Usikubali kusaini nyaraka hii unapopekuliwa na Polisi

Mimi naona ameelezea vizuri. Kuna upekuzi mwingine unafanyika ili kupandikiza ushahidi wa uongo. Fikiria askari ana kusearch na katika kufanya hivyo anaonesha ulikuwa na bangi ilhali sio kweli! Utakubali kusign?
Huyu ni Wakili kweli? Nina mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini.
 
Asante sana Mkuu kwa Elimu yako Muhimu ya Kututahadharisha kwani huenda Wengine kwa Upopoma wetu uliotukuka tungesaini tukiamini ndiyo tunaonyesha Ushirikiano Kwao kumbe tunaonyesha Ushirikiano wa kwenda kuanza Maisha mapya Jela ( Gerezani )
 
Huwi kwenye anga zao unakuwa kwenye anga zako

Upekuzi hufanyika nyumbani kwako, ofisini kwako nk kwahiyo huwezi kubisha kusaini nyaraka zilizokutwa ofisini kwako wakati hakuna namna ya mtu mwingine kuziingiza

Hapo utakuwa umejitakia kipigo
 
Shukrani wakili. Bora usisaini hata ukikutwa nacho ili mahakamani uwe na pakuanzia kujitetea.
 
Na unaweza kukataa kusaini lakini endapo ni kweli kitu hicho kimekutwa kwako, polisi wanaweza kutumia njia nyingine kama kupiga picha au video ikionyesha mazingira ya hapo kilipokutwa. Siku hizo ele tro onic evidence ipo admissible mahakamani
 
Huyu ni Wakili kweli? Nina mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini.
Umeniwahi mkuu, mwenyewe nimemshangaa sana, sasa kama umekutwa na hizo mali unaanzaje kukataa?, na je wasipokuja na hiyo form wakaenda kujaza wanavyojua wao utamlaumu nani,? Hapa wambie watu kwamba ile form isome vizuri na hakikisha kilichoandikwa ndicho ulichokutwa nacho ndio utie sahihi sio kusema asisaini.
 
Mkuu hiyo haikupi nguvu kisheria,
 
Shukrani sana mkuu nimekuelewa
 
Uko sahihi kabisaa kama amekuja kujitangaza hapa na uwakili wake ni dhahiri ajitafajari upya unapotoa ushauri ni lazima ujiridhishe ukamilifu wako katika swala unalolitolea ushauri sasa unakuja hapa na mihemko yako na kujaza watu ujinga.
Lakini mbona kasema wazi kuwa ... 'ukiona kitu kisichokuwa chako hata kama ni kidogo kama pipi ama sindano usikubali kusaini'...

Hapo hajaesema ukatae tu 'mazima' kusaini fomu hiyo hata kama vitu vilivyoorodheshwa katika fomu ni vyako.
 
Asipoelewa basi, tena sasa hivi wameenda mbali zaidi huyo independent witness asiwe mwenyekiti wa mtaa awe mtumishi wa serikali kama vile mwl mkuu, afsa mtendaji nk. Hii ni kuepusha hawa wenyeviti wanaweza kuwalinda wapiga kura wao. OVA
 
Huu uzi nlijua tu lazima Mapolisi (Mapongo) lazima waje kupinga wakati Wakili kaeleza vizuri kabisa na mfano wa kesi kamili katoa... Toa hoja sio mnaleta mipasho
 
Unawajua Polisi wa Tz? Hujakaa sawa una mbata moja inakukalisha chini, ile unataka kujua ni yupi kakupiga unapigwa katafunua moja halafu unapewa pen usaini.
Hapo utajipima mwenyewe.
 
Barikiwa sana Wakili. Ukija uje na jinsi ya kujilinda na kesi za trafiki wa barabarani. Vipi ile kesi ya makampuni ya simu ulifanikiwa kututetea wachumia juani.
 
Huyu ni Wakili kweli? Nina mashaka na uwakili wake!! Upekuzi umefanyika kwa kufuata taratibu na sheria halafu mtu akatae kusaini.
Umeelewa hata kilichoandikwa? Labda nimekwenda mbali, umesoma hicho kilichoandikwa ??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…