Usijidanganye kuwa ukioa mwanamke atakuja na baraka ya kipato chako kuongezeka

Usijidanganye kuwa ukioa mwanamke atakuja na baraka ya kipato chako kuongezeka

N.B No soft game in life , PROTECT YOUR LIFE, SAY NO DEMONSTRATION❌
 
Ukipata Mwanamke anayekupenda na mnapendana.
Oa hata kama Hauna kazi. OA.

Mkipendana ndoa na familia yenu lazima iende tuu na lazima mpige hatua.

Lakini kama hujampata anayekupenda, na huna unayempenda hata uwe kama Elon Musk usijejiingiza kwenye ndoa au kuanzisha familia

Ndoa inahitaji
I) watu wanaopendana.
ii) Watu wanaosikilizana na kuelewana.
iii) Watu walioamua kuishi na kufanya Maisha pamoja.
Pesa na Mali huja baadaye sana.

Kwa hili binafsi ninaushahidi.
Kaka angu mmoja alioa ilifika kipindi ALIKUA anashindia uji wa chumvi na mkewe, Kuna watu wana zari na ndoa Yani demu mkali kama huyo unamshindisha uji wa chumvi na anarixika mpaka Leo bado wapo pamoja na washa Jenga wanaishi vizuri tu
 
Kaka angu mmoja aliona ilifika kipindi ALIKUA anashindia uji wa chumvi na mkewe, Kuna watu wana zari na ndoa Yani demu mkali kama huyo unamshindisha uji wa chumvi na anarixika mpaka Leo bado wapo pamoja na washa Jenga wanaishi vizuri tu
Kuna kitu kingine ambacho wewe haukijui ni siri yao...
 
Kuoa hakuna uhusiano wowote ule na maisha kuwa mazuri au mabaya.

Maisha mazuri ni matokeo ya Nidhamu, mbinu sahihi na kutake risks
Hakuna kingine hapo.
sahihi mkuu, ukweli ni kwamba watu wengi huanza kutake risk na kuwa na nidhamu baada ya kuoa hivyo kuona kama mke ndo kamletea baraka. na hufanya hivyo coz wanakuwa hawana option nyingine ya kusolve changamoto za familia
 
Nilishawahi kusema hiyo kitu mda mrefu. Tafuteni thread yangu yenye title: Kuna delusional theory imesambaa kwenye jamii za kiafrika kwamba ndoa inafungua milango ya mafanikio.

Umeongea ukweli ndugu yangu lakini kuna kitu tunakisahau nafikiri uenda ikawa moja ya sababu taasisi ya ndoa kuendelea kupolomoka.

Bado tunaishi katika fikra za kizamani kwamba mwanaume ndie anawajibika kubeba mahusiano/ndoa kifedha. Tupitia narrative hii tunatengeneza fikra kwenye akili za wanawake kwamba wanapoingia kwenye mahusiano au ndoa basi hela au mali zinazotakiwa kutumika na wote ni zile za mwanaume tu, kwamba hata kama mwanamke akiwa nazo basi kuchangia iwe hiyari sio wajibu.

Katika jamii ya usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa mwanaume na mwanamke, mawazo ya kwamba mwanaume ndie anatakiwa kuwa the only provider hayana mantiki. Mawazo kama hayo ni sababu ya ndoa kupolomoka na vijana wengi kiume kugoma kuoa maana mwanamke anaonekana liability.

Tusome shule moja, chuo kimoja, tusajiri wote ajira portal, tukipata kazi tulipwe mshahara kwa scale inayolingana halafu mwanaume nibebe jukumu la kumuhudumia mwanamke na mahitaji yote ya nyumbani. Sasa yeye hela yake inaenda wapi. Kuna umuhimu gani wa kumwezesha mwanamke awe na elimu na kipato kama mwishoe mwanaume atalazimika kulipa bill zote wakati anachokipata in-return ni sex? Kijana anaona bora akanunue dada poa tu.
We jamaa ni mkweli.
 
Kama hujaoa kwa nia sahihi huwezi kuliona hilo, ila take it from me baraka ipo kubwa sana.

Pia huondoa mawazo mengi ya kipuuzi ambayo kijana ambaye hajaoa anakuwa nayo, ukioa kichwa kinakuwa focused kuliko kawaida.

La muhimu kuoa kwa nia sahihi
Hakuna baraka hapo
Ni hivi, ukioa akili inachamngamka kujua sasa sio wewe tu, bali kuna mtu mwingine kwenye bajeti yako, kwa hiyo unachakarika kupata mara mbili ya ulichokuwa unakipata, hakuna baraka hapo
Na unapoleta kiumbe kingine, maana yake sasa fanya kazi mara tatu kwa kuwa mko watatu, ugumu uko wapi hapo?
 
Back
Top Bottom