Usijaribu kununua haya magari mawili utalia kilio cha mbwa mdomo juu

Usijaribu kununua haya magari mawili utalia kilio cha mbwa mdomo juu

Chukua Chuma Hicho Uepuke Karaha Na Fedheha
MManual
4WD
Mafuta Inanusa

Haipitwi Na Fashion
Utulivu Barabarani, Inabeba Watu Vibonge
Popote Tanzania Unakwenda
Ukianzia Mtwara Mpaka Misenyi Kagera Bila Kuzima Zaidi Unaweka Fuel Tu
images.jpeg.jpg
 
Nimekuja mkoa flani kikazi nilitumia usafiri wa ndege. Huku kuna jamaa yangu akaniambia kwa kuwa akija Dar huwa nampatia usafiri nitumie gari ndogo ambayo huwa anatumia mkewe. Niende kwake nikachukue. Nikaenda.

Nimefika nikakaribishwa ndani n.k nikamwambia shemeji nimeambiwa nije chukua gari. Akasema Yes anazo taarifa. Akanipa funguo nichukue gari nje. But kutoka nje sioni gari. Naona Passo tu imepark. Nikarudi kuuliza gari ipo wapi. Akaniambia hiyo hapo Passo. Daaah... Nikashtuka nikawaza basi ni mtie moyo shemeji yangu nikachukua nikaenda zangu Hotel. Nlipark

Passo vigari vina kisirani sana unaweza ukakaa hivi kakajiwasha. Unasikia tu kanyenyeee nyeeee kanyeeee nyeeeeeeeee vrruuuuum..... Halafu kanaendelea kunguruma. Basi unaenda una kazima. Ukiwa unarudi kukaa kanajiwasha tena. Yaani ili mradi kakukere tu.

Wakati mwingine upo barabarani kanasusa kanazima. For no apparent reason. Ukikawasha kanatetemeka kama kana degedege. Yaani ni shida tu kwa kweli.

Nikakumbuka Dualis hizi gari tunaziita Mnyalu. Zina hasira kinoma. Yaani kama wahehe tu. Unaweza ukapark nje ukakuta kamejitia moto. Unashangaa why? Basi tu ndo imeshaamua ife. Yaani kwa watu wengi sasa hivi Dualis wanazipark kwenye swimming pool au ndani ya bwawa la maji.

Maana watu wanakwambia at any tea time inaweza jitia kiberiti ikawaka moto ina hasira kama wahehe. Sasa watu wakipark wanahakikisha ni karibu na maji au wanaenda park pale kariakoo fire. Usije ukanunua hayo magari ni kichefu chefu sana.
moderators pelekeni huu uzi jukwaa la vichekesho. Topic kama hizi ndio zinatufanya watanzania tuonekane wajinga.
 
kama ilikupeleka unakotaka inapendeza..... haya mengine vihoja tu
 
.......mi nafikiri Jamaa alikuwa ana ujumbe na tahadhari nzuri tu kwa wadau kuhusu hizi gari mbili, sidhani kama kuna ubaya Kwa namna alivyowadilisha hoja yake kwa staili ya kuchekesha kidogo.......
.......tusiwe too emotional naona watu wanamuattack vibaya ila sijaona shida kubwa kwenye huu Uzi kama utazingatia ujumbe, hizo gari mbona zimeshalalamikiwa sana, tupunguze stress wakuu, akikasirika akatukana hapa tutaanza kulaumu tena.......
 
sie wa daladala tunaona gari ni gari tu
 
We jamaa naona uchizi unaelekea kukomaa kabisa. Soon utashindikana kutibiwa kabisa,na utaanza kuingia barababrani kunusa makopo ya mikojo na kupuliza kondom za kuokota.

Huu uzi wa pili ndani ya siku nne unaandika pumba.
Mbona hasira mkuu
 
.......mi nafikiri Jamaa alikuwa ana ujumbe na tahadhari nzuri tu kwa wadau kuhusu hizi gari mbili, sidhani kama kuna ubaya Kwa namna alivyowadilisha hoja yake kwa staili ya kuchekesha kidogo.......
.......tusiwe too emotional naona watu wanamuattack vibaya ila sijaona shida kubwa kwenye huu Uzi kama utazingatia ujumbe, hizo gari mbona zimeshalalamikiwa sana, tupunguze stress wakuu, akikasirika akatukana hapa tutaanza kulaumu tena.......
Watu wana makasiriko. Yaani kushindwa kwao kwa maisha wanataka hamishia kwa wengine. Na wengi wenye passo naona wameumia sana. But they should just relax mtu hujikuna anapofikia.
 
Kuna jamaa yangu ana Passo aliinunua simce 2013 au 2014 hivi...
Mpaka hivi leo bado anayo au ushakaa juu ya mawe kitambo? Maana hizi gari watu wanalalamika ni majanga ,,lakin ninachoamini hakuna gari mbaya ila kuna matumizi mabaya ..ivo hata Passo ukitumia vizur kutokana na uwezo wake basi utadumu nayo
 
Back
Top Bottom