Usijidanganye kuwa ukioa mwanamke atakuja na baraka ya kipato chako kuongezeka

Usijidanganye kuwa ukioa mwanamke atakuja na baraka ya kipato chako kuongezeka

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Kuna hii imani ya kishirikina kuwa hata kama huna hela UOE kwa sababu mwanamke huja na baraka ya kipato. Ni upuuzi mtupu. Hakuna kitu kama hicho. Usiishi kwa kutegemea miujiza. Jiambie ukweli kuwa unapooa gharama za maisha zitaongezeka kwasababu ya jukumu jipya la kuhudumia mke na baadae watoto.

Unajua gharama za matibabu hospitalini? Hizo ni hatari kuliko gharama zingine zote nyumbani ikiwemo kulipa ada za shule. Sasa ukioa hizo utakutana nazo. Mimi ninashauri watu waoe wakiwa angalau na mwelekeo wa kuwa sawa kiuchumi.
 
Inategemea unaoa mke ambaye ana hali Gani ya KIPATO.mfano uoe mtoto wa kizimkazi au mtoto wa mfanyabiashara mkubwa lazima utapata baraka ya maendeleo Kwa kasi ya 5G.

Sasa wewe ni MASIKINI na unaoa Kwa MASIKINI utegemee baraka upate haraka?
 
Kama hujaoa kwa nia sahihi huwezi kuliona hilo, ila take it from me baraka ipo kubwa sana.

Pia huondoa mawazo mengi ya kipuuzi ambayo kijana ambaye hajaoa anakuwa nayo, ukioa kichwa kinakuwa focused kuliko kawaida.

La muhimu kuoa kwa nia sahihi
 
Unamchukua mwanamke nyumbani kwao unamleta kwako muishi pamoja unatumia gharama kubwa kumuhudumia kwa kila namna halafu anageuka kuwa pasua kichwa.

Mara achepuke akuletee magonjwa au watoto wasio damu yako.Kuna wanawake wengine ni hovyo kabisa, hata kile kipato kidogo cha familia anadokoa kuhonga vibenten.

Hata ukiwa na hela kuishi na mwanamke kunachangia kupunguza maisha ya mwanaume.
 
Inategemea unaoa mke ambaye anahali Gani ya KIPATO.mfano uoe mtoto wa kizimkazi au mtoto wa mfanyabiashara mkubwa lazima utapata baraka ya maendeleo Kwa kasi ya 5G.Sasa wewe ni MASIKINI na unaoa Kwa MASIKINI utegemee baraka upate haraka?
Kweli kaka kuwapata watt wa kishua ndokazi.
 
Ukipata Mwanamke anayekupenda na mnapendana.
Oa hata kama Hauna kazi. OA.

Mkipendana ndoa na familia yenu lazima iende tuu na lazima mpige hatua.

Lakini kama hujampata anayekupenda, na huna unayempenda hata uwe kama Elon Musk usijejiingiza kwenye ndoa au kuanzisha familia

Ndoa inahitaji
I) watu wanaopendana.
ii) Watu wanaosikilizana na kuelewana.
iii) Watu walioamua kuishi na kufanya Maisha pamoja.
Pesa na Mali huja baadaye sana.

Kwa hili binafsi ninaushahidi.
 
Kama hujaoa kwa nia sahihi huwezi kuliona hilo, ila take it from me baraka ipo kubwa sana.

Pia huondoa mawazo mengi ya kipuuzi ambayo kijana ambaye hajaoa anakuwa nayo, ukioa kichwa kinakuwa focused kuliko kawaida.

La muhimu kuoa kwa nia sahihi
Who are you?
 
Acha kudanganya watu baraka zinakuja kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nizamu ya pesa mungu humbariki mtu kwa kwa kazi unayofanya hizo baraka za kuoa mke zinatoka wap
 
Acha kudanganya watu baraka zinakuja kwa kufanya kazi kwa bidii na kuwa na nizamu ya pesa mungu humbariki mtu kwa kwa kazi unayofanya hizo baraka za kuoa mke zinatoka wap
Hakuna kitu kinachoitwa baraka wala laana.

Usipotumia akili utaumia no soft game in life

Hakuna jambo baya kuishi kwa kutegemea IMANI
 
Back
Top Bottom