Ikiwa itabidi uwe na mawasiliano na mke wa mtu basi yawe kwa heshima na umbali na yasikaribie mipaka ya vishawishi.
Mi nimeshajiwekea sihitaji ukaribu na mke wa mtu yeyote hata awe rafiki yangu wa karibu kwa sababu kuu mbili.
1. Ukiwa karibu na mke wa rafiki yako wa karibu sana, jiandae kwa lolote mke wake akigundua jamaa yake anachepuka, huyo shem naye atakuweka kundi moja na jamaa yake, na ataona wewe unamlindia jamaa siri zake.
2. Kuna mashem wengine ukishakuwa karibu naye na akagundua jamaa yake anachepuka, yeye analipiza kwa kuja kukupa utelezi. Kwenye hili niliponea chupu chupu kwa mke wa rafiki yangu Mtu wangu wa karibu sana, aliyenifanyia mambo makubwa sana zaidi hata ya ndugu. Huyu bidada alikuja kugundua jamaa yake ana mchepuko ambaye hadi jamaa alimjengea nyumba na kumpa gari. Nilikuja kugundua shem ananiuliza maswali ya ki FBI, sema bahati na mimi nilikuwa sijui maana jamaa alikuwa msiri sana. Baadaye shem akanifungukia kuwa ana ushahidi ila akawa anashindwa aanzie wapi. kuanzia hapo akaanza kuwa karibu na mm kila wakati ananipigia simu especially jamaa anaposafiri. Kuna kipindi mwanamke alikuja Dar akiwa anadrive gari, alipofika mjini akaniomba nimsaidie kumtembeza Dar anaogopa kuendesha gari Dar. Kwenye story za hapa na pale nikagundua kuwa yupo tayari nimle. Nikafanya juu chini kumkwepa.
Aliporudi mkoani ikawa ananipigia video call akiwa kitandani. Nako nikakwepa. kuanzia hapo hadi leo hajanitafuta tena