Usilolijua ni kwamba Aron Kagurumujuli amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutoka Wilaya ya Kinondoni

Usilolijua ni kwamba Aron Kagurumujuli amechaguliwa kuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa kutoka Wilaya ya Kinondoni

..Ccm mnaharibu nchi.

..mmejaza watu wa hovyo kama Karugumjuli kila mahali ikiwemo polisi, tiss, mahakamani etc

..hii nchi ni yetu sote.
 
Sawa alikuwa mkurugenzi wakati ule Akwilina alipouwawa. Sasa yeye kushiriki chaguzi za CCM kama mwanaCCM kunq ubaya gani? Je kama alishastaafu utumishi wa umma?

Acheni siasa njaa bana.View attachment 2381711
Damu ya binti huyu itamlilia na kumuandama muda wote wa maisha yake, ni lazima itafika muda naye yatamfika majanga makubwa tu.
 
Kwa wageni wa JF ama labda na Wenyeji lakini Wasahaulifu , Aron Kagurumujuli alikuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni , aliyeshiriki kikamilifu kutokomeza Demokrasia na kuhusika kwa Udi na Uvumba kwenye Mauaji ya Akwilina , Mwanafunzi wa chuo cha NIT , aliyepigwa risasi na Polisi na kupasuliwa kichwa ndani ya Daladala , kwenye Mauaji ambayo walengwa hasa walikuwa viongozi wa Chadema , Kagurumujuli alishirikiana Kikamilifu na RPC wa Kanda Maalum aliyeitwa Lazaro Mambosasa .

Hadithi hii ni ndefu sana , na nina hakika kwa dondoo hizo hapo juu angalau nimewakumbusha jambo .

Bali itoshe tu kusema kwamba Kagurumujuli , aliyekuwa Msimamizi wa Uchaguzi unaoandaliwa na Tume ya Uchaguzi , Amechaguliwa kwa kishindo kuwa MJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM TAIFA kutokea Wilaya ya Kinondoni , kwa tafsiri ya haraka , inaonyesha kwamba wanaccm wa Kinondoni wamemlipa Kagurumujuli kwa kazi nzuri ya kukisaidia chama chao na kushiriki mauaji ya Akwilina .

#Katiba mpya ni sasa
Kukichwa kutapambazuka... Mungu ibariki CHADEMA
 
Back
Top Bottom