Usiichukulie poa Tanzania katika medani za kivita, walioijaribu walifutika

..tunaweza kushinda.

..kwani tulipowadunda m23 na Rwanda waziri wa ulinzi si alikuwa Husseni?

..Na Husseni alikwepa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria?

..ushanfahamu?
Mkuu enzi zile za kina Idd Amin tulipiga gorilla war,sasa hivi wenzetu kama Rwanda wana silaha,wanaupdate silaha zao, hivi tuna silaha kweli za maana na kujiamini kwamba tupo vizuri ? Leo hii sidhani kama tunaweza kutoka mipaka yetu tukaenda kumfuata adui kwake na kumpiga.

Swali langu je silaha zipo? Jeshi letu limeficha silaha tusizione? Maana tukiaanza kugoogle takwimu hapa ambazo zipo wazi tutakuwa nyuma ya wenzetu.
 
Ngoja kagame awachakaze huko goma mpk wasemeee!!!
 

..matumizi ya silaha mara nyingi ni uharibifu.

..uharibifu wa maisha, uhai, au mali.

..badala ya kushindana nchi gani ina silaha kumzidi mwenzake, tushindane nchi gani ina vifaa vya kilimo kumzidi mwenzake.

..badala ya kushindana nchi gani ina wanajeshi / wauwaji wakatili zaidi, tushindane nchi gani ina wakulima wenye maarifa kuzidi nyingine.

..kwa kifupi tushindane kwenye mambo yanayoboresha maisha ya raia ktk nchi zetu.
 
Inaonekana inanguvu kwasabab imekubali kuwalamba mabwenyenye!As long as Tz bado imekumbatia mikataba ya kikoloni kwa maliasili zake,imekubali kucheza tune ya mataifa ya magharibi kiasi kwamba haiwez hata kushirikiana kwa uwazi na mataifa hasimu ya magharibi(Urusi/Iran/Cuba/Venezuela/Nicaragua nk) basi tunaachwa tulivu na kwahyo tunaonekana tunaamani na tupo imara kijeshi lakini kwa ground sisi ni chui wa karatasi!
You want to prove me wrong ask Tshisekedi of Congo,amejifanya anataka kujielekeza Urusi mataifa ya magharibi yamemtumia Kagame kumsambaratisha.No one will stop Kagame unless his masters(the west) waliomtuma wamzuie,literally no one hata ninyi mkienda mtapigwa
 
Mkuu simulizi siku zote hutiwa chumvi.

Wanajeshi wetu ni mahiri kwa kumwaga vyakula vya mama ntilie na kuzima maandamano ya chadema tu.

Lkn kwenye vita serious hakuna kitu, kila mwaka wanachezea kichapo kwa M23.
Ni wapi JWZT walimwaga chakula na kuzima maandamano ya Chadema?
 
Ni wapi JWZT walimwaga chakula na kuzima maandamano ya Chadema?
Umesahau walipewa kazi ya kufagia mitaa siku ambayo chadema wamepanga maandamano?

Ushawahi kusikia jeshi la Marekani linafanyishwa kazi za kijinga namna hii?

Na kuna mwaka JWTZ waligeuzwa kuwa makuli wa kukusanya korosho. 😂 😂
 
Umesahau walipewa kazi ya kufagia mitaa siku ambayo chadema wamepanga maandamano?

Ushawahi kusikia jeshi la Marekani linafanyishwa kazi za kijinga namna hii?

Na kuna mwaka JWTZ waligeuzwa kuwa makuli wa kukusanya korosho. 😂 😂
Ni jambo baya Jeshi kuwa sehemu ya chama cha siasa au kupelekeshwa na wanasiasa wabadhilifu wenye uchu wa madaraka na kusahau mipaka na wajibu wao kwa raia
 
Sasa hivi ikitokea Tanzania tukavamiwa,mimi nitaungana na maadui kuwaonyesha viongozi wa serikali na ccm walipo.
 
Sasa hivi ikitokea Tanzania tukavamiwa,mimi nitaungana na maadui kuwaonyesha viongozi wa serikali na ccm walipo.
Nyie ndiyo mlikuwa mnapinga ujenzi wa SGR
 
Nadhani ni Tanzania pekee kwa ukanda wetu ndio ina mfumo wa kuwapeleka wahitimu jeshini, na kuwa na mfumo wa kujiunga jeshi kwa lengo la kujitolea... So kimantiki.. Tanzania ina wanajeshi wengi sana... Ukiachana na hao ambao wapo kambini
 
Mnapenda kuongelea historia jeshi lenu haliko hivyo tena ndo maana mr slim na ontelijensia yale wana jeuri na hamna cha kiwafanya
Jeshi letu ni dhaifu sana
 
Naamini silaha tunazo, na si lazima kuzionyesha onyesha, mfano pale mashariki ya kati, sidhani kama Israel ana tabia ya kuonyesha onyesha silaha zake ukizingatia kwamba ni mkorofi na amezungukwa na maadui, tena adui si wa mbali
 
Mnapenda kuongelea historia jeshi lenu haliko hivyo tena ndo maana mr slim na ontelijensia yale wana jeuri na hamna cha kiwafanya
Jeshi letu ni dhaifu sana
Walilijaribu juzi tu wale wa kibiti
 
hukuiona hii...

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…