Nitaenda Misaa yaTatu
JF-Expert Member
- Apr 14, 2025
- 403
- 812
Mapendo Daima.
Mwanzoni mwa miaka ya 2000 nikiwa na umri wa miaka 10 Famili yetu ilipatwa na tukio kubwa lenye kuacha historia kubwa sana. Tukio la kinyama ambalo daima tulikuwa tuna sikia tu kwa wengine.
Majira ya saa12 jioni jua likielekea kuzama nikiwa mimi na wadogo zangu wa3 tukirudisha ng'ombe kutoka machungani ndipo nilipomkuta bibi yangu akiwa amelala kifudifudi na damu nyingi sana sana zimechuruzika na kuganda ardhini na kwenye mwili.
Wadogo zangu waliingiwa na butwa kubwa na mimi pia mshangao mkubwa ulinipata ndipo niliposogea zaidi na kugundua kuwa bibi amekatwa na panga sehemu mbili kichwani na kwa muonekano huo nilijua wazi bibi kafariki.
Wadogo zangu wakiwa hawajui wafanyanye nini mimi nilikimbia hadi shamba walilokuwa wakubwa zangu nikawapa taarifa hima mbiombio nao walifika wasiamini macho yao.
Hatimae giza likaingia tulijaribu kumuamsha bibi pale lkn hakuamka kabisa licha ya wote hakika tulijua kuwa kashafariki. Mmoja wetu kati ya wanafamilia alianza kupiga kelele akiomba msaada ndipo majirani walianza kuja na hatimae taarifa zikampata mwenyekiti wa mtaa/kitongoji.
Yowe lilipigwa then tukawekwa mtu kati kuanza kuelezea kwa sababu mimi ndo nilikuwa mtu wa kwanza kabisa kuona maswali kadhaa niliulizwa na pale maswali yalipozidi niliwaomba niende nikamwamshe bibi huenda ataamka maana nilijihisi mimi ndo mtuhumiwa NO1.
Siku hiyo sikulala wala wengine wote hawakulala yowe lilikuwa kubwa mno watu walisambaa huko na kule wakipga yowe.Watu walizidi kuwa wengi mno zaidi ya vijiji vitatu vilikusanyika.
Kesho yake polisi walikuja na kama kawaida nikawekwa mtu kati tena kueleza ilikuwaje.Basi ule usiku mtendaji alikuwaa ameniita pembeni na kunifundisha namna sahihi ya kuja kuwaambia polisi ili nisichanganye mafaili.
Police walinihoji baada ya mimi wakawahoji na wazazi kisha kuondoka nao moja ya swali nililo ulizwa ni kuwa tuna mashaka na nani kwakweli sikuwa na jibu japo bibi alikuwa na tuhuma za uchawi hasa shuleni nilikuwa naambiwa sana na kuogopwa na watoto wenzangu kuwa huyo usimpige bibi yake ni mchawi.
Wazazi walirudi na kwakweli hatukujua hasa ninani alifanya tukio kubwa la kinyama kwa bibi yetu. Bibi hata kama kweli alikuwa mchawi lakini kwenye familia yetu hakuwa na madhara.
Leo hii mimi mtu mzima na kamwe hilo tukio sijawahi kuliona jepesi katika maisha.Tumefiwa n ndg marafiki nk lakini tukio la bibi limebaki kuwa zito zaidi maisha mwangu japo lina zaidi ya miaka 20.
Bibi alishambuliwa na kuuliwa kinyama akiwa anaandaa chakula cha jioni na chote kilijaa na kutapakaa damu tupu.
RIP BIBI