Usijaribu kufanya biashara za ahadi na wabongo utaumia (Promissory Notes)

Usijaribu kufanya biashara za ahadi na wabongo utaumia (Promissory Notes)

hahahhaaa Daah amu njoo

Niliua biashara ya Madera sababu ya huu upuuzi,

nilichojifunza kwa biashara bora kuwekesha ,yaani Mtu aweke pesa mzigo nibakie nayo mwenyewe.

halafu kuna wanaojifanya wajanja wa mjini anakuambia niletee mzigo pesa ninayo mkononi ukifika ana hela nusu,
usiwe mnyonge MPE mzigo kulingana na pesa yake...
 
Biashara za ahadi ya malipo ya tarehe fulani (Promissory Notes). Kwa wabongo ni sumu usijaribu huwa hawajali muda!

Hii kitu imenisababishia headaches mpaka sasa nimekwama. Kuna watu nimewauzia mali wakalipia Advance ila kumalizia mikia ndio imekuwa shughuli.

Tunasumbuana mpaka nafikiria nikafungue kesi polisi. Wanakera kinoma yani. Mmoja biashara ya 19/5 akaahidi kumalizia 2/6 ila hajafanya hivyo mpaka sasa ni story nyingi tu mara msiba, mara vile mwisho ananiambia nimepambana nimeshindwa labda mpaka mwisho wa mwezi. Ina maana nipoteze mwezi wote wa 6 bure tu!

Mwengine nae wa Tarehe 9/4 akaahidi by tarehe 30/4 anamaliza. Imefika siku ya kulipa hela hana, akanipiga sound mpaka 15/5 hela yenyewe akatoa nusu. Tumesumbuana tarehe 23/5 akatoa tena nusu ya iliobaki. Toka na hapo hela hajamalizia tena kila nikimcheki anapambana mambo magumu.

Yani usumbufu ninaoupata ndio naelewa umuhimu wa biashara za cash in hand. Mnafunguana mashati mapema tu kila mtu anasonga na njaro zake.
Ukifanya hizo mishe na mbongo kuambiwa bibi kadedi niskilizie tupitishe kwanza arobaini mbona kawaida sana mkuu.
 
Kama hutaki kumpoteza mtu usimkopeshe, watu wakishapata huduma u kitu wanachokitaka wanasahau kulipa deni.. hadi uchukue action ndo anakulipa
 
Yani jau sana mwanangu mwenyewe...Sema nn nimejifunza kitu mkuu! Sahivi mikazo ntakayowapa walimwengu Nduli Iddi Amini akasome. Wacha niitwe roho mbaya kmmmk maana roho za kikristo zinaturudisha nyuma sana wabongo.

Ku deal na wapuuzi ni ushwaini!
Sisi waswahili hatuna uungwana kabisa. Kumbuka nilipe nisepe wa Belle9 jaribu kusikiliza ukufariji mzee.

Weka mikakati na kanuni ya namna unataka kuendesha biashara yako. Hakikisha hata wewe mwenyewe huzivunji. Mambo yatakuwa shwari baadae. Ila ogopa sana biashara ya mali kauli hasa kipindi hiki cha COVID-19.
 
Hawawezi kunisaidia kuharakisha malipo maana naona usumbufu umekuwa mkubwa na hasa muda wangu ndio mali.
Watoe pesa ya usumbufu halafu waambie wakusaidie kuwapa presha hawa wahusika ili walipe ama mali zao zitashikiliwa kufidia hayo madeni
 
Unae mdai atasema ana uwezo wa kukulipa elfu 5 kila mwezi kutokana na hali mbaya ya uchumi. Hivyo atakuwa anapunguza hiyo buku 5 hadi deni liishe.

Hapo unakuta unadai laki 5! Mna andikihsna kituoni na kila mtu anaenda na njia zake. Ndio taratibu za kesi za madai zinavyokuwa polisi.
Hapana. Haina haja ni jamaa tu kupigwa presha na kesi unaiweka katika sura ya utapeli ambayo itakuwa jinai
 
Hapana. Haina haja ni jamaa tu kupigwa presha na kesi unaiweka katika sura ya utapeli ambayo itakuwa jinai

Ni rahisi kuifungua kesi kwa jalada hilo ila mbaya itakuja pale wanapomchukua maelezo unae mdai. Akijieleza vizuri mbona anachomoka tu. Ngoma inarudi kwenye madai. Na kama ni mtu anaejiamini na anajielewa ndio hapo anapoleta kukulipa deni kwa kuligusa kidogo kidogo kwa kukukomoa.
 
Sisi waswahili hatuna uungwana kabisa. Kumbuka nilipe nisepe wa Belle9 jaribu kusikiliza ukufariji mzee.

Weka mikakati na kanuni ya namna unataka kuendesha biashara yako. Hakikisha hata wewe mwenyewe huzivunji. Mambo yatakuwa shwari baadae. Ila ogopa sana biashara ya mali kauli hasa kipindi hiki cha COVID-19.
Kweli mkuu, nmejifunza aisee bora kubaki na mali yako kuliko kumuuzia mtu kwa advance ambaye atasumbua kumalizia malipo.
 
Sio biashara tu, kukopeshana pia ndio mwanzo wa ndugu kugombana na urafiki kufa[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
Ni kweli, mie naona miyeyusho sana maana kulipa ni mpaka mgombane.
 
Back
Top Bottom