uvunjifu wa katiba, wanajua Tanzania ya sasa haiendeshwi kwa mujibu wa katiba bali inaendeshwa kwa mujibu wa zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM mtukufu mkazi wa chato
 
Ndungai kajitoa fahamu zote kaamua kuwakomoa chadema kasahau kuwa Dunia imebadilika na huo ujinga wake unaenda kuisha pindi CCM wote wakipelekwa mahakama ya uhalifu dhidi ya binadamu The Hague
 
Ndungai siyo spika wa Bunge ni spika wa mtukufu malaika toka chato ni Aina ya spika wa ajabu kupata kutokea Duniani.
minyoo
Ndiyo maana nikasema wananchi watafika mahala watashindwa kuendelea kuvumilia maonevu hayo wanayofanyiwa wapinzani.

Ndipo hapo ninaposema kuwa amani ya nchi hii itatoweka
 
minyoo
Ndiyo maana nikasema wananchi watafika mahala watashindwa kuendelea kuvumilia maonevu hayo wanayofanyiwa wapinzani.............

Ndipo hapo ninaposema kuwa amani ya nchi hii itatoweka
Ndiko wanalazimisha wafike sasa kwa ujinga huo mda si mrefu wananchi watachoka
 
Kwa
We jamaa upeo wako ni mdogo sana. Kwanza unasubiriaga ishu inaongelewa siku kibao unaibuka nayo upya. Pili unawaongelea watanzania wapi?, Alifungwa Lema, Sugu , mwisho Mbowe kwa miezi kadhaa kuna mtanzania ulimuona akiinua pua yake kuwatetea?, Hapa namaanisha Arusha, Mbeya Kisha upinzani kwa ujumla(Mbowe).. Sasa wananchi gani watafika wapi washindwe kuuvumilia?, bado miezi miwili mnatakiwa mtaje mgombea wenu wala hamjui mtamchagua nani?, Nyie ni wa kupuuzwa tu.
Kwahiyo unawachochea ili wakiritaliate useme wahaini?
 
We jamaa upeo wako ni mdogo sana. Kwanza unasubiriaga ishu inaongelewa siku kibao unaibuka nayo upya. Pili unawaongelea watanzania wapi?, Alifungwa Lema, Sugu , mwisho Mbowe kwa miezi kadhaa kuna mtanzania ulimuona akiinua pua yake kuwatetea?, Hapa namaanisha Arusha, Mbeya Kisha upinzani kwa ujumla(Mbowe).. Sasa wananchi gani watafika wapi washindwe kuuvumilia?, bado miezi miwili mnatakiwa mtaje mgombea wenu wala hamjui mtamchagua nani?, Nyie ni wa kupuuzwa tu.
Jerusalem2006
Usitoe povu, bali naomba unijibie swali langu, je ni sahihi alichofanya Spika Ndugai kwa kumuita aliyekuwa Mbunge Cecil Mwambe na kumwambia kuwa anaweza kuendelea na ubunge wake.

Wakati tayari yeye mwenyewe Cecil Mwambe, aliushautangazia Ulimwengu, mbele ya waandishi wa habari kuwa tayari keshajivua uanachama wa Chadema na kujiunga na CCM??
 
Ni kesi muhimu sana, tatizo Je , Tuna Mahakama? Kuna Makahama Kuu yenye ubavu wa kukataa "amri kutoka juu"?
Concern yangu ni hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Tatizo Lenu mna mahaba sana na JPM. Lakini kuwa reserved kabla ya kupiga Kelele Ni muhimu sana. Lazima Kuna mwanya huyo Spika katumia.

Mnajisahau na kudhani wenzenu wajinga kama nyie. Sheria huwa zina mianya Muda utaongea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom