Usiku ni wa kupumzika, kwanini bado tunakesha?

Usiku ni alama ya utambuzi kati ya mtu anayeishi katika Comfort zone na yule aliye katikati ya vita ya kubadili sura ya maisha yake na majina ambayo alishaitwa na mengine yakisubiri wakati yaje zamuni.
Aiseeee sawa
 
Tunakesha usiku kwa sababu ya mwingiliano wa majukumu ya kimaisha, changamoto za kisaikolojia, na mabadiliko ya teknolojia yanayovuruga mfumo wa asili wa miili yetu.
Ingawa usiku uliumbwa kibaolojia kwa ajili ya kulala na kuufanya mwili ujijenge upya, mwanadamu wa sasa anakabiliwa na mambo mengi yanayomfanya aendelee kuwa macho.
 
Sahihi
 
Hayo ni maisha ya kukariri tu. Ni sawa na tulishakariri kuwa lazma mtu anywe chai au uji asubuhi. Kulala sio lazima ulale ucku ndugu yangu na ndio maana watu wanakosa ucngizi ucku coz mda mwili ulihitaji ulale ulikuwa unapambana na matv au tusema kazi. Na ndio maana watu sasa hivi bp ni nje nje, sukari ni ya kufikia.
Mfano umetoka kazini saa12 upo nyumbani unaweza ukaoga ukala hadi saa 4 uamke ule ukae hadi saa sita ulale tena hadi saa11 uamke ujiandae kwenda kazi na sio kuzoeasha mwili ati by saa nne tano upo kitandani na mchana mwili ulikuhitaji uupumzishe ukaenda kula makonyag na washkaji.
Unaweza kuishi maisha ya kiafya ukitaka mfano asubuh badala ya chai kula matunda kama mgonjwa, mchana kula heavy meal afu jion kunywa chai ulale na utalala tena vizuri sana tena usingizi mzito. Ikifka sa kumi na moja ile umeamka kunywa uji uende kutafta riziki na kuhusu kulala ukiamua unaweza usilale had pale mwili utahitaji kulala wenyewe.
 
Ahaaa kumbe sawa mkuu asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…