Usijidanganye kuwa ukioa mwanamke atakuja na baraka ya kipato chako kuongezeka

Usijidanganye kuwa ukioa mwanamke atakuja na baraka ya kipato chako kuongezeka

Kuna hii imani ya kishirikina kuwa hata kama huna hela UOE kwa sababu mwanamke huja na baraka ya kipato. Ni upuuzi mtupu. Hakuna kitu kama hicho. Usiishi kwa kutegemea miujiza. Jiambie ukweli kuwa unapooa gharama za maisha zitaongezeka kwasababu ya jukumu jipya la kuhudumia mke na baadae watoto.

Unajua gharama za matibabu hospitalini? Hizo ni hatari kuliko gharama zingine zote nyumbani ikiwemo kulipa ada za shule. Sasa ukioa hizo utakutana nazo. Mimi ninashauri watu waoe wakiwa angalau na mwelekeo wa kuwa sawa kiuchumi.
Mwanamke asiye na akili kama wewe siwezi kumuoa.

Atakaye kuoa atakuwa kapata hasara kupitiliza, unaendekeza sana uchawa.
 
Ukipata mwanamke sahii ni baraka. But ukipata mwanamke asie sahihi ni mkosi
 
Ukipata Mwanamke anayekupenda na mnapendana.
Oa hata kama Hauna kazi. OA.

Mkipendana ndoa na familia yenu lazima iende tuu na lazima mpige hatua.

Lakini kama hujampata anayekupenda, na huna unayempenda hata uwe kama Elon Musk usijejiingiza kwenye ndoa au kuanzisha familia

Ndoa inahitaji
I) watu wanaopendana.
ii) Watu wanaosikilizana na kuelewana.
iii) Watu walioamua kuishi na kufanya Maisha pamoja.
Pesa na Mali huja baadaye sana.

Kwa hili binafsi ninaushahidi.
Chai
 
Unamchukua mwanamke nyumbani kwao unamleta kwako muishi pamoja unatumia gharama kubwa kumuhudumia kwa kila namna halafu anageuka kuwa pasua kichwa.

Mara achepuke akuletee magonjwa au watoto wasio damu yako.Kuna wanawake wengine ni hovyo kabisa, hata kile kipato kidogo cha familia anadokoa kuhonga vibenten.

Hata ukiwa na hela kuishi na mwanamke kunachangia kupunguza maisha ya mwanaume.
Ww huchepuki!?
 
Kikubwa oa mtu sahihi anayeweza kusimamia mambo yako wewe unapokua kwenye mihangaiko mingine
 
(A) 1+0=1 mume +mke=1
Mke ambaye sio sahihi.

(B) 1+1=2. Mume +mke =2
Mke sahihi..

That's it.
 
Ukizaa watoto wengi ambao hauna uwezo wa kuwalea na kuwapa maisha ujue unakuwa umewasadia wachina na wahindi kupata vibarua
Hata ukiwa na uwezo ukawasomesha utakuwa umesaidia chama cha kijani kupata chawa
 
Kuna hii imani ya kishirikina kuwa hata kama huna hela UOE kwa sababu mwanamke huja na baraka ya kipato. Ni upuuzi mtupu. Hakuna kitu kama hicho. Usiishi kwa kutegemea miujiza. Jiambie ukweli kuwa unapooa gharama za maisha zitaongezeka kwasababu ya jukumu jipya la kuhudumia mke na baadae watoto.

Unajua gharama za matibabu hospitalini? Hizo ni hatari kuliko gharama zingine zote nyumbani ikiwemo kulipa ada za shule. Sasa ukioa hizo utakutana nazo. Mimi ninashauri watu waoe wakiwa angalau na mwelekeo wa kuwa sawa kiuchumi.
Kipindi nataka kuoa nilikuwa na simamia biashara ya boss fulani mji fulani.
Baada ya kuoa tu na ndoa kuanza kutangazwa tu niliitwa kufanya kazi mgodini kama miner Trainer na badae nikajifunza machine kadhaa za underground nilianza na basics ya 546k ukiweka na makolo kolo mengine take home nilikuwa sikuwa laki9 na unyama kidogo.

Baada ya kujifunza machine mojawapo na kubadilishiwa Title kutoka miner trainer hadi op nilikuwa sikoswi take home m3 na unyama kadhaa.

Badae tena nikavuka hapo hadi .............. je hii sio baraka maana sikutegemea nitakuja kulipwa hivyo wala kupata nafasi hiyo mgodini.

Boss alikuwa ananilipa laki1 tu kwa mwezi.Nimemaliza ku sign mkataba ndoa imebaki na siku3 tu hapohapo nikawepa mkwajaa m1 chap.

Mkuu baraka zipo. sema wewe ulioa mwenye nuksi zake mimba katoa ana janaba na majasho ya kila mwanaume bikira ndo kabisa hata wewe hukuitarajia kutoka kwakwe je mwanamke kama huyo kama huongezi mabalaa ni nini?
 
Nilishawahi kusema hiyo kitu mda mrefu. Tafuteni thread yangu yenye title: Kuna delusional theory imesambaa kwenye jamii za kiafrika kwamba ndoa inafungua milango ya mafanikio.

Umeongea ukweli ndugu yangu lakini kuna kitu tunakisahau nafikiri uenda ikawa moja ya sababu taasisi ya ndoa kuendelea kupolomoka.

Bado tunaishi katika fikra za kizamani kwamba mwanaume ndie anawajibika kubeba mahusiano/ndoa kifedha. Tupitia narrative hii tunatengeneza fikra kwenye akili za wanawake kwamba wanapoingia kwenye mahusiano au ndoa basi hela au mali zinazotakiwa kutumika na wote ni zile za mwanaume tu, kwamba hata kama mwanamke akiwa nazo basi kuchangia iwe hiyari sio wajibu.

Katika jamii ya usawa wa kijinsia na fursa sawa kwa mwanaume na mwanamke, mawazo ya kwamba mwanaume ndie anatakiwa kuwa the only provider hayana mantiki. Mawazo kama hayo ni sababu ya ndoa kupolomoka na vijana wengi kiume kugoma kuoa maana mwanamke anaonekana liability.

Tusome shule moja, chuo kimoja, tusajiri wote ajira portal, tukipata kazi tulipwe mshahara kwa scale inayolingana halafu mwanaume nibebe jukumu la kumuhudumia mwanamke na mahitaji yote ya nyumbani. Sasa yeye hela yake inaenda wapi. Kuna umuhimu gani wa kumwezesha mwanamke awe na elimu na kipato kama mwishoe mwanaume atalazimika kulipa bill zote wakati anachokipata in-return ni sex? Kijana anaona bora akanunue dada poa tu.
 
Back
Top Bottom