You are one in a million, mmebakia wachache sana wenye roho kama yako. Ni jambo jema!
Ngoja nimalizie na kisa hiki! Ni changu Mimi.
Baada ya break up kutokea na yule dada! Ile miezi ya kwanza kwanza nilikuwa kwenye frustration kubwa sana sana!
Kwanza jambo Hilo limetokea kipindi namalizia kuandika Kitabu Cha Uamsho na mifumo .... Sasa Si unajua kazi yangu 🤣
Kuna mdada akanitafuta ... She was my client ambaye tulikutana kwenye counseling na tulifika kwenye hatua ya termination na akavuka kwenye tatizo lake!
This time anarudi akiwa na shida ingine, na Mimi ndo nipo kwenye frustration mode! 😂
Katika Ile Hali ya kupeana moyo na gafla tukaingia kwenye mahusiano ... Kumbuka Mimi sijawa healed
Ngoja niandike afu nitafuta hii comments 😂
Basi bhana! Akaniomba sana nimetembee mkoa alipo!
Nilikuwa kwenye kazi fulani Moshi 😂 ... Sikumaliza nikatoroka nikaanza safari ya kuitafuta Tarime!
Nikipanda basi ya mwanza, nikachelewa kufika mwanza ... Mida ya saa moja Nikakuta gari za Tarime zimeondoka!
Nikahangaika kupata usafiri wa fuso linaenda Bunda saa sita usiku! Nikafika saa 8 Bunda nikapata fuso la kwenda Tarime
Nimefika saa kumi na mbili asubuhi 😂 ... Chap nikafika kwake akafurahi kuniona!
Kwa sababu ya frustration niliyokuwa napitia basi muda mwingi nilikuwa nipo njwiii! Nimelewa ila vigumu kujua Hilo.
Basi yakafanyika ya kufanyika 😂 .. I stayed kama siku 3 ... Siku zote hizo Mimi na wine!
Asubuhi Moja akiwa kazini, akanitumia text kuwa ameota ndoto, Mimi namwambia kuwa siwezi kuendelea na hii relationship kwa sababu Bado Nina hisia na ex Wangu
Nilishangaa sana maana ilikuwa ni kweli, Mimi niliingia kwenye relationship na yeye kwa sababu ya upweke tu!
So nikazidi kuvurugwa! Maana nikaona naenda kuumiza moyo wa huyu mtu ... KITU NINACHOKUCHUKIA MAISHA YANGU YOTEEE!
kesho nikaaga kuondoka! Nilivyofika dar!
Nikamweleza ukweli na kumuomba msamaha ... Toka siku hiyo update
Wino umeisha 😂