Usije kujaribu kumuomba msamaha mwanamke hata kama umekosea!

Mshangazi dot com

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
1,345
Reaction score
3,503
Eti ni udhaifu 🤷🏾

Hivi ni kweli wanaume mnafikiri kwa namna hii au ni baadhi tu ya vijana wasiojielewa?

Kama humuombi mkeo au mpenzi wako msamaha ukikosea, huwa unamalizaje migogoro kwenye mahusiano yako?

Mwisho kabisa, Je, ni sahihi kwa huyo mwenza wako pia kutukukuomba msamaha akikosea, au hiyo ni kwa ajili ya wanaume tu?

giphy-downsized.gif

IMG_2040.jpeg

🤷🏽‍♀️

IMG_2051.jpeg

Mzee wangu Ushimen , njoo nawe utugawie uzoefu wako kidogo.

Cc:
Nomadix , Poor Brain , realMamy , Monetary doctor , Intelligent businessman , mzabzab , Extrovert , Wagumu Tunadumu , Mwachiluwi , Kadhi Mkuu 1
 
Mwisho kabisa, Je, ni sahihi kwa huyo mwenza wako pia kutukukuomba msamaha akikosea, au hiyo ni kwa ajili ya wanaume tu?
Huo ni udhaifu, Mwanaume kuomba Msamaha mkeo ni sawa na kujivua madaraka maana mwanamke hua hasahau ila anahifadhi kwa matumizi ya baadae kwa hio mbwaimbwai tu km vipi mwaga mboga nimwage ugali kwanini Unga shingap na Tembele shingap?
 
Ukimuomba mwanamke msamaha unakua umekabidhi power yako yote kwake!!!

Siku nyingine ukikosea atakukumbushia na hata yeye ikitokea amezingua atakua anakwambia kumbuka mimi ulinikosea nikakusamehe kidume ukiambiwa hivyo una calm down.

Wakati mwingine anaweza kukunyima unyumba kabisaa eti kisa amekumbuka ulimkoseaga( emotional being )
 
Daah Bueno 😅 basi sawa
 
Sijui kama nimeelewa swali 😂! Ila ninacho amini .. this is my personal philosophy "Mtu dhaifu ni mtu asiyeweza kuomba msamaha pale ambapo amekosea"

Pengine labda kama huyo mwanamke humpendi na huna Malengo nae, unataka tu kupiga na kusepa!

Ila kuwa mwanaume Haina maana unapomkosea mwenzi wako, hupaswi kuomba msamaha si kweli!

Kuna kisa fulani nimekikumbuka, sikumbuki vizuri Nini kilitokea baina ya Mimi na rafiki zangu watatu ila kuliibuka ugomvi mkubwa sana.

Na nilisingiziwa kuwa ndio chanzo Cha huo ugomvi. Nakumbuka Ile siku nilipopata hizo taarifa nilienda madhabahuni pale Kijitonyama nikasali sana, Mimi ni yule mwenye hasira za karibu!

Ndani yangu, Nina amini ni Roho Mtakatifu alinisemesha ... Kuwa hiyo siku ya hicho kikao nikifika nisijitete na kujionyesha kuwa Mimi sio mkosaji! Bali nikubali na kuwaambiwa wote naomba mnisamehe Mimi ndiye niliyewakosea!

Nadhani Mungu alikuwa ana deal na Roho ya kiburi ndani yangu! Haikuwa rahisi

Siku ilipofikia wotee wakaongea! Ilipofika zamu yangu, huku natetemeka kwa hasira! Niliwaomba msamaha ... Gafla kukawa na ukimya! Afu nikasepa zangu!

Kesho yake wote walikuja kukubali kuwa wao ndio waliokosea na wanaomba msamaha maana Roho zao zinawasuta!

Sasa turudi kwenye mada yako!

Mahusiano yangu ya mwisho, mbali na ukiburi niliokuwa nao na hulka ya kimasai

Kila mara magomvi yalipokuwa yakitokea nilikuwa wa kwanza kujishusha na kuomba msamaha (Kuna kitu kulikuwa kinani push kufanya ivo)

Siku moja, huyo dada akaniambia "yaani wewe ni ajabu sana, ni mwepesi kuomba msamaha na kuyafanya mambo yaishe ili tu amani ipatikane kati yetu, sijui kwa namna hii tunavyoishi ikitokea siku tukaachana, kama nitaweza kuja kuishi na mwanaume mwingine asiye na moyo kama wako"

Binafsi ni mtu ambaye sipendi magomvi kabisa na sipendi Mimi kuwa sababu ya maumivu kwa mtu mwingine Hilo limenijenga kuwa mwepesi wa kuomba msamaha na kujishusha kwa haraka sana kwa mtu yoyote!

Nina amini, hakuna faida kwenye ugomvi.

Ndo maisha yanaenda 😂
 
Apart from mama
Siwezi kumuomba msamaha mwanamke kwa kutamka "samahani"

Nitamuomba msamaha kwa vitendo au kibishi, "kausha basi we hujawahi kukosea".

Kumuomba mwanamke msamaha kwa maneno ya kipole ni kumpa full authority na power ya kujua anaweza kukucontrol akitaka na huwezi bila yeye

ZINGATIA: Siwezi kuomba msamaha kwa maneno napendelea vitendo zaidi.
 
Ukimuomba mwanamke msamaha unakua umekabidhi power yako yote kwake!!!

Siku nyingine ukikosea atakukumbushia na hata yeye ikitokea amezingua atakua anakwambia kumbuka mimi ulinikosea nikakusamehe kidume ukiambiwa hivyo una calm down.

Wakati mwingine anaweza kukunyima unyumba kabisaa eti kisa amekumbuka ulimkoseaga( emotional being )
Nimekusoma

Je na yeye akikukosea ni hivyo hivyo, asikuombe msamaha au ni wewe tu ndo una haki ya kutumia hicho kigezo?
 
Sijui kama nimeelewa swali 😂! Ila ninacho amini .. this is my personal philosophy "Mtu dhaifu ni mtu asiyeweza kuomba msamaha pale ambapo amekosea"

Pengine labda kama huyo mwanamke humpendi na huna Malengo nae, unataka tu kupiga na kusepa!

Ila kuwa mwanaume Haina maana unapomkosea mwenzi wako, hupaswi kuomba msamaha si kweli!

Kuna kisa fulani nimekikumbuka, sikumbuki vizuri Nini kilitokea baina ya Mimi na rafiki zangu watatu ila kuliibuka ugomvi mkubwa sana.

Na nilisingiziwa kuwa ndio chanzo Cha huo ugomvi. Nakumbuka Ile siku nilipopata hizo taarifa nilienda madhabahuni pale Kijitonyama nikasali sana, Mimi ni yule mwenye hasira za karibu!

Ndani yangu, Nina amini ni Roho Mtakatifu alinisemesha ... Kuwa hiyo siku ya hicho kikao nikifika nisijitete na kujionyesha kuwa Mimi sio mkosaji! Bali nikubali na kuwaambiwa wote naomba mnisamehe Mimi ndiye niliyewakosea!

Nadhani Mungu alikuwa ana deal na Roho ya kiburi ndani yangu! Haikuwa rahisi

Siku ilipofikia wotee wakaongea! Ilipofika zamu yangu, huku natetemeka kwa hasira! Niliwaomba msamaha ... Gafla kukawa na ukimya! Afu nikasepa zangu!

Kesho yake wote walikuja kukubali kuwa wao ndio waliokosea na wanaomba msamaha maana Roho zao zinawasuta!

Sasa turudi kwenye mada yako!

Mahusiano yangu ya mwisho, mbali na ukiburi niliokuwa nao na hulka ya kimasai

Kila mara magomvi yalipokuwa yakitokea nilikuwa wa kwanza kujishusha na kuomba msamaha (Kuna kitu kulikuwa kinani push kufanya ivo)

Siku moja, huyo dada akaniambia "yaani wewe ni ajabu sana, ni mwepesi kuomba msamaha na kuyafanya mambo yaishe ili tu amani ipatikane kati yetu, sijui kwa namna hii tunavyoishi ikitokea siku tukaachana, kama nitaweza kuja kuishi na mwanaume mwingine asiye na moyo kama wako"

Binafsi ni mtu ambaye sipendi magomvi kabisa na sipendi Mimi kuwa sababu ya maumivu kwa mtu mwingine Hilo limenijenga kuwa mwepesi wa kuomba msamaha na kujishusha kwa haraka sana kwa mtu yoyote!

Nina amini, hakuna faida kwenye ugomvi.

Ndo maisha yanaenda 😂
Ok brother
 
Back
Top Bottom