Usimkatie tamaa mtu..! Zikiisha akili humrudi.. Hiari yashinda utumwa!

Usimkatie tamaa mtu..! Zikiisha akili humrudi.. Hiari yashinda utumwa!

Naona mnajitekenya na kujichekesha wenyewe kama Mazuzu. Kila kitu kudakia na kujifariji tu . Ma CHADEMA huwa hamjitambui kabisa na huwa hamjui mnataka nini. Umbeya , upashikuna na ushakunoko ndio vinawasumbua. Mnashindwa kufanya kazi badala yake mnakalia kupiga Majungu kutwa nzima.

Wewe endelea na kazi yako ya matunguli na uganga wa kupiga malamli.
Chizi karogwa tena!
downloadfile.jpg
 
tuombee tu Mungu western powers waingilie watusadie kumuondoa (whatever the cost), hiyo ndiyo salama yetu, damage ambayo ameifanya na anaendelea kuifanya kwenye nchi yeu ni kubwa sana na itachukua muda mrefu kuirekebisha if we are lucky, wamebomoa elimu yetu, taasisi zote wameua, hivyo salama yetu ni western powers kuingilia kutuokoa.

ni rahisi kubomoa klk kujenga, sasa hivi wana undo system yote iliyokuwepo na iliyopfanya kazi kwa miaka zaidi ya 100 na kuweka islamic ambayo ushahidi uko wazi hakuna nchi ya islamic sharia inayaifanya vizuri duniani, irani ndiyo hiyo wairani wote walioweza wameikimbilia islamic republic na ni pamoja na familia za mullahs wanaishi western countries, pakistan na afghanstan hakuna mtu anayependa kwenda kuishi huko na kila anayeweza anakimbia hizo nchi, sasa wanaleta uncivilized barbaria somalis kwenye nchi yetu mpaka bungeni ...
 
Ameandika Mch. Peter Msigwa
Historia inaonyesha:

Mataifa mengi duniani hayakuanguka kwanza kwa sababu ya vita au mapinduzi bali ,
Yalianza kudhoofika taratibu pale ambapo mamlaka isiyo rasmi inaanza kuogopwa kuliko taasisi rasmi. (Illusion power)

Historia ina mifano mingi sana ya mataifa yaliyodhoofika si kwa sababu ya adui wa nje kwanza bali kwa sababu ndani ya mfumo wao, mamlaka isiyo rasmi ilikuwa kubwa kuliko taasisi rasmi.

Hapa kuna mifano kutoka ulimwengu wa kale hadi dunia ya kisasa:

1. Dola ya Roma (Roman Empire)

Fall of the Western Roman Empire
Mwanzoni Roma ilikuwa na:
  • Seneti,
  • sheria,
  • jeshi lenye nidhamu,
  • taasisi imara.
Lakini kadri muda ulivyopita:
  • familia za kifalme,
  • walinzi wa mfalme (Praetorian Guard),
  • watu wa karibu na Kaisari,
walianza kuwa na nguvu kuliko taasisi rasmi.

Mfano:
Praetorian Guard waliweza:
  • kumuua Kaisari,
  • kumteua Kaisari mpya,
  • hata “kuuza” ufalme kwa anayelipa zaidi.

Kikatiba?
Haikuwa kazi yao.
Lakini kiuhalisia:
walikuwa na nguvu kuliko mfumo wenyewe.

Roma haikuanguka siku moja. Ilianza kuoza taratibu kutoka ndani.

2. Ufaransa Kabla ya Mapinduzi ya 1789

French Revolution

Kabla ya mapinduzi:
familia ya kifalme ya Louis XVI ilikuwa imezungukwa na:
  • watu wa karibu,
  • wakwe,
  • watu wa ikulu,
  • tabaka la kifahari lisiloguswa.
Wananchi wa kawaida waliona:
  • sheria haikuwa sawa kwa wote,
  • ukaribu na mfalme ulikupa kinga,
  • mfumo ulikuwa wa watu wachache.
Polepole, hasira dhidi ya “invisible power structure” ikakua.

Mwisho wake:
taasisi zikapoteza uhalali mbele ya wananchi.

3. Dola ya Ottoman (Mwisho wa Himaya)

Dissolution of the Ottoman Empire

Katika miaka ya mwisho ya dola ya Ottoman:
  • watu wa ndani ya kasri,
  • familia za kifalme,
  • washauri binafsi,
  • makundi ya kijeshi,
walianza kuwa na ushawishi mkubwa kuliko taasisi rasmi za serikali.

Sultani alizidi kutegemea:
“inner circles” kuliko mfumo wa kitaifa.

Taasisi zikaanza kudhoofika,
rushwa ikaongezeka,
uaminifu kwa dola ukapungua.

Dola kubwa sana ikaanza kuoza kutoka ndani kabla hata haijashindwa nje.

4. Urusi ya Tsar Nicholas II

Russian Revolution

Mfano maarufu ni ushawishi wa Grigori Rasputin.

Rasputin hakuwa:
  • waziri,
  • jenerali,
  • wala kiongozi wa serikali.
Lakini kutokana na ukaribu wake na familia ya kifalme, watu waliamini alikuwa anaathiri maamuzi ya taifa.

Matokeo yake:
  • taasisi zikaanza kuonekana dhaifu,
  • serikali ikapoteza heshima,
  • wananchi wakaanza kuona mfumo mzima umeoza.
Urusi haikuanguka tu kwa sababu ya vita
ilianguka kwa sababu wananchi walikuwa wamepoteza imani na uhalali wa mfumo.

5. Enzi ya “State Capture” Afrika Kusini

State capture in South Africa

Wakati wa utawala wa Jacob Zuma,
familia ya Gupta family ilitajwa sana.

Hoja kuu ilikuwa:
je watu binafsi waliokuwa karibu na mamlaka walikuwa na ushawishi mkubwa kuliko taasisi rasmi?

Wananchi wengi walihisi:
  • teuzi zilikuwa zinaathiriwa,
  • mikataba ilikuwa inaelekezwa,
  • serikali ilikuwa inaanza kutumikia mtandao binafsi.
Kilichoumiza zaidi si tu tuhuma zenyewe
bali perception kwamba:

“Nguvu halisi haipo tena kwenye taasisi.”

Na perception hiyo pekee inaweza kudhoofisha taifa.

6. Libya ya Gaddafi

Muammar Gaddafi

Katika Libya:
watoto wa Gaddafi walionekana kuwa na ushawishi mkubwa sana kijamii, kiusalama, na kiuchumi.

Watu wengi walihisi:
  • mfumo ulikuwa umeunganishwa na familia,
  • ukosoaji ulikuwa hatari,
  • taasisi hazikuwa huru kweli.
Tatizo la mifumo ya aina hii ni kwamba:
kiongozi akiwa imara, mfumo unaonekana imara.

Lakini taasisi zikishakuwa dhaifu,
mara kiongozi akiondoka —
nchi inaweza kuingia kwenye vurugu haraka sana.

7. Ufilipino – Familia ya Marcos

Ferdinand Marcos

Katika kipindi cha Marcos:
familia ya kwanza ilianza kuwa kitovu cha:
  • biashara,
  • siasa,
  • ushawishi wa taifa.
Mke wake Imelda Marcos akawa ishara ya namna ukaribu na mamlaka ulivyoweza kuzalisha nguvu zisizo rasmi.

Wananchi walipoanza kuona:
  • familia iko juu ya mfumo,
  • sheria si sawa kwa wote,
imani kwa serikali ikaanza kufa.

8. Korea Kaskazini (Mfumo wa Kifamilia)

North Korea

Hapa tunaona mfano wa wazi kabisa ambapo:
familia yenyewe imekuwa karibu sawa na taifa.

Utii kwa taasisi mara nyingi umechanganyika na:
  • utii kwa ukoo,
  • ibada ya viongozi,
  • mythology ya kisiasa.
Mfumo unategemea sana:
hofu, taswira, na nguvu ya kisaikolojia.

Somo Kubwa La Historia

Karibu mifumo yote iliyodhoofika ilikuwa na dalili hizi:
  • watu wanaoogopa watu kuliko sheria,
  • ukaribu na mamlaka kuwa muhimu kuliko uwezo,
  • taasisi kuwa dhaifu mbele ya personalities,
  • wananchi kupoteza imani kuwa sheria ni sawa kwa wote.
Na hiyo ndiyo hatua hatari sana kwa taifa lolote.

Kwa sababu: taasisi zikidhoofika, taifa linaweza kuonekana imara kwa nje
lakini ndani tayari limeanza kuoza.

Hitimisho

Historia inaonyesha kuwa:
mataifa mengi hayafi kwanza kwa risasi.

Huanzia kufa pale ambapo:
  • sheria inapoteza heshima,
  • taasisi zinaanza kuogopa personalities,
  • na wananchi wanaamini kwamba nguvu halisi ipo kwenye “invisible networks” kuliko kwenye katiba.
Ndipo dola inaanza kubadilika:
kutoka republic → kwenda mfumo wa watu binafsi.

Rev Peter Simon Msigwa
IringaView attachment 3586303
Nachofurahia wakosoaji wengi wa Msigwa ni empty brain. 90% ya wakosoaji wa Msigwa hawana uwezo wa ku analyse kwa ukubwa na kitaalamu kama anavyofanya Peter Msigwa. Weng wao wanachoweza ni ku copy na ku paste ujinga wa wakina Hilda
 
Mkuu Kalamu nawajibika na kichwa cha habari. Hicho ni uhandisi wangu. Maudhui ni Mchungaji Peter Msigwa.. Nakushauri uyasome kuna picha utapata
Kwenye hayo maudhui sijaongeza wala kupunguza hats nukta!
Unanipa adhabu kidiplomasia sana kwa ushauri wako huo.
Kwa heshima, ngoja niikubali hiyo adhabu. Nakwenda kusoma ujumbe toka kwa mtu ambaye namdharau sana kwa ukigeugeu wakwe wa mara kwa mara..

Sina hakika kama nitaleta mrejesho tofauti na ule nilioutoa hapo juu, kabla ya kusoma takataka hiyo..
Usipoona jibu jingine, chukulia kuwa lililopo toka mwanzo linajitosheleza.
 
Amshajikatia tamaa ya kuteuliwa
Tunaona tofauti kubwa hata katika swala hili kati ya Samia na Magufuli. Samia ni kitu tofauti kabisa na Magufuli kwa kila jambo. Sasa sijui aliwezawezaje kujificha hadi kuondoka kwa Magufuli!
 
Unanipa adhabu kidiplomasia sana kwa ushauri wako huo.
Kwa heshima, ngoja niikubali hiyo adhabu. Nakwenda kusoma ujumbe toka kwa mtu ambaye namdharau sana kwa ukigeugeu wakwe wa mara kwa mara..

Sina hakika kama nitaleta mrejesho tofauti na ule nilioutoa hapo juu, kabla ya kusoma takataka hiyo..
Usipoona jibu jingine, chukulia kuwa lililopo toka mwanzo linajitosheleza.
Kwakweli kajishushia heshima mno na haitakaa irudi tena! Nimeamua kusoma andishi lake na kulipandisha hapa ili wengine waone na kuthibitisha yale ambayo tuliyaandika kabla

Je, Msigwa ndani ya CCM ni assert ama ni liability? | JamiiForums Tanzania Je, Msigwa ndani ya CCM ni assert ama ni liability?
 
Bado sijaelewa; pamoja na kwamba hiyo taarifa ndefu sijaisoma!

Ila nimesoma kichwa cha mada na hayo maneno niliyonyanyua na kuyabandika hapo; halafu nikasoma picha iliyoandamana na hiyo taarifa ndefu.

Kutoelewa kwangu ni pamoja na swali: hii taarifa kaiandaa huyo anayeitwa Rev.?

Huyo mtu "asiyekatiwa tamaa ni nani"
Kuna mtu anayeweza kusema kwa uso ulioonyooka kuwa bado anayo matumaini na Samia Suluhu Hassan; maana mada ni kutomkatia tamaa mtu!

Mtu asiyekuwa na akili kama Samia, hizo akili zitamrudi vipi sasa!

Na huyo Rev.? Naye asikatiwe tamaa?

This is asking for too much!

Samahani mkuu Mshana, jr. Sijawahi kuandika maneno ya aina hii kwenye andiko lolote lenye jina lako; lakini leo nadiriki kusema bila ya shaka yoyote: hii ni mada mbovu kabisa.

NA PICHA KAWEKA YEYE; YA NINI SASA!
Mbovu mno

Ila kama kwa hila katafaulu kujua nini watu na husda zao
 
Kwakweli kajishushia heshima mno na haitakaa irudi tena! Nimeamua kusoma andishi lake na kulipandisha hapa ili wengine waone na kuthibitisha yale ambayo tuliyaandika kabla

Je, Msigwa ndani ya CCM ni assert ama ni liability? | JamiiForums Tanzania Je, Msigwa ndani ya CCM ni assert ama ni liability?
Naomba nitoe shukrani kwako kwa kuweka hiyo taarifa hapa JF.
Sijaisoma, na sina nia tena ya kuisoma.
 
Naomba nitoe shukrani kwako kwa kuweka hiyo taarifa hapa JF.
Sijaisoma, na sina nia tena ya kuisoma.
Natambua hivyo brother ni lama mimi ninapoona hotuba za watu fulani
 
Nachofurahia wakosoaji wengi wa Msigwa ni empty brain. 90% ya wakosoaji wa Msigwa hawana uwezo wa ku analyse kwa ukubwa na kitaalamu kama anavyofanya Peter Msigwa. Weng wao wanachoweza ni ku copy na ku paste ujinga wa wakina Hilda
Tatizo ni kwamba "unafurahia" mwenyewe kuwa hata chini ya hao "emppy brain".
Isn't that amazing!
 
Naomba nitoe shukrani kwako kwa kuweka hiyo taarifa hapa JF.
Sijaisoma, na sina nia tena ya kuisoma.
Halafu anakuja mtu hapa ameshiba maharage mazuri ya Ilembula anawabeza Gen Z. Hivi kweli kwa akili kama ya akina Msigwa, sinafadhali nchi wapewe Gen Z na wao wajaribishe, baba na babu zao waliposhindwa?
 
Back
Top Bottom