Usijaribu kufanya biashara za ahadi na wabongo utaumia (Promissory Notes)

hahahhaaa Daah amu njoo

Niliua biashara ya Madera sababu ya huu upuuzi,

nilichojifunza kwa biashara bora kuwekesha ,yaani Mtu aweke pesa mzigo nibakie nayo mwenyewe.

halafu kuna wanaojifanya wajanja wa mjini anakuambia niletee mzigo pesa ninayo mkononi ukifika ana hela nusu,
usiwe mnyonge MPE mzigo kulingana na pesa yake...
 
Ukifanya hizo mishe na mbongo kuambiwa bibi kadedi niskilizie tupitishe kwanza arobaini mbona kawaida sana mkuu.
 
Kama hutaki kumpoteza mtu usimkopeshe, watu wakishapata huduma u kitu wanachokitaka wanasahau kulipa deni.. hadi uchukue action ndo anakulipa
 
Yani jau sana mwanangu mwenyewe...Sema nn nimejifunza kitu mkuu! Sahivi mikazo ntakayowapa walimwengu Nduli Iddi Amini akasome. Wacha niitwe roho mbaya kmmmk maana roho za kikristo zinaturudisha nyuma sana wabongo.

Ku deal na wapuuzi ni ushwaini!
Sisi waswahili hatuna uungwana kabisa. Kumbuka nilipe nisepe wa Belle9 jaribu kusikiliza ukufariji mzee.

Weka mikakati na kanuni ya namna unataka kuendesha biashara yako. Hakikisha hata wewe mwenyewe huzivunji. Mambo yatakuwa shwari baadae. Ila ogopa sana biashara ya mali kauli hasa kipindi hiki cha COVID-19.
 
Hawawezi kunisaidia kuharakisha malipo maana naona usumbufu umekuwa mkubwa na hasa muda wangu ndio mali.
Watoe pesa ya usumbufu halafu waambie wakusaidie kuwapa presha hawa wahusika ili walipe ama mali zao zitashikiliwa kufidia hayo madeni
 
Hapana. Haina haja ni jamaa tu kupigwa presha na kesi unaiweka katika sura ya utapeli ambayo itakuwa jinai
 
Hapana. Haina haja ni jamaa tu kupigwa presha na kesi unaiweka katika sura ya utapeli ambayo itakuwa jinai

Ni rahisi kuifungua kesi kwa jalada hilo ila mbaya itakuja pale wanapomchukua maelezo unae mdai. Akijieleza vizuri mbona anachomoka tu. Ngoma inarudi kwenye madai. Na kama ni mtu anaejiamini na anajielewa ndio hapo anapoleta kukulipa deni kwa kuligusa kidogo kidogo kwa kukukomoa.
 
Kweli mkuu, nmejifunza aisee bora kubaki na mali yako kuliko kumuuzia mtu kwa advance ambaye atasumbua kumalizia malipo.
 
Sio biashara tu, kukopeshana pia ndio mwanzo wa ndugu kugombana na urafiki kufa[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
Ni kweli, mie naona miyeyusho sana maana kulipa ni mpaka mgombane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…