SEHEMU YA KUMI NA NNE
Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,,,
Basi nikachkua boda pale buku paka kisongo, nikaulizia gest pale nikaelekezwa gest moja maeneo yale, nikafika nikaulizia chumba nikaambiwa single elf 5 nikasema fresh, basi nikapewa chumba nikaeka begi langu nikaenda kuoga, nikatoka nikaenda kucheki msosi huko road,nikala nikarudi zangu room, nikajilaza kitandani nikampigia Sity tukaanza kupiga story
Endelea,,,,,,,,,,
Nikakaa pale gest paka ijumaa ifike, ila nikawa natoka naenda kutembea tembea kuangalia maisha ya huko yanaendaje, Basi ijumaa ikafika, nikadamka mapema sana ili niwahi pale kiwandani, kweli nikafika pale,
Ebwanaee!! nikakuta nyomi la kutosha hapo nje, nikajiuliza hawa wote wanatafuta kazi? Duuuh!! Hatari, Basi tukakaa pale, badae wakaja viongozi kuandika majina, kumbe paka jina lako liandikwe inabidi upigane kishenzi, yaani ni kusukumana na utaje jina kwa nguvu paka lisikike,
Daah basi nikafight pale kidume paka jina langu likaandikwa, nikarudi nyuma nikatulia naangalia wengine wanavyopigana, Mwisho wakasema kwa leo inatosha, wengine siku nyingine, wakaondoka na yale majina yetu,
Basi watu wakatawanyika tukabaki sisi tulioandikwa majina, Badae wale viongozi wakarudi, wakaanza kuita majina, ukiitwa jina unaingia ndani, Basi nikaskia jina langu nikaingia ndani, badae tukachukuliwa paka kwenye darasa hivi, tukaanza kupewa maelezo ya kazi,
Tukaambiwa pale mshahara ni laki na nusu, Humo ndani kuna nyumba kwaiyo kwa atakae taka utapewa pa kukaa humo ndani ila utalipia kodi, umeme na maji, aliye tayari mikataba ipo pale tujaze,
Daah sa mi nikatae naenda wapi, Nikawa sina jinsi mtu mzima nikaanguka saini pale, Basi tukachukuliwa tukapelekwa kwa watu wa usalama kazini wakatupa induction pale,
Tukatolewa tukapelekwa kwa mlezi ili atuandikishe na atupangie vyumba, Basi bana hilo likiwanda ni likubwa balaa, yaani huko ndani ni pakubwa unaweza tembea usimalize, humo ndani kuna nyumba za kutosha,zipo ghorofa, zipo za kawaida, kuna maduka kuna baa, yaani ni mji kabisa na ukiwa nje huwezi amini kama humo ndani kuna mji mkubwa hivyo,
Basi tukapangiwa chumba, yaani utafikiri shule, chumba kina vitanda double, mnakaa wa nne chumba kimoja, Basi mlezi akatuchukua akatupeleka sehemu akaaza kutupa sheria za kukaa mule ndani,
Basi badae tukapewa vitambulisho, yaan kama kikadi hivi kimekunjwa huko ndan ni vijedwali vya tarehe, kila siku supervisor wako anatakiwa asaini kibox kimoja kulingana na tarehe husika paka mwezi uishe utapewa kingine, Tukambiwa bila hicho huwezi kuingia wala kutoka mule kiwandani, hata uwe unafahamika,kwaiyo tuvitunze kama mboni ya jicho,
Basi tukaambiwa twende vyumbani badae tutaitwa chakula kikiletwa, kesho ndo tutapelekwa huko kiwandani kwenye kazi, Kweli badae msosi ukaja,tukapanga foleni tukapakuliwa makande pale tukala, jioni tena hivyo hivyo, basi siku ikaisha hivyo,
Kesho yake asubuhi tukapelekwa huko ma idarani kulingana na ulivyopangiwa, mimi nikapelekwa idara ya kuweka rangi kwenye nguo inaitwa dying, Basi nikakabiziwa kwa kiongozi wangu yeye ndo atakuwa ananipangia kazi na pia kusign kitambulisho changu,
Basi kazi ndo ikawa imeanza hivyo, mule ndani kuna matanki ya kuchanganyia rangi, kuna joto balaa, yaani ukiingia asubuhi paka utoke jioni umeiva,na hapo katikati huruhusiwi kutoka hata hapo nje paka upate ruksa, mzee si mchezo,
Basi tukapiga kazi pale mwezi ukakata nikapewa hela yangu pamoja na makato yote nikapewa lak na 20, Nikasema kwa maisha haya hamna kutoboa, hapa ni kusukuma siku tu ili mradi usife ila kwa maisha hamna maisha hapa,
Nikaona nibora nipige tu huku nacheki mishe nyingine kuliko kukaa bure, Basi nikapiga pale miezi ikakata, baada ya kuzoea mazingira nikajaribu kuwatafuta wale jamaa zangu ila nikapata habari walishatambaa kitambo sana baada ya kuona mshahara mdogo, Basi nikapeleleza pale kama kwa vyeti vyangu vile naweza kupata kazi ya maana ila nako nikaona giza tu, Alafu hata hao wenye kazi nnazoona za maana mishahara yao midogo vilevile,
Siku moja nipo room ilikuwa jumapili watu wameenda zao town nimebaki mi na jamaangu pale room tunapiga stori, nikamsimulia bwana kwamba mi nimesomea uinjinia sema sababu ya tatizo la ajira ndo maana nipo pale, daah jamaa akasikitika sana, ila akaniambia pale wapo watu na fani zao,kuna walimu,madaktari,wanasheria ila kwa vile kazi hakuna wapo pale wanapiga mzigo kama mimi kwaiyo nisjilaumu, akasema hata kaka yake na yeye alisomea uinjinia akatafuta kazi sana akakosa, bahati akapata shule moja pale moshi anafundisha kidogo analipwa fresh, nikamuuliza shule gani hiyo akasema inaitwa majengo secondary ipo moshi,
Basi nikawa interested na hiyo shule, labda niende na mimi nnaweza kubahatika, Nikapanga siku moja nitaenda,
Kweli nikajipanga siku hiyo kesho yake ilikuwa off yangu kwaiyo siingii job, basi nikajipanga ili kesho niende huko moshi,
Kweli kesho ikafika, Daah ni siku ambayo sitakaa niisahau maishani mwangu, yani yaliyonipata siku ile ni Mungu tu aliingilia kati, daah!! We acha tu, Basi bana siku ilianza fresh tu yaani,kulipambazuka vizuri nikajiandaa pale niende zangu moshi,
Itaendelea