Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Junior ni Mholanzi mwenye asili ya Tanzania. Wazazi wake walihamia Uholanzi wakiwa bado vijana. Maisha yake yote Junior ameishi Amsterdam. Alikuja Tanzania kwa mara ya kwanza akiwa na miaka mitano.
Baada ya sherehe yake ya kuzaliwa akifikisha miaka 18, babu na bibi walimnunulia tiketi aje awaone. Junior alibeba misikoto kama mitatu ya bangi, jambo ambalo huko kwao ni sawa kabisa kama si ya kuuza ni kwa matumizi binafsi.
Junior alipotua Tanzania aligundulika kuwa na misokoto. Alipoulizwa alisema ni kwa matumizi yake binafsi. Aliwekwa chini ya ulinzi. Usiku wa kwanza babu hakufanikiwa kumtoa na alilala Keko.
Tuwaeleze vijana wetu wanaozaliwa Ughaibuni sheria za Tanzania kuepusha matatizo kama haya.