Usiginwaji wa Katiba Bungeni: Watetezi wa Haki za Binadamu nchini walaani. Wawakumbushia umuhimu wa kila raia kuilinda Katiba ya Nchi

Usiginwaji wa Katiba Bungeni: Watetezi wa Haki za Binadamu nchini walaani. Wawakumbushia umuhimu wa kila raia kuilinda Katiba ya Nchi

Tuwe wavumilivu bado wanaandaa hoja zisizopingana baina yao wenyewe
 
Katiba ya Ufipa inabakwa na DJ na hamsemi,,
Kila mtu ashinde mechi zake tukutane fainali
 
Mbona hao Mataga na Praise team wenyewe hawana tofauti na bendera! Wenyewe hufuata tu uelekeo wa upepo. Usije ukashangaa wakija kwa kasi huku wakiunga mkono hicho kitendo. Ndivyo walivyo siku zote! Wapo kama misukule tu.
Wako wanajifukiza (wanapiga nyungu) wakimaliza watajitokeza. Mhimili wa Bunge umedhalilishwa sana awamu hii ya tano.

Hili halina tofauti na Hospitali kuamua kukabidhi Uongozi kwa Mgonja badala ya Daktari. Aibu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
AZIMIO LA KUMSHTAKI SPIKA WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE. JOB NDUGAI KWA KUKIUKA MISINGI YA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BAADA YA KUMRUHUSU BW. CECIL MWAMBE KUENDELEA NA UBUNGE

Ndugu RAIA MWEMA,
Awali ya yote tunakushukuru na kukupongeza kwa kazi kubwa unayoifanya ya kuzuia kuenea kwa maambukizi ya COVID-19 hasa wakati huu ambapo dunia inaendelea kupambana na janga la virusi vya Corona (COVID 19). Sisi kama watetezi wa haki za binadamu tunapenda kukutia moyo uendelee kujilinda wewe pamoja na uwapendao.

Ndugu RAIA MWEMA,
Shirika la Elimu ya Uraia na Msaada wa Sheria (CILAO) limesikitishwa na kitendo cha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufanya maamuzi yanayokiuka misingi ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Itakumbukwa kwamba, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Vyama vya Siasa vinaongozwa kwa mujibu wa Katiba na sheria zingine za nchi. Ibara ya 71 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza wazi kuhusu ukomo wa mtu kuwa Mbunge. Kwa mujibu wa Ibara ya 71(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni wazi kuwa Mbunge atapoteza nafasi yake ya ubunge ikiwa atapoteza uanachama wa chama chake kilichompatia dhamana ya ubunge wakati wa uchaguzi.

Mnamo tarehe 6 Mei 2020, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, aliruhusu, aliyekua mbunge wa Ndanda, Bw. Cecil Mwambe ambaye alishajiuzulu nafasi yake ya ubunge aendelee na kazi hiyo. Hata hivyo, Bw. Cecil Mwambe alishaonekana katika vyombo vya habari akitangaza kujivua uanachama wa CHADEMA na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Kwa kuwa Bw. Mwambe alishatangaza kijiondoa CHADEMA, basi tunaamini pasipo shaka kwamba alipoteza tayari sifa ya kuendelea kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ndugu RAIA MWEMA,
Kitendo cha Spika kumruhusu Bw. Cecil Mwambe kuendelea kuwa Mbunge ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa kuwa Katiba inatamka wazi katika Ibara ya 26(1) kuwa kila RAIA ana wajibu wa kusimamia na kutetea Katiba na Sheria, sisi kama Taasisi tunaomba kushirikiana nawe na wadau wengine kusaini azimio hili la haraka ili kumtaka SPIKA kubatilisha maamuzi yake. Pia tunaomba tushirikiane haraka iwezekanavyo kufungua kesi katika Mahakama Kuu kuomba ufafanuzi wa Mahakama kuhusu kitendo hiki cha Spika.

#PamojaTulindeKatiba

Azimio hili limeandaliwa na: Civic and Legal Aid Organisation (CILAO)



Sent using Jamii Forums mobile app
Anuani ya mawasiliano na makazi tafadhali, yaani Tanzania au visiwa vya Tonga.
 
Chadema kimekuwa chama Cha hovyo sana
Walishindwaje kukaa kikao maalumu ili kuthibitibitisha kujivua kwa Mwambe ..

Yaani ofisi ya Spika iamini kikaratasi Cha Mnyika tu? Hovyo kabisa

Kwa Sasa Chadema wanachoweza ni kutukana,kukejeli na kubeza Serikali yetu tu

Wanajaribu kuanzisha utamaduni wa hovyo kabisa Kama ukoo wa Sultani wao
 
Haya mambo mwalimu NYERERE, aliyaona sana, ndio maana akasema binadamu anaweza akajifanya MUNGU mtu, na ndio kinachotokea na hiyo ni spika tu chanzo ni radio ipo sehemu nyingine kijijini imetulia, mambo yanaendeshwa kama mpira wa makaratasi?
Yaani imebidi nicheke msibani eti " ... hiyo ni spika tu chanzo ni redio ..."

Kwakweli subwoofer safari hii kaboronga sana kama masihara vile kaweka historia mpya katika bunge kwa vizazi na vizazi vijavyo ...

Bado nazidi kuthibitisha kwa Nini CCM inanunua vijana wa upinzani ilikuokoa nafasi za uongozi kwa sababu walioko huko ni Mandunga Embe matupu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa hichi kitendo angekua nchi nyingine yoyote watu wangekua washaandamana spika aachie kiti, ila kwa kua ni Tanzania watu wanamezea tu, hili li nchi upumbavu wa watu ushanishinda, sirudi bongo kwa style hii, kuishi na washenzi namna hii inakera sana, tutaendelea kua masikini tu. Na jiwe yuko ovyo ila mshukuru sana akija mbovu zaidi ya jiwe bado atawapelekesha zaidi ya hivi na watanzania watamshangilia. Pumbavu kabisa
 
Iko siku tutachoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Tanzania sahau hili halitokuja kutokea, kuna watu hata hili wanamuunga mkono 100%. Nchi ambayo majority ni vilaza labda itokee kitu kiue 50% ya vilaza wote kitu ambacho ni impossible. Power play itazidi kua hivi Tanzania miaka na miaka. Ukichoka haisaidii huku majority ya nchi nzima wanaunga mkono
 
mnalaumu Spika bure tu....

fuatilia uone Nani kashika microphone
Lazima alaumiwe sababu amekaa anasikiliza mambo anajua si ya haki ila anafata tu, yeye si mtu mzima ana elimu anaweza kataa? Kama kiongozi wa muhimili unaojitegemea kukubali kuendeshwa na mtu mwingine lazima tumlaumu, kashikwa map****bu tu anatekenywa anacheka, jinga kabisa
 
Vipi kuhusu Mheshimiwa Selasini Mbunge wa Rombo aliyetangaza hadharani kujivua uwanachama wa Chadema na kuhamia NCCR-Mageuzi na bado anaendelea na ubunge?.

Yaani Chadema inatangaza kwamba Wabunge wake waliohamia NCCR Mageuzi wataendelea na Ubunge lakini aliyehamia CCM avuliwe, hii ni akili?

Nakumbuka vizuri kwamba, Spika alihitaji Muhtasari wa Kikao cha chama cha CHADEMA kuhusu kumuondolea Mwambe Ubunge. Lakini Chadema waliwasilisha barua pekee pasipo viambatanisho.

Civil Society msitumike kama mawakala wa Mabeberu na Vyama vya upinzani, teteeni Haki za Kiraia zenye tija kwa wananchi na Taifa.

Lengo lenu ni kuikomoa CCM, Kumkomoa mbunge au Wananchi wa Rombo wasipate mwakilishi katika bunge la bajeti?.
Ikumbukwe kwamba, Mheshimiwa Zitto, wakati amezuliwa uwanacha na Chadema, bado aliendelea na ubunge, Mbona hamkuazimia kumshtaki spika wala mahakama?.

Mbunge ni mwakilishi wa wananchi sio chama, hivyo tulieni

Ni kweli mbunge ni mwakilishi wa wananchi sio chama, Nami naamini kabisa ni vema katiba ingerekebishwa hapo kwamba mbunge ataendelea kuwa mbunge licha ya kuvuliwa uanachama mpaka atakapo maliza muhula wake lakini kwa sasa pasipo shaka katiba imekiukwa na ni lazima tuifate katiba, tukiamua juu juu kama unavofikiria wewe ni dalili mbaya kwa nchi inayoongozwa kwa katiba. Ni lazima tufate katiba
 
Tunamwomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali ajitokeze hadharani atafafanulie inakuwa Lazaro Nyalandu wa Ccm aliweza kupoteza Ubunge wake mara tu alipojiunga na Chadema na inakuwaje Cecil Mwambe wa Chadema aendelee kuwa Mbunge licha ya kujiunga na CCM.Njia aliyoitumia Mh.

Nyalandu ya kujiuzulu uanachama wake CCM na kujiunga Chadema kwa maana ya kuita Waandishi wa habari na ndio hiyo hiyo aliyoitumia Mh.Mwambe.Najiuliza Mwambe ni Mbunge wa Chama gani kati ya Chadema na CCM? Kama ni Chadema alikwisha jivua uanachama,kama ni CCM uchaguzi ulifanyika lini? Mwanasheria Mkuu wa Serikali hebu tusaidie tusiojua sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG_20200507_214326.jpg
 
Nyalandu bado Mbunge wa CCM mkuu, yeye mwenyewe hataki tu kwenda Bungeni. Bunge letu safi chini ya uongozi makini wa bwana Ndugai, hata kama umestaafu wewe bado Mbunge tu labda ukifa ndio ukomo unafikia..
 
Back
Top Bottom